Serikali kwa hili la tozo za miamala mmechemka na kukosa ubunifu

sambulugu

JF-Expert Member
Jun 1, 2021
3,932
7,269
Serkali inatakiwa kutambua kuwa watanzania wako tayari kuchamgia lakini tatizo ni viwango vya makato mfano:
  • Mtu akitoa 10,000 anatozwa makato ya serkali wastani wa shilingi 320 lakini serkali ingeweza kukata shilingi 100 kwenye makato ya kuanzia mtu anapotoa 1,000-10,000
  • Mtu akitoa 100,000 makato ya serkali ni sh 2050 lakini serkali inaweza kukata sh 1000 kwa watu wote wanaotoa kuanzia 100,000 mpaka 500,000 na itapata pesa nyingi sana maana mwananchi hatahisi mzigo kwa makato hayo.
  • Ukitoa milioni moja (1000,000) makatao ya serkali ni 9,400 lakini serkali inaweza kukakata shilingi 5,000 kwa kila mwamala unaozidi milioni moja na mwananchi hataona maumivu kwa hilo. Upande wa mtu kumrushia hela mtu mwingine sioni haja ya serkali kutoza tozo ili kururusu mzunguko wa pesa maana mtu akirusha pesa mwisho ataenda kuitoa kwa wakala au kulipia huduma​
Madhara yafuatayo yanatoea na yatayotokea
  • Kupungua kwa mzunguko wa pesa maana miamala itapungua sana baina ya mtu na mtu kwa mfano watu kutuma pesa kwa ndugu na watu wanaowategemea kama wazee na wazazi.
  • Kuongezeka wa uhaba wa ajira maana watu wote hususani vijana waliokuwa wakitoa huduma hii watafirisika kutokana wa upungufu wa wateja.
  • Serkali haitapa fedha ilizotarajia hata kwa asilimia 50% kwa kuwa imeshupaza shingo kwa kufanya uuaji wa biashara na mzunguko wa pesa
  • Watu wengi watalazimika kutembea na pesa nyingi hususani watu wanaoenda kufanya biashara kijijini na kuongeza mataukio ya ujambazi.
Ushauri kwa serkali.
  • Serkali ifanye marekebisho ili pawepo na manufaa kila upande serkali ipate na watu wapate kwa maana biashara ya uwakala iendelee kuwanufaisha watanzania.
  • Serkali ilinde ajira za vijana waliowekeza kwenye biashara hii ya uwakala kwa kurekebisha makato
  • Serkali iendelee kutoa elimu na kuhakikisha inawahimiza watanzania wote kutambua umuhimu wa kulipia kodi.
  • Serkali lazima ihakikishe inakuwa na kauli moja kwenye mambo ya kodi badala ya kuwa na kauli tofauti na za kejeli kwa watanzania mfano Mwigulu nchemba aliwaambia watanzania kuhamia Burundi na Makamu wa Rais pia kauli zake zinakuwa sio rafiki kwa wananchi.
  • Serkali ihakikishe kila mtumishi wa uma na mwanasiasa kama WABUNGE, WAKUU WA WILAYA/MIKOA wanatoa kodi na sivinginevyo.
 
Tumeambiwa kelele zetu amezisikia,kamati inakaa tena
"Kelele" hii ni dharau.
Viongozi wengi sio waathirika wa moja kwa moja na sheria hizi, maana wao sio watumiaji wa huduma ya kifedha za simu.

Watunga sheria na sera wa taifa wanatakiwa kubadilika,wasiwe wabunge,bali wabobezi wa eneo husika.
Kila leo tunatunga sheria nyingi zisizotekelezeka.

Sasa naamini tunahitaji KATIBA MPYA yenye meno.
 
Sasa Waziri mwenyewe mwigulu! Unategemea kuwepo na ubunifu? Yeye anadesa tu na kuokoteza mapendekezo ya watu kwenye mitandao, na pasipo kufanya utafiti wowote ule!! Kazi ipo.
 
Back
Top Bottom