Serikali :Lowassa na wenzake waliojiuzulu walilipwa mafao-Udhaifu wa sheria ya Mafao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali :Lowassa na wenzake waliojiuzulu walilipwa mafao-Udhaifu wa sheria ya Mafao

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Shadow, Feb 3, 2009.

 1. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Kulingana na baadhi ya hizi sheria za mafao ya viongozi zimekaa kimtego zaidi . Inabidi zifanyiwe marekebisho hili kulinda maslahi ya Taifa. Mfano mtu aliyeshindwa uongozi kwa uzembe au ufisadi anaweza kuishia kujiuzulu na kuendelea kufaidi pesa ya walipa kodi.This will be hard but 'yes we can get there' if there is a political will accompanied by a public pressure through our representatives and civic sociaties


  Serikali :Lowassa na wenzake waliojiuzulu walilipwa mafao
  Na Mwandishi Wetu

  SERIKALI imesema viongozi wa kisiasa waliojiuzulu kutokana na sababu mbalimbali, walilipwa mafao yao kwa kuzingatia sheria za kazi pamoja na katiba ya nchi.


  Viongozi waliojiuzulu ni pamoja na aliyekuwa waziri mkuu wa awamu ya nne, Edward Lowassa.


  Akijibu swali la Mbunge wa Karatu, Dk. Wilibrod Slaa (Chadema), Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Jeremiah Sumari, alisema kumekuwepo na utata wa kutafsiri juu mtu kufukuzwa kazi na kujiuzulu.


  Alisema kuwa suala hilo halijafafanuliwa katika sheria za mafao ya viongozi wa kisiasa namba tatu ya mwaka 1999 kifungu cha tano na sheria ya pensheni ya mafao kwa watumishi wa

  umma namba mbili ya mwaka 1999, kifungu cha 16.


  Pamoja na utata huo, Sumari alisema: “Viongozi wa kisiasa wanaojiuzulu wanastahili kulipwa mafao kama ilivyoainishwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”


  Kwa sababu hiyo, alisema viongozi wote wa kisiasa waliojiuzulu walilipwa mafao yao kwa kuzingatia sheria namba tatu ya mwaka 1999 kifungu cha tano.


  Sumari aliwataja waliofaidika na sheria hiyo kuwa ni rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, makamu wa rais wa serikali ya awamu ya tatu, Hayati Dk. Omar Juma.


  Wengine ni waliowahi kuwa mawaziri wakuu, Lowassa (awamu ya nne) na Frederick Sumaye (awamu ya tatu).


  Wengine ni spika wa bunge la serikali ya awamu ya tatu, Pius Msekwa, mawaziri na manaibu wa serikali ya awamu ya nne na tatu, wakuu wa mikoa na wilaya (awamu ya tatu) na

  wabunge wote walioishia katika kipindi cha mwaka 2000 na 2005.


  Katika kuuliza swali lake, Dk. Slaa alisema kuwa kifungu cha nne cha sheria ya mafao ya viongozi wa kisiasa, kinatoa tafsiri ya viongozi wastaafu kwa maneno ya aliyeshika nafasi na aliyeacha kushika nafasi hiyo.


  Katika kujenga hoja yake, Dk. Slaa alisema kuwa tafsiri inaacha utata jinsi mhusika anavyoacha uongozi yaani kwa kustaafu, kustaafishwa, kufukuzwa au kujiuzulu mwenyewe na hasa ikizingatiwa kuwa kwa mujibu wa sheria maneno hayo yanatofautiana kuhusiana na malipo ya mafao.


  Dk. Slaa alitaka kufahamu tafsiri inayostahili malipo ya mafao, taratibu za mafao zinazotumika kwa viongozi hao na pia idadi ya viongozi ambao wamefaidika kwa majina na vyeo pamoja na kiasi walicholipwa.


  Hata hivyo, Sumari alikataa kutaja kiwango cha fedha walizolipwa viongozi hao wa kisiasa kwa maelezo kuwa “walilipwa kulingana na stahili zao.”

  Mwananchi Read News
   
 2. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Napata mashaka kwamba sheria nyingi zinaundwa kimtego mtego ili kuwalinda vigogo. Mfano huu hauna tofauti na ile sheria ya takrima. Nadhani umma unayo nguvu na ni wakati muafaka kukataa huu upuuzi. Hii ni aina nyingine ya ufisadi. Kwani mtu akingundua kwamba karibia anafukuzwa kazi anawahi kujiuzulu ili aendelee kukomba pensheni. Sina hakika ila nasikia kwa mtumishi wa kawaida hakuna pensheni hadi ufikishe miaka 55 toka utumishi wako ulipokoma. Ila kwa wanasiasa wanajiuzulu leo na kuanza kukomba pensheni papo hapo!! Kweli hii ni bongo Dar!
   
 3. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Swali linapaswa kua kama bado wanaendelea kulipwa mpaka leo, na sio kama walilipwa huko nyuma.
   
 4. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sheria ni bora ikabadilishwa ili kuimarisha maadili kwa watumishi wa umma na wam kisiasa.
   
 5. Mchola

  Mchola Member

  #5
  Feb 3, 2009
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 88
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamaa wanaotunga hizo sheria wanajua kabisa kwamba hata wao zinawahusu ikitokezea kwamba wameachishwa kwa hiyo they are not objective when drafting them, they leave loopholes!!. Kwa upande mwingine wabunge wanaopitisha sheria huwa hawazisomi critically. Laiti kama kila mtu angetimiza wajibu wake(i.e. watunga sheria na wapitishao bungeni) basi haya yasingejitokeza. sheria zingekuwa water tight!!
   
 6. A

  August JF-Expert Member

  #6
  Feb 3, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Hizi sheria waliziweka kimtego mtego kwa makusudi wakijua wanacho taka kufanya, sasa bahati mbaya wabunge wetu wengi au kwa ujinga au kutokujua wanapitisha wakichukulia kwamba ni sera ya chama na ni uamuzi wa Raisi hiyo sheria ndi iwe hivyo, na vitu vingi tu wabunge wetu wanakuwa bendera fuata upepo
   
 7. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #7
  Feb 3, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Acha tu kusoma critically, sina hakika ni asilimia ngapi ya wabunge wanapitisha macho kwenye miswada (to just go through the documents or scan them). Kama kuna utafiti ulikwishafanyika kuhusu jambo hili ungetusaidia kupata data zaidi. Lakini kwa mwenendo huu ambapo baadhi ya wabunge ni wafanyabiashara au wanahusika na uendeshaji wa kila siku wa makampuni binafsi, itakuwa ndoto kwao kupata muda wa kusoma. Kwa uzoefu wangu, kama kuna kitu kigumu sana kwa watu wengi, ni kusoma mambo kama repoti na nyalaka nyinginezo ambazo zinamtaka mtu kutuliza akili na kutafakari.
   
 8. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #8
  Feb 3, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Kama hakuna 'real political will' basi hii ni kuonyesha serikali haiko serious katika kupambana na hao mafisadi. Huu ndIo muda wa MUAFAKA wa kuanza kuzifanyia mabadiliko hizi sheria zilizokaa kimtego mtego.

  Najua madiliko hayo hayawezi kuwakumba waliokwisha faidika na hizi sheria za mafao (restrospectively) lakini itakuwa ujumbe tosha kwa waliopo na walioko mbioni kujinufaisha kwa njia zisizo halali.

  Sheria nyingine ambayo imekosa 'politcal will' ambayo hipo hipo tu ni ile kuhusu kutaja mali za viongozi (Code of Ethics). Nayo hamna mtu anayeifuatilia. Leo hii Chenge angekuwa mahakani kwa kuisigina ( Naongelea mabilioni yake aliyoficha huko New Jersey-UK).

  LACK OF POLITICAL WILL AND IMPUNITY will kill the nation at the end of the day.

  Shadow.
   
Loading...