nizakale
JF-Expert Member
- Oct 23, 2019
- 4,029
- 2,895
Umeandika huu uzi ukidhani utawashawishi wanamwanza waichukie CCM. Umejidanganya sana. Tafuta kazi ya kufanya.Mmekuwa mkituimbia ka wimbo ka tunataka kuifanya Mwanza kuwa kitovu cha biashara cha maziwa makuu kwa kuimarisha miundombinu na miundomsingi.
Hatukatai kuwa juhudi zenu baadhi zinaonekana kama ujenzi wa meli, daraja, masoko, stendi za magari,reli, uwanja wa ndege n.k kwa hapa niwapongeze kwa nia yenu ya dhati kabisaa mliyonayo kwa jiji letu pendwa la sato.
Kinachonikera mimi si kingine bali naona kama nyie SERIKALI ndiyo kikwazo cha ukuaji chanya wa mji wetu wa Mwanza, mnauzorotesha na wala hamuupi kipaumbele unachostahili kama jiji la pili hapa Tanzania nayakwamba ni taswira ya pili ya nchi yetu ikitoka hiyo Dar mnayoangaika kuiboresha kila uchao.
Leo hii jiji kubwa kama Mwanza halina taa hata moja ya barabarani kuanzia usagara mpaka unafika mjini na tokea mjini mpaka kisesa ni giza tupu, mabatini ilivyokuwa ikijulikana kwa kuchangamka nyakati za usiku pale gengeni leo hii kweli nipakukutana na ulinzi shirikishi highway saa 3 wamebebelea mapanga kisa wanaimarisha ulinzi eti mitaa ina giza hivyo vibaka na wezi ni tishio.
Bila aibu mmewaachia kazi yenu wanamwanza waishio milimani ndo wawashe taa za majumbani mwao ndo waupe mji mwangaza kisa magari yenu yanataa hivyo haina haja ya kuweka taa za kumulika barabara, eti Mwanza na fahari yake yote inabakia kuwa jiji la taa moja tena ya kuongozea magari pale buzuruga junction, Are we serious?
Jiji la Mwanza linakabiliwa na uhaba mkubwa mno wa mtandao wa barabara za LAMI kuanzia zile kuu mpaka za mitaani ni vumbi tupu, tunawazeeshea watu magari yao utadhani wanafanya biashara kijijini, Vituo vya daladala ndo sasa usiseme ni full vumbi na makorongo.
Hivi inawapendeza sana waheshimiwa mkipita na magari yenu ya kifahari na ving'ora kwenye highway ya lanes mbili na tatu ambazo hamna hata mpango wa kuzitanua at least ziwe 6,8 au 12 kuondoa misongamano na overtakes zisizo na ulazima katika majiji yetu au mnawaona watanzania kama vile wapo usingizini na wala miji yao haiwaumi ikipitwa kwenye suala la miundombinu na vimiji vidogo vidogo kwenye nchi za jirani.
Hivi kwanini suala la ring roads, barabara pana, fly overs,taa za barabarani, n.k kwa miji yetu yote hata kama mkiamua kuanza na ile mikubwa hamuipi kipaumbele na wala hamuonekani kujishtukia kuwa kama nchi mnadumaza ukuaji mzuri wa miji na majiji pia mnatuchelewesha kimaendeleo, mnatufanya tuonekane hatuna maana mbele ya vinchi vichanga tudharaulike na kuonekana watanzania ni washamba na miji yao miundombinu yake haiendani na karne ya 21.
Ifikie wakati kama nchi masula ya miundombinu bora katika majiji yetu uwe ni ushindani wa kawaida na majiji yaliyoendelea zaidi duniani natuchukulie ni jambo la kawaida na siyo ufahari au kuhisi watanzania sote hatuna exposure,
hivyo inapotokea mkijenga kitu kidogo kama kidaraja cha juu cha waendao kwa miguu matangazo yanakuwa mengi na bado mnategemea tuwasifiwe kana kwamba hatukupaswa kuwa navyo ila kwa hisani mmeamua kutuzawadia vitu ambavyo si level zetu sijuhi huwa mnatuonaje.
Mlikuwa na mpango mzuri kabisa wa kuondoa vipanya(hiace) katika mzunguko wa jiji nabadala yake zitumike basi kubwa au coaster kama daladala na wananchi wa Mwanza walivyo wapenda maendeleo mwitikio ulikuwa mkubwa,
watu wakaanza kuingiza barabarani magari yao cha ajabu ruti zote mpaka leo zimebakia kusomeka nyashishi au airport no otherwise kwingineko miundombinu majanga nani ajitose kupeleka gari kwenye vumbi,milima na majabari akagongeshe gari kwenye mashimo na kudondosha vioo vya gari lake au kukata shock ups zake.
Hivi hata kutenga maeneo kadhaa ya wazi nakupanda miti,nyasi, kuweka mabenchi, swimming, sanamu, sinema au mabembea kuufanya mji uwe na bustani kadhaa za kupumzikia kuanzia CBD hadi mitaani
kupendezesha jiji pia ni mpaka mkumbushwe nyie mnaojihita mamlaka ya jiji.
Kuna ufahari gani kutembea ukiona maghorofa lakini huna pa kupumzikia matokeo yake tunajazana tukikaa kwenye msingi mbele ya geti la pamba sekondari utafikiri omba omba kumbe hatuna namna.
Leo hii unashuhudia kati kati ya jiji la Mwanza (CBD) mtu bado anapewa kibali na anafanya ujenzi wa nyumba ya chini(isiyo ya ghorofa) kwa ajili ya kuishi yeye na wapangaji wake tena around main roads sehemu ambazo ni promising sana na anaruhusiwa kuendelea na ujenzi wake bila bughudha vitu vinavyopelekea mwonekano mbovu wa sura ya jiji, hapo pembeni utashuhudia jumba la ghorofa 8 pembeni(chini yake) vibanda kama sita vyenye bati za kutu zimezingira.
Kuna maeneo kadhaa bado miundombinu ya maji ni shida na miundombinu mingi ya maji inajengwa kwa mwendo wa kuchechemea mno.
Itoshe kusema kuwa changamoto ni nyingi katika jiji hili ila chanzo kikuu ni SERIKALI naomba BADILIKENI.