Serikali/Mabenki yawe na mkopo special kwaajili ya mwezi wa kwanza.

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,887
Imekuwa ni wimbi wa kila mwaka ifikapo January watu kupiga kelele ukata. Ni wazi kuwa mwezi january uchumi huwa unadorora. Si vizuri kulialia kila mwaka.

Serikali/mabenki wangekuja na mkakati wa kutoa mkopo special kwa mwezi january. Kama mtu mshahara wake takehome ni laki sita basi akapeshwe sita nyingine, ailipe kwa miezi kumi na moja. Kama mfanyabiashara anarejesha kila mwezi basi walau akopeshwe kama rejesho lake, iwe kama hajarejesha mwezi huo.

Kudorora kwa uchumi mwezi january ni tatizo na si kitu cha kukichekea au kikifanyia utani. Kinahitaji suluhisho. Unafikiri nini kifanyike kuboost uchumi mwezi january?
 
Kudorora kwa uchumi Januari?Kwani mapato yanapungua kwa sababu gani au matumizi yanazidi kwa sababu gani?
Do not chew what you cannot swallow.Matumizi yako yaendane na kipato chako.Fanya budget weka akiba hata kidogo.Wacha matumizi yasiyokuwa na lazima.
 
January matumizi yanakuwa mengi hata ubane bajeti. Ada, leseni za biashara, kuhuisha vibali, TRA, nk, nk.
N mbaya zaidi unakuwa umetoka disemba, mwezi wa sherehe. Wa matumizi mengi. Nguo za sikukuu, kusafiri kuona jamaa, tafrija nk.
 
Kupanga ni kuchagua Mambo yote hayo uliyonitajia hayaji ghafla .Watu wanajua wazi kwamba kuna ada, leseni na kadhalika. Weka akiba hasa kama ni mfanyabiashara tokea Februari mpaka Desemba ili kufidia Januari kama ni lazima ufanye sherehe kubwa na kuingia kwenye gharama ambazo huna uwezo nazo.
 
Ingekuwa kwa mtu mmoja au wawili watatu ningesema kupanga ni kuchagua. Lakini inakuwa nchi nzima. Hii ni shida ya nchi. We unaongea kinadharia zaidi, kwamba mtu aweke akiba, kwa mapato gani? Watu wasile pilau kuku krismasi na mwaka mpya, wasifanye ubatizo , vipaimara na komunio?

Unachosema kinamake sense ila ni nadharia tupu.
 
Ukichagua kutembea miguu peku usilalamike kuchomwa na jua au mbigiri.
Kwani ni choice yako.Matumizi yakizidi mapato lazima uchumi wako utayumba.
 
January matumizi yanakuwa mengi hata ubane bajeti. Ada, leseni za biashara, kuhuisha vibali, TRA, nk, nk.
N mbaya zaidi unakuwa umetoka disemba, mwezi wa sherehe. Wa matumizi mengi. Nguo za sikukuu, kusafiri kuona jamaa, tafrija nk.
Hivi vitu vyote ulivyo vitaja hapa vinahitaji tu maandalizi na bajeti. Ukifanya kwa kukurupuka, ndipo shida inapoanza.
 
Ingekuwa mtu mmoja sawa, lakini ni kila kona ya nchi na kila mwaka. Hata wale 'wasiokurupuka' hujikuta wanaathirika na mdororo wa uchumi wa january.
 
Ukichagua kutembea miguu peku usilalamike kuchomwa na jua au mbigiri.
Kwani ni choice yako.Matumizi yakizidi mapato lazima uchumi wako utayumba.
Hili si suala la mtu mmojammoja, mwezi january uchumi wa nchi nzima hudorora.
 
Wachaga bwana hela mnamaliza bar na kwenye mizimu halafu mnataka mikopo hii nchi mnaishi wenyewe?
 
Umesema sahihi, mtu akitaka kuelewa january inavyokuwaga ngumu aende benki. Akae tu aone jinsi watumishi na wafanyabiashara wanavyoenda kiililia benki iwakopeshe.
 
Imekuwa ni wimbi wa kila mwaka ifikapo January watu kupiga kelele ukata. Ni wazi kuwa mwezi january uchumi huwa unadorora. Si vizuri kulialia kila mwaka.

Serikali/mabenki wangekuja na mkakati wa kutoa mkopo special kwa mwezi january. Kama mtu mshahara wake takehome ni laki sita basi akapeshwe sita nyingine, ailipe kwa miezi kumi na moja. Kama mfanyabiashara anarejesha kila mwezi basi walau akopeshwe kama rejesho lake, iwe kama hajarejesha mwezi huo.

Kudorora kwa uchumi mwezi january ni tatizo na si kitu cha kukichekea au kikifanyia utani. Kinahitaji suluhisho. Unafikiri nini kifanyike kuboost uchumi mwezi january?
January 1.Ada 2 .TRA 3.Kulipa madeni yaliyokopwa December 4 .kuwarudisha makwao ndugu waliokuja Kula sikukuu ....ni balaa tupu
 
Imekuwa ni wimbi wa kila mwaka ifikapo January watu kupiga kelele ukata. Ni wazi kuwa mwezi january uchumi huwa unadorora. Si vizuri kulialia kila mwaka.

Serikali/mabenki wangekuja na mkakati wa kutoa mkopo special kwa mwezi january. Kama mtu mshahara wake takehome ni laki sita basi akapeshwe sita nyingine, ailipe kwa miezi kumi na moja. Kama mfanyabiashara anarejesha kila mwezi basi walau akopeshwe kama rejesho lake, iwe kama hajarejesha mwezi huo.

Kudorora kwa uchumi mwezi january ni tatizo na si kitu cha kukichekea au kikifanyia utani. Kinahitaji suluhisho. Unafikiri nini kifanyike kuboost uchumi mwezi january?
Na wa saba😂😂
 
Daaah, inasikitisha
 
Back
Top Bottom