Serikali: Mchakato wa Katiba Mpya una gharama kubwa! Kipaumbele cha Serikali ni kutoa huduma za jamii kwa Watanzania

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
Wakati watanzania wakihitaji Katiba Mpya na Serikali ya awamu ya nne kuzunguka kutafuta maoni ya Watanzania. Serikali ya awamu ya tano yasema Katiba mpya sio kipaumbele kwa serikali na inagharama

Waziri Mkuu Bungeni leo amesema;

"Swala la Katiba linahitaji gharama kubwa ya fedha na linategemea mapato yanayokusanywa ndani ya nchi. Lakini kila mwaka wa fedha una vipaumbele vyake na sisi tumejikita katika kutoa huduma za jamii kwa wananchi".

"Tumekuwa tukishuhudia watanzania wanahitaji maji kwenye vijiji, kumekuwa na mahitaji ya huduma za afya, elimu inahiatajika kuimarishwa, miundombinu ili kuwezesha watanzania kuendelea na maisha yao"

"Katiba ni muongozo ambao unaelekeza mambo kadhaa, na sasa tunayo katiba ambayo ile ile ingawa tumekusudia kuibadilisha."

"Kwa kuwa tunayo Katiba inaendelea na miongozo ipo na haya ni mapendekezo ya kufanya marekebisho katika maeneo kadhaa lakini mchakato wake unahitaji gharama kubwa na kipaumbele cha serikali ni kutoa huduma za jamii kwa watanzania."

"Kwanza tumeimarisha makusanyo ya ndani ili kuweza kutoa huduma za jamii kwa watanzania, Pale ambapo tutafikia kiwango kizuri cha mapato huku tukiendelea kutoa huduma hiyo."

 
Back
Top Bottom