Serikali kuwasilisha Muswada wa Katiba mpya bungeni la 10

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
Baada ya kupokonya hoja ya Mh. Mnyika kuhusu uundwaji wa katiba mpya serikali imetangaza leo bungeni kuwa itawasilisha muswada wa kuundwa kwa Tume itakayoratibu mchakato wa Katiba hiyo katika mkutano wa Tatu wa Bunge la 10, Aprili mwaka huu.

Source: HabariLeo
 
Safari hii tunataka bunge ndio liunde tume ya bunge ya kuratibu mchakato wa kuandika katiba mpya kwani hawa ndio wa Wakilishi wa wananchi.
 
Nimejikuta hata imani yangu kwa competence ya bunge letu la sasa na speaker wake kama wanaweza kubeba jambo hili kwa umakini. Kwa niliyofuatilia kwenye kikao cha jana na fikra za wabunge wengi na speaker wao bado nahisi hata wakipewa itaweza kuwa na matokeo tusiyotarajia

Bunge hili sio lile la Sitta ambalo kamati inaundwa na kupewa wigo wa kufanya kazi yake. Anyway, bado ina stand kuwa bunge kuunda kamati itakayoundwa kwa makundi mbalimbali ndani ya jamii na kuwajibika kwa bunge na sio raisi ni best option kwenye jambo hili
 
Nimeipata point yako ni kweli, lakini wabunge wanajua suala hili la katiba linagusa maslahi ya wananchi wengi na litawaamulia ama kurudi kwao bungeni au la, hivyo watalazimika kuwa makini nalo. Sasa huyu rais anayemaliza kipindi chake, du inanipa mashaka, kwani sana ataangalia maslahi yake hasa baada ya kung'atuka na akizidi kidogo labda kwa chama chake zaidi si kwa wananchi kwa ujumla wao.

Back
Top Bottom