Serikali, lini kituo cha Daladala Kawe kitafanyiwa ukarabati?

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,191
4,104
Kawe ni sehemu yenye wakazi wengi na pia eneo hilo hutumiwa na watu wanaosafiri kutoka sehemu mbalimbali kwa katika kusaka riziki zao.

Cha kusikitisha, Kawe haina kituo cha daladala cha kueleweka. Kwa sasa magari husimama pembezoni mwa uwanja wa Tanganyika Packers, sijui kama ndio eneo sahihi ambalo Serikali ilikusudia liwe kituo cha daladala au gari husimama hapo kwa kukosa kituo cha kusimama. Nasema hivi kutokana na changamoto ya udogo wa eneo hilo.

Pamoja na udogo wa eneo hilo, awali magari yalijibana na angalau yakaweza kutosha japo kwa kubanana sana. Kwa sasa baada ya kubomoa vibanda vya wamachinga na kujengwa uzio ambao umepunguza zaidi eneo ambalo magari yalikuwa yakisimama kupakia abiria, kwa kweli imekuwa kero kubwa sana kwani magari yamebanana na kusababisha usumbufu kwa abiria.

Sambamba na hilo, eneo hilo linalotumika kwa sasa limejaa mashimo, hakuna huduma muhimu ya choo chenye ubora kwa ajili ya abiria watakaofika hapo kupata huduma ya usafiri.

Choo kilichopo ni "mobile toilet" ambacho kimsingi yataka moyo kuingia humo, na kwa mazingira kilipo kinasababisha kero ya harufu mbaya kwa abiria kwani kimewekwa sehemu ambapo abiria husimama ili kupanda magari.

Wito wangu kwa Serikali na wote wanaohusika waone umuhimu wa kushughulikia kero hii ili huduma hii muhimu iweze kuwa rafiki kwa watumiaji wa kituo cha Daladala cha Kawe.
 
Back
Top Bottom