Serikali kwanini inawapa mikataba wastaafu kwenye nafasi za Menejimenti?

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
19,586
14,137
Twende moja kwa moja kwenye nada..

Kuna tabia imezuka kwenye utumishi wa Umma ya kuwapa watu ajira za mikataba licha ya kwamba wamestaafu.Tabia hii imekita mizizi kwa TANROADS na TARURA.

Tabia hii ilianzishwa na Serikali ya awamu ya 5 kwa kuwaongezea mameneja wa Mikoa, mtendaji mkuu na wakurugenzi wengine Wizarani na Makao Makuu ya Tanroads mikataba licha ya kwamba wamestaafu utumishi wa Umma..

Hivi unaanzaje kuwapa watu mikataba kwenye ngazi za administration? Si afadhari wawape mikataba watu kwenye Nafsi za utendaji ambazo zina upungufu mkubwa na ni za muhimu zaidi kwa sababu ni operational in nature?

Pili kuna tatizo kubwa la ajira Nchini lakini cha ajabu mnaendelea kuwapa mikataba watu waliostaafu badala ya ku recruit staff wapya. Hivo hata ile inaitwa Succession plan kwenye taasisi itafanikiwaje ikiwa mnawa ng'amg'ania wazee mpaka wanafia maofisini?

Kazi zenyewe hawawezi,wanalala mda mwingi,wanawahi kuondoka ofisini sababu za uchovu na wanafanya Kazi kwa mazoea badala ya kuendana na Kasi na ubunifu?

Wizara ya Utumishi ikomeshe hii tabia, unawapaje Kazi za mikataba watu waliostaafu na mbaya zaidi kwenye Nafasi za Management badala ya nafasi za kiutendaji.

Utashangaa maofisa wakubwa kwenye Idara mbalimbali za serikali ndio wanaongezewa mikataba lakini manesi au madaktari wa kawaida wakistaafu hawapewi hiyo mikataba. What is the rationale behind this?

Haya ni matusi kwa maelfu ya graduates walioko mtaani kwa kukosa ajira wakati kuna watu wanastaafu utumishi wa Umma na wanaendelea kuongezewa mikataba.

Kama kuna haja ya kuwapa mikataba watu waliostaafu basi iwe ni kweli kada za watendaji na palipo na upungufu au panapohitaji utaalamu wa kipekee lakini sio kama inavyofanyika sasa hivi.

Tunaomba Waziri wa Utumishi ukomeshe hii tabia na chunguza kwenye taasisi tajwa hapo juu,hai make sense kuongezea mikataba watu waliochoka na wasio hata na ufanisi kwenye utendaji.
 
Hakuna vijana wenye uwezo


USSR
Wewe ni mjinga tu ...hii nchi ina vijana kibao Wana uchu wa kulitumikia taifa ila wazee wasio na nguvu wamejazana oficn ni swala la muda tu wataachia wenyewe hayo ma oficn na hao unaowaita hawana uwezo ndio tegemeo la kesho
 
Wastaafu wangejua maisha baada ya kustaafu yalivyo mazuri wasingerudi huko ofisini kwa njia ya mikataba.

Waache kuogopa maisha
 
Wewe ni mjinga tu ...hii nchi ina vijana kibao Wana uchu wa kulitumikia taifa ila wazee wasio na nguvu wamejazana oficn ni swala la muda tu wataachia wenyewe hayo ma oficn na hao unaowaita hawana uwezo ndio tegemeo la kesho
Ni kweli ni wengi ni kweli wana uchu? But do they cut it?
Siwatetei but nafasi zingine uzoefu.
Kijana huwez kutoka fresh from university gafla ukawa head of management..
Haipo
 
Ni kweli ni wengi ni kweli wana uchu? But do they cut it?
Siwatetei but nafasi zingine uzoefu.
Kijana huwez kutoka fresh from university gafla ukawa head of management..
Haipo
Uzoefu gani gani wewe mtu? Hivi hiyo ofisi inakuwa haina watu wa chini ambao wamefanya Kazi kuweza kuchukua nafasi ya huyo anaestaafu? Kuna ofisi ina meneja au Mkurugenzi na wengine wote wa chini ni vijana tuu?

Kwa hiyo Mfugale kwa mfano wakati ni mtendaji wa Mkuu wa Tanrods hakukiwa na watu wenye uzoefu chini yake hadi afie madarakani? Mbona saizi yuko mwingine uzoefu kautoa wapi?

Meneja wa Tanroads mkoa unapompa mkataba hakuna wahandisi wa chini yake? Uzoefu gani unazungumzia?
 
Hakuna vijana wenye uwezo


USSR
Na wewe unaamini hakuna vijana wenye uwezo?

Na wewe ni kiazi aisee.Haya Mfugale alifia kwenye kiti,saizi yuko Rogatus umeona mambo hayaendi? Au umeona hakuna hana uwezo? Acha kutetea ujinga.
 
Uzoefu gani gani wewe mtu? Hivi hiyo ofisi inakuwa haina watu wa chini ambao wamefanya Kazi kuweza kuchukua nafasi ya huyo anaestaafu? Kuna ofisi ina meneja au Mkurugenzi na wengine wote wa chini ni vijana tu...
Wapo wasaidizi watu wa chini. Ndio maana nikasema pale juu.

Kuwa hatolewi mtu katoka chuo na kuajiriwa kuwa manager wa taasisi kubwa over night.

Sijasema wafanyakazi ambao wapo kazini tayari.

Nini kitawabeba hao wafanyakazi wa chini? Muda kazini na uchapa kazi. Muda kazin ndio uzoefu wenyewe huo.
 
Back
Top Bottom