gimmy's
JF-Expert Member
- Sep 22, 2011
- 3,283
- 3,274
Salaam,
Tafiti zinaonesha kwamba wagonjwa wengi wa Saratani wamekuwa wakitokea Kanda ya Ziwa jambo ambalo linapelekea Serikali kuhangaika kutafuta sababu kwanini Kanda ya Ziwa?
Jana nimeona Mh Makamu wa Rais akiwa hospitali ya Bugando ameeleza moja ya sababu inayopelekea takwimu za saratani kuwa juu Kanda ya Ziwa ni watu wanaotumia maji ya kuoshea maiti kuhifadhia samaki.
Nimeona niijulishe Serikali kwamba moja ya wateja wakubwa wa maji haya ni waganga wa kienyeji na maji haya yanauzwa kwenye maduka ya dawa asili.
Ili Serikali ifanikiwe kudhibiti usambaaji wa biashara hii nashauri wahakikishe masoko yote pamoja na mochwari ambapo ndipo yanapotoka wanadhibiti vinginevyo tatizo hili litaendelea.
Asante.
---
Baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK. Phillip Mpango amesema ongezeko kubwa la ugonjwa wa saratani katika mikoa ya kanda ya ziwa unatokana na baadhi ya watu kutumia maji ya yanayotumika kuoshea maiti pamoja na dawa aina ya Cloroform inayotumika kuhifadhi samaki.
DK. Mpango alizungumza hayo wakati wa uzinduzi wa jengo la wagonjwa wa saratani katika huspitali ya rufani ya kanda Bugando jijini Mwanza, jengo ambalo limejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 5.6.
Baada ya kauli hiyo, inadaiwa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, Jana jioni ilianza kugawa fedha kwa waandishi wa habari kuzuia stori hiyo isitoke kwenye vyombo vya habari.
Taarifa kutoka ndani ya ofisi ya mkuu wa mkoa zinadai, fedha hizo zilikuwa zikitolewa na Katibu wa mkuu wa mkoa, bwana Matia Levi.
Inaelezwa zaidi ya waandishi 20 walipokea mshiko huo ili habari hiyo isiandikwe, lakini waandishi walipokea na kutoa habari hiyo.
Hata hivyo Leo mchana, Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza kitazungumza na vyombo vya habari kuhusu taarifa hiyo na inaelezwa wamesikitishwa na kauli ya Makamu wa Rais.

Kauli Makamu wa Rais kuhusu maji ya kuoshea maiti Kusababisha kansa
Picha: Sehemu ya gazeti iliyoandika habari hii