Serikali/Magufuli Ili Wazungu wasiwasumbue Suala La Ushoga Itisha Kura ya Maoni

MkamaP

JF-Expert Member
Jan 27, 2007
8,142
3,217
Ili Serikali ya Tanzania iachwe kusumbuliwa na wazungu na viongozi wake kuandamwa, itisheni kura ya maoni kwa wananchi kwa swali moja tu.
1: Je unakubali ushoga?
a. Ndiyo
b. Hapana.

Mnajua wazi halitapita wananchi watalikataa, hivyo wazungu wakiwa wanawafuata mnasema mnaheshimu demokrasia, na tena waiteni wazungu wawemo ktk kuhesabu hizo kura. Bila kuwanyamazisha hawa wazungu kwa kura ya wazi watawasumbua sana kila siku watakuwa na pretext zao ili kukusumbueni tu.

Hili dubwasha hapa chini viongozi wetu labda wawili ama watatu walishapiga saini, litawasumbua sana bila kulipeleka kwa kura za maoni kwa wananchi.
 
Sahivi nchi inaingia gharama kuliko kuitisha hiyo kitu. Hiyo kitu inatumika kuharamisha mambo mengi sana.

Midomo isafishwe kwa kura ya maoni, tena ya uwazi nawao wakiwamo ktk usimamizi. Bila hivyo watawasumbua sana mpaka mtaukubali ushoga maana washapata entry point.
 
Wao hawalizimishi nchi kukubali ushoga ila wanataka haki za hao mashoga kufanya mambo yao ya ushoga zitambuliwe, wanasema iko stipulated kwenye UN charter for human rights ambazo Tanzania ni signatory, hapo ndo kasheshe ilipo..
 
Mkuu nakerwa na uminywaji wa demokrsia, lakini hata tufe njaa na umaskini wa kutupwa Hatuna haja ya kupiga kura...hatuwezi kukubali Ushoga....yaani hili hata mimi nasema wote mashoga wakafie mbele lakini...kama suala ni uminyaji wa demokrasia waendelee kuibana serikali hadi ijirudi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magufuli usiumize Watanzania milioni 55 ili kulinda maslahi ya mtanzania mmoja, unatuangusha.

Unafikiri ushoga ni sababu ya mtu huyo mmoja? ni sera ya wazungu huyo makonda amewapa entry point tu yakuwezesha sera yao. Sahivi hata mmetoe makonda ama mmuache washapata pa kuingilia. Njia rahisi ni kura ya maoni na wao wakiwemo watulizwe bila hivyo yanaweza wawekea hadi sanctions.

Maana hapo hapo kinachofuata nikuwaambia tuhakikishie haki zao zitalindwa ktk katiba. Ili kuwashinda kirahisi twende na kura ya maoni ya wazi.
 
Back
Top Bottom