Serikali: Marufuku wamiliki wa shule binafsi kutoza wazazi fedha za vifaa kinga

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
7A6803CB-928B-42C9-A6AC-B330D1B47E1B.jpeg


Serikali imepiga marufuku maelekezo yaliyoanza kutolewa na baadhi ya wamiliki wa shule za binafsi ya kuwataka wazazi wenye wanafunzi wa kidato cha sita kuhakikisha wanalipa shilingi laki 7 kabla ya kuripoti shuleni kama gharama za kununulia barakoa, sabuni, ndoo na vitakasa mikono kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi kujikinga na corona.

Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya rais TAMISEMI Mh. Mwita Waitara ametangaza marufuku hiyo jijini Mwanza baada ya kukagua ukarabati wa majengo ya shule kongwe ya sekondari Pamba na kuona maandalizi ya mapokezi ya wanafunzi 227 wa kidato cha sita katika shule hiyo.

Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo Fatuma Mashaka pamoja na Afisa Mtendaji wa kata ya Pamba Jonas Mugisha wamepongeza uamuzi wa Rais Dk. John Magufuli wa kufungua shule na vyuo, huku mafundi wanaoendelea na ukarabati wa majengo hayo wakiezelezea hatua waliyofikia.
 
Hapo wamiliki wa shule binafsi watakuwa wamenuna baada ya kusikia kauli iyo
 
Laki saba? mchanganuo wake ukoje yaani barakoa laki mbili khalafu sabuni laki na nusu kisha aah sijui nawaza nini huyu corona huyu
 
Serikali imefanya vizuri kuingilia kati, watu walikuwa wanataka kugeuza janga la covid-19 fursa wapige pesa kwa kuleta michango ya ajabu ajabu.Hongera Prof.Ndalichako kwa kuliona hilo.
 
Hapo shule binafsi walikuwa wanataka kuwafanya watoto wetu wawalipie mishahara walimu🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom