Puma yetu
Senior Member
- Sep 23, 2016
- 111
- 125
Kama kuna kitendo kinachoumuza watumishi wengi wa umma ni serikali kuzuia uhamisho kwa watumishi wao, sababu kuu ni kua ati uhakiki wa watumishi bado unaendelea.
Huu ni unyanyasaji wa wazi wazi kabisa, inawezekanaje mtu mke wa ndoa anataka kumfuata mume wake wa ndoa kukaathiri uhakiki? Yaani nimeoa mke wangu mimi kwa hiyari yangu,akanizalia na watoto nipangiwe kuishi naye?Mimi na familia yangu tumeokisea nini serikali ya sasa ikiwa hata kubadilisha tu nafasi ni shida?
Ok, sisi sote ni walimu, mama Shule ya msingi na mimi baba Sekondari. Ninafahamu kua mimi kuhama kuifuata familia yanfu ni ngumu, basi kuna ugumu gani wa kumruhusu mke wangu kunifuata mimi baba wa familia?
Hivi kwa mazingira haya na vimishahara vyetu hivi nitasafirije Mara kwa mara nitoke Tanga kila mara kwenda Ngara Bukoba kusalimia familia yangu? Inaniuma sana kila ninachojaribu naambiwa uhamisho umezuiwa mpaka hapo tamko litakapotilewa.
Inafikia mahali watoto wangu wananiita Mjomba tu kwa sababu ya kutoonana nao mara kwa Mara, kisaikolojia watoto hawa kuna kitu muhimu sana wanakosa kutokaa na Baba yao karibu.Kila nikikaa nfikiria sana nakuta sababu tu ni kazi.
Kwakweli binafsi nimeamua bila kushawishiwa na mtu ikifikia mwezi June bado halii hii inaendelea, Ni bora mwanamke aache kazi anifuate nilipo tutengenze familia bora. Sitaki kuishi kama mtumwa kwa kupangiwa aina ya familia yangu itakayoathiriwa na kutopata malezi ya uhakika ya upande zote mbili.Tutagawana hiki kidogo ninachopata kisha maisha yataendelea tu.
Kule mkoani DSM tunasikia viongozi wengi wa serikali wamehamishia wake zao Ostabey wanaendelea na kazi zao za utumishi kama kawaida, lakini Wanyonge tunabaki kuugulia maumivu pale mwanao wa kumzaa anapokuita "ANKO"