macho_mdiliko
JF-Expert Member
- Mar 10, 2008
- 21,697
- 39,396
Unajaribu kusema au kuomba nini ndugu! Kuwa kama ''wana moyo wa kwenda'' basi wapunguziwe gharama ili waende? Kwani umeshambiwa kuwa kuna upungufu wa watu wenye moyo wa kusafiri na timu? Kama unataka kwenda basi tafuta hizo fedha! Katika maisha ya kila siku moyo huwa unapenda kufanya mengi lakini uwezo ndiyo unatuzuia.Habari za asubuhi watu wa JF,
Leo nimesikia Serikali imetoa ndege kwa lengo la kuipeleka Taifa Stars ktk visiwa vya Cape Verde, kwa jambo hilo kwanza naipongeza Serikali yetu saaaaana.
Lakini napenda kutoa wazo katika hilo juu ya bei ya abiria ambao watapenda kwenda na timu huko Cape Verde ili kuishangilia timu yetu hii pendwa ya taifa.
Serikali imetangaza shabiki yeyote atakayetaka kwenda na timu atalipia kiasi cha 1,500 USD Ambayo ni zaidi ya Shilingi 3,000,000,/= (milioni tatu). Kwa kiasi hiki kuna watu watashindwa kulipia japo wana moyo. Mimi naomba liangaliwe upya hili swala la washingiliaji ama bei ipungue au isiwepo kabisa ili kuhakikisha idadi kubwa ya mashabiki kuhudhuria.
Asanteni.