Serikali: Miaka 2 ya Rais Magufuli, tumeongeza ari na nidhamu kwa watumishi! Mapato yapanda toka trion 9.9 hadi trion 14

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,927


Dkt. Hassan Abbasi anaongea;

abbasi.jpg


"Katika miaka miwili hii tumefarijika kuona watanzania wengi wanaunga mkono mageuzi makubwa nchini"

"Tunajivunia kuongezeka kwa ari na nidhamu kwa watumishi wa umma"

"Mpaka sasa tumebaini watumishi hewa elfu ishirini ambao kama wangelipwa ingegharimu Tzs bil. 236"

"Eneo lingine ni kubaini watumishi wenye vyeti feki 12,000 ambapo kama wangelipwa ingegharimu TZS Bil. 142.9"

"Kwa mwezi Serikali inatumia Tzs Bil. 23 kwa mwezi kwa ajili ya Elimu Bure"

"Serikali ilianzisha Mahakama ya Mafisadi ambapo mpaka sasa kesi 3 za uhujumu uchumi zimeanza kusikilizwa"

"Miaka ya 2014-2015 safari za nje za watumishi na viongozi wa serikali ziligharimu sh. 216 bilioni"

"Miaka miwili ya serikali ya awamu ya 5 safari za nje zimegharimu kiasi kisichozidi sh. 25 bilioni"

"Makusanyo ya mwaka yameongezeka kutoka trilioni 9.9 mwaka 2015 hadi trilioni 14 mwaka 2017"

"Uzalishaji wa madini ya Tanzanite na Almasi umeongezeka kutoka karati 15,000 - 18,000 hadi karati 28,000 - 32,000"

"Kama nchi, safari ya kuelekea kujitegemea tumeshaianza kwa njia nyingi"

"Kwa mwaka 2015, Bajeti ya dawa na vifaa tiba ilikua TZS Bil. 30, kwa miaka 2 bajeti imefikia TZS Bil. 261"

"Katika kipindi cha uongozi wa Rais Magufuli tumefanikiwa kufufua viwanda 17 kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina"

"Tupo kwenye awamu ya mageuzi, vyombo vya habari vinapaswa kuungana na matamanio ya wananchi"

"Mkoani Arusha kuna mradi wa maji wa TZS Bil. 476 unaendelea na mingine ya TZS Tril.1.2 inaendelea katika miji 17"

"Kuanzia mwisho wa mwezi huu watumishi wataanza kuongezewa mishahara na kupandisha madaraja, na kulipwa stahiki zao"

"Katika sekta ya kilimo tumeondoa Tozo na Kodi nyingi zilizokuwa kero kwa watanzania"

"Tumefanya udhibiti katika bei za mazao na juzi tumesikia Mtwara bei ya korosho imefika Tsh. 4100/= kwa kilo"

"Wafanyakazi kwa sasa wanauhakika na misharaha ikifika tarehe 25 ya mwezi hela imeshaingia"

"Kipande cha reli ya kisasa kinachojengwa kutoka Dar hadi Dom kitagharimu TZS Tril 7.1 ikiwa ni fedha za ndani"

"Mradi wa Kinyerezi 2 wa megawati 240 uko katika 84% kukamilika, mtambo wa 1 wa megawati 30 utawashwa Desemba,2017"

"Kuhusu ndege ni kama nilivyosema tunanunua ndege nne, kufika mwakani ndege zote tulizoagiza zitafika nchi"

"Ndege Boing Dreamliner kuwasili July mwakani na zile za c-series kuwasili June mwakani"

"Takwimu za mwaka 2017 za TIC na UNCTAD, katika nchi za EAC, Tanzania inaongoza kwa wawekezaji kutoka nje"
 
  1. "Tunajivunia kuongezeka kwa ari na nidhamu kwa watumishi wa umma"- Nidhamu Yes!
  2. "Mpaka sasa tumebaini watumishi hewa elfu ishirini ambao kama wangelipwa ingegharimu Tzs bil. 236"- CCM iwaombe radhi watanzania.
  3. "Eneo lingine ni kubaini watumishi wenye vyeti feki 12,000 ambapo kama wangelipwa ingegharimu TZS Bil. 142.9"-CCM iwaombe radhi watanzania.
  4. "Kwa mwezi Serikali inatumia Tzs Bil. 23 kwa mwezi kwa ajili ya Elimu Bure"- Big up-Ongezeni juhudi
  5. "Serikali ilianzisha Mahakama ya Mafisadi ambapo mpaka sasa kesi 3 za uhujumu uchumi zimeanza kusikilizwa"- Bado sana. Poor so far
  6. "Miaka ya 2014-2015 safari za nje za watumishi na viongozi wa serikali ziligharimu sh. 216 bilioni"-CCM iwaombe radhi watanzania.
  7. "Miaka miwili ya serikali ya awamu ya 5 safari za nje zimegharimu kiasi kisichozidi sh. 25 bilioni"-rejea Juu
  8. "Makusanyo ya mwaka yameongezeka kutoka trilioni 9.9 mwaka 2015 hadi trilioni 14 mwaka 2017-Good Job-rejea Nidhamu
  9. "Uzalishaji wa madini ya Tanzanite na Almasi umeongezeka kutoka karati 15,000 - 18,000 hadi karati 28,000 - 32,000"-Uzalishaji haujaongezeka bali udhibiti ndiyo ulioleta hatua hiyo.
  10. "Kama nchi, safari ya kuelekea kujitegemea tumeshaianza kwa njia nyingi"- Kungumu kuamini.
  11. "Kwa mwaka 2015, Bajeti ya dawa na vifaa tiba ilikua TZS Bil. 30, kwa miaka 2 bajeti imefikia TZS Bil. 261"- Safi kazeni Buti.
  12. "Katika kipindi cha uongozi wa Rais Magufuli tumefanikiwa kufufua viwanda 17 kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina- Zipi? na Vinahusika na nini?
  13. "Tupo kwenye awamu ya mageuzi, vyombo vya habari vinapaswa kuungana na matamanio ya wananchi"- Hii mbele ya safari itawaangusha sana- Mnaminya uhuru wa Vyombo vya habari.
  14. "Mkoani Arusha kuna mradi wa maji wa TZS Bil. 476 unaendelea na mingine ya TZS Tril.1.2 inaendelea katika miji 17"- ????????
  15. "Kuanzia mwisho wa mwezi huu watumishi wataanza kuongezewa mishahara na kupandisha madaraja, na kulipwa stahiki zao"- ????????????????
  16. "Katika sekta ya kilimo tumeondoa Tozo na Kodi nyingi zilizokuwa kero kwa watanzania"- Safi- kazi zaidi kwenye masoko
  17. "Tumefanya udhibiti katika bei za mazao na juzi tumesikia Mtwara bei ya korosho imefika Tsh. 4100/= kwa kilo"-????
  18. "Wafanyakazi kwa sasa wanauhakika na misharaha ikifika tarehe 25 ya mwezi hela imeshaingia"- ???????
 
Sioni sababu ya kutumia nguvu nyingi kuelezea mambo ambayo yanatakiwa yajieleze yenyewe.

Tuuzieni sukari, wala sio kwa bei ndogo, bali kwa 1,500/= mliyoikuta nayo. Tubadilishieni dola wala sio kwa 500/= bali kwa 1,800/=. Tuuzieni mafuta wala sio kwa 1,000/ bali kwa 1,500/=. Tuwekeeni mazingira mazuri ya kibiashara na kodi rafiki.

That simple; wala hiyo MAELEZO isingehitaji kuwepo "kutoa ufafanuzi".
 
Msemaji wa serikali kupitia TBC muda huu ametoa taarifa kuwa mwishoni mwa mwaka 2015 TRA walifikia shs Trilion 9 kama makusanyo ya kodi kwa mwaka na hadi sasa ni trilion 14 ikiwa ni ongezeko la trilion 5 kwa mwaka.
Bila shaka si jambo la kubeza japo bado kuna pengo kulingana na bajeti ya taifa.
 
tumetokomeza rushwa
tumejenga bomba la mafuta
tumetokomeza wafanyakazi hewa
tumejenga reli ya umeme
tumeimarisha ukabila
tumeua upinzani
tunaendelea kuua uchumi taratibu
tumezibaka mahakama na bunge
tupo chato tunapumzika
.......
.
.
.
kuna lingine kaongea?????
 
Sioni sababu ya kutumia nguvu nyingi kuelezea mambo ambayo yanatakiwa yajieleze yenyewe. Tuuzieni sukari, wala sio kwa bei ndogo, bali kwa 1,500/= mliyoikuta nayo. Tubadilishieni dola wala sio kwa 500/= bali kwa 1,800/=. Tuuzieni mafuta wala sio kwa 1,000/ bali kwa 1,500/=. Tuwekeeni mazingira mazuri ya kibiashara na kodi rafiki. That simple; wala hiyo MAELEZO isingehitaji kuwepo "kutoa ufafanuzi".
Fair enough ....constructive criticism
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom