Serikali kwa ufadhili wa Benki ya Dunia imezindua Programu ya BOOST ya miaka mitano yenye thamani ya Trilioni 1

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,802
11,961
Serikali kwa ufadhili wa Benki ya Dunia imezindua Programu ya miaka mitano yenye thamani zaidi ya shilingi Trioni moja,lengo kuu ikiwa ni kuhimarisha ufundishaji na ujifunzaji (BOOST)katika shule za awali na msingi.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika leo Juni 6,jijini Arusha, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Programu hiyo inalenga kuboresha mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji, ujuzi na ubora wa walimu katika ufundishaji na kuimarisha upatikanaji wa rasilimali za kuwezesha utoaji wa huduma katika ngazi ya Halmashauri.

Prof. Mkenda ameeleza kuwa katika maeneo hayo matatu, programu itajikita katika kuboresha miundombinu ya shule za Msingi kwa kuzingatia mahitaji hususani ujenzi wa madarasa, uimarishaji wa mpango wa shule salama, kuimarisha uwiano wa uandikishaji wa wanafunzi wa Elimu ya Awali, kuboresha vifaa na njia za ufundishaji katika madarasa ya Elimu ya Awali.

“Pia itaimarisha na kuendeleza mpango wa mafunzo ya walimu kazini, kuimarisha vituo vya walimu na shule za msingi katika utekelezaji wa mtaala wa TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji na kuendeleza utengaji wa bajeti kwa ajili ya kugharimia shughuli mbalimbali za utoaji wa Elimu na kuimarisha utawala bora katika elimu.” Ameongeza Prof. Mkenda

Waziri Mkenda ameongeza kuwa ili Serikali iweze tekeleza program hiyo kwa ufanisi,amewataka watendaji wote kutoka katika ngazi ya Wizara na Taasisi watakaohusika na utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Programu kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili kufikia vigezo na viwango vyote vilivyowekwa kwa kila mwaka.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa(TAMISEMI) David Silinde amesema ofisi yake imepanga kuwajengea uwezo watekelezaji wa programu hiyo.

Silinde amesema kuwa,TAMISEMI itaendelea kuchukua hatua za haraka na maboresho pale inapohitajika ili kuondoa changamoto zote ambazo zinaweza kukwamisha programu hiyo.

Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini, Mara Warwick amesema matarajio ya taasisi hiyo ni kuona elimu ya awali na msingi inakuwa bora,salama na jumuishi kwa watoto wote wanaotakiwa kuwa shuleni.
“Tunatarajia program hii ya Boost itanufaisha wanafunzi zaidi ya milioni 12 katika eneo la Tanzania Bara,uwekezaji katika eneo hili unaweza ukawa kichocheo kikubwa katika kukabiliana na umaskini”alieleza.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii Aloyce Kamamba ameipongeza serikali kwa kuzindua programu hiyo, ambapo ameshauri miundombinu inayokwenda kujengwa isimamiwe kwa umakini ili iwe bora na ikamilike kwa wakati huku akisisitiza kuangaliwa kwa walimu kwa kuwapatia mafunzo endelevu na kuajiri walimu wapya.
IMG-20220606-WA0009.jpg
IMG-20220606-WA0012.jpg
IMG-20220606-WA0010.jpg
IMG-20220606-WA0013.jpg
IMG-20220606-WA0011.jpg
 
Hizi hera za elimu sizimetoka karibuni miaka ya nyuma enzi ya magufuri ,, au kunazingine zinapigwa tu
 
..hizo fedha, trilion 1, ni mkopo au msaada?

..sasa linganisheni na ujenzi wa maofisi ya vigogo / mji mkuu Dodoma. Tumetumia trilion ngapi.

..pia linganisha na fedha tulizotumia kununua ndege na hasara ya kila mwaka ya Atcl. Ni trilion ngapi tumepoteza.
 
Pamoja na matrilioni yote, utaja sikia...'wanafunzi wadaiwa karo' nahisi

Nipo na shauku kubwa ya kuona utekelezaji wa watekelezaji.
CCM Oyee
 
Hizo pesa wataishia kulipana posho wakubwa na makongamano kwenye hoteli za kitalii badala ya kuwapa motisha walimu + kuwawekea mazingira mazuri ya kufundishia
 
Back
Top Bottom