Serikali, madaktari rudini kwenye meza ya mazungumzo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali, madaktari rudini kwenye meza ya mazungumzo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Jun 30, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  KATIKA mgogoro unaoendelea hivi sasa kati ya Serikali na madaktari, yapo mambo matano ambayo sisi hatutaki kuyaamini. Kwanza, hatutaki kuamini kwamba unyama aliofanyiwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka juzi ulifanywa na Serikali au washirika wake kwa lengo la kumnyamazisha na kusitisha harakati za madaktari nchini kudai haki zao pamoja na kuboreshwa kwa mazingira ya kazi katika hospitali zetu hapa nchini.


  Pili, hatutaki kuamini kwamba mgogoro huo unaweza kumalizwa kwa vitendo vya ubabe na vitisho, ikiwa pamoja na kudhani kwamba suluhisho la mgogoro huo ni kwenda mahakamani. Jambo la tatu ambalo hatutaki kuliamini ni kwamba mgogoro huo utatoa mshindi iwe isiwe, kwa maana ya kumpata mshindi katika mazingira hayo ya uhasama na chuki pasipo kuwapo maridhiano kati ya pande zote mbili kupitia meza ya mazungumzo.

  Nne, hatutaki kuamini kwamba Serikali inaweza kuwa mchezaji na wakati huo ikawa mwamuzi wa mgogoro huo kutokana na ukweli kwamba nayo, kama walivyo madaktari ni sehemu ya tatizo. Kutokana na mgogoro huo kuwapo kwa muda mrefu, pande hizo mbili tayari zimejikuta katika mazingira ya uhasama, chuki, utengano na kutoaminiana kiasi cha kutoweza kufanya mawasiliano ya moja kwa moja pasipo kuwapo kiungo kati yao cha kuwaleta pamoja.

  Tano, hatutaki kuamini kwamba Serikali imekata tamaa kiasi cha kushawishika kutumia mabavu ya dola kuwafukuza kazi madaktari wote au viongozi wao wanaoratibu mgomo wao nchi nzima. Hii ni kwa sababu hatua hiyo itazaa balaa nchi nzima kwa sababu hatuoni mbadala wa madaktari hao wote waliogoma na kwamba kuwachukua madaktari wastaafu au wale walio katika majeshi yetu itakuwa ni kukuza tatizo, ikiwa ni pamoja na kuwafanya wauguzi na madaktari wanaofanya kazi kwa vitendo (interns) katika hospitali zetu kukasirika na kuamua kujiunga na mgomo huo.

  Tangu mgogoro huo uanze mwishoni mwa mwaka jana, tumekuwa tukiishauri Serikali bila mafanikio kwamba itulie na ijiepushe kufanya maamuzi ya ovyo, bali ifungue milango yote ya mawasiliano kati yake na upande wa pili. Kadri mgogoro huo ulivyokua na kuchukua sura ya migomo na uhasama wa kutisha tulishauri kuwa, watafutwe wasuluhishi waadilifu wanaokubalika pande zote mbili ambao busara, weledi na uwezo wao utazijengea pande hizo mazingira ya kuaminiana ili kila upande uweze kuzungumza na mwingine.

  Hivi ndivyo inavyofanyika sasa duniani kote. Katika kufuata kanuni na taratibu za usuluhishi, Serikali zimeacha utamaduni wa kujihusisha na usuluhishi wa migogoro ambayo serikali hizo zinahusika kwa namna moja ama nyingine kama njia ya kupata suluhisho la kudumu la migogoro. Kama tulivyosema hapo juu, haiwezekani Serikali ambayo inatuhumiwa na madaktari ikubalike kama msuluhishi wa mgogoro ambao pia unaihusu. Ndiyo maana tunasema kukua na kushindwa kutatuliwa kwa mgogoro huo kumesababishwa na Serikali yenyewe ambayo imekuwa kama mchezaji na mwamuzi wa mchezo kwa wakati mmoja.

  Serikali sasa itakuwa imetambua kwamba baadhi ya watu wamelihusisha na mgogoro wa madaktari, tukio la juzi ambapo Dk Ulimboka alifanyiwa unyama wa kutisha kwa kupigwa, kuteswa na kutupwa msituni. Bila shaka tukio hilo linafanya utatuzi wa mgogoro huo kuwa mgumu zaidi na ndiyo maana tunasema kuwa, kama Serikali inayo dhamira ya kweli ya kumaliza mgogoro huo, lazima ishirikiane na madaktari hao kupata watu waadilifu na wasiokuwa na maslahi binafsi katika mgogoro huo ili wawe wasuluhishi.

  Wakati suala hilo likifanyiwa kazi, ni matumaini yetu kwamba Serikali itahakikisha wahusika wote waliomfanyia unyama Dk Ulimboka wanatiwa mbaroni na kushtakiwa. Ushauri wetu ni kwamba pengine Serikali ingeunda tume huru kuchunguza suala hilo badala ya kuliachia Jeshi la Polisi ambalo pia ni moja ya watuhumiwa.
  Serikali, madaktari rudini kwenye meza ya mazungumzo

   
 2. 4

  4change JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2012
  Joined: Mar 4, 2012
  Messages: 535
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  hii serikali sijui wanasoma magazeti kama haya au wamebaki na magazeti yao ya 'udaku' ya habari leo,uhuru,mzalendo nk.
   
 3. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,168
  Likes Received: 1,173
  Trophy Points: 280
  Rais wa tanzania alijhuzuru pale igunga watu wakazimia, tunaye pm tu! (Joking)
   
 4. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2012
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Hakuna uongozi na kiongozi wa nchi. Halo ni mbaya, kama alivyopendekeza MMK ni bora tuagize viongozi toka ughaibuni watoe maamuzi magumu.
  Ni upumbavu kufikiri eti ukiboresha huduma za afya, nchi itayumba.
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Jun 30, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  This is silly; hii meza ya mazungumzo tangu 2006 hadi leo hii kwanini haimaliziki? Imekuwa kama kero za muungano? Miaka nenda rudi watu wanafanya vikao, wanalipwa posho, wanakuja na ahadi zaidi na vikao zaidi. KUna wakati mazungumzo inabidi yavunjike ili kulazimisha suluhisho la kudumu.
   
 6. chitalula

  chitalula JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,307
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  kama pm amekiri kushindwa na kikwete naye ameshindwa kuutatua basi tumkabidhi nchi dr slaa tu, maana waliolazimisha kutawala wameshakiri kushindwa wawaachie watawala wanaopendwa
   
Loading...