Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,807
- 11,969
MCHAKATO WA KATIBA MPYA KUTENGEWA FUNGU KWENYE BAJETI YA 2023/ 2024
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro amesema kuwa mchakato wa Katiba Mpya pamoja na maboresho ya sheria ya vyama vya siasa na Uchaguzi unatarajiwa kuanza kufanyiwa kazi baada kupitishwa kwa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Waziri Ndumbaro ameyasema hayo jana Machi 24, 2023 alipokuwa akifungua kikao cha baraza la wafanyakazi la wizara hiyo kilichofanyika jijini Dodoma.
Akizungumzia mchakato wa katiba mpya Ndumbaro alisema kuwa marekebisho yataanza baada ya kupitishwa kwa michakato ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kupitia Baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo na mwisho kuidhinishwa na Bunge.
“Mchakato wa Katiba mpya ni agizo la Rais Samia Suluhu Hassan, hivyo ili kufanikiwa inahitaji rasilimali fedha nyingi na wajumbe wa kikao cha baraza la wafanyakazi mtambue mna jukumu hilo la kupitia mapebdekezo ya baheti ya mwaka huu (2023/2024) ili kufanikisha mambo hayo makubwa ya kitaifa” alisema Waziri Ndumbaro
Ikumbukwe Rais Samia Suluhu Hassan aliagiza Wizara kuanza kujipanga kwa ajili mchakato wa marekebisho ya Katiba. Hata hivyo Rais Samia kupitia kauli yake ambayo aliitoa Machi 8, 2023 kwenye maadhimisho ya siku ya Wanawake aligusia suala hilo kuwa mchakato wake hauwezi kupelekwa haraka haraka lakini Serikali inalifanyia kazi.