Serikali kuwashtaki viongozi wa chadema?

Jaffary

JF-Expert Member
Oct 29, 2011
806
385
Baada ya tuhuma nzito ya moja ya chombo cha serikali TISS tunatarajia serikali kuwafungulia mashtaka wakati wowote kutoka sasa. Hii ni defamation kwa serikali na kama serikal haitachukua hatua yoyote itakuwa imetuaminisha sisi wananchi tusioamini juu ya matendo ya kinyama inayotuhumiwa kuyafanya. Kwa hiyo serikal sasa mda umefika kwa nyie kujisafisha mbele ya jamii kwa kuwaburuza hawa cdm mahkman
 
Kama "walivyomshtaki" Mengi kwa defarmation ya Polisi kupanga mpango na Manji wa kutaka kumwekea mtoto wa Mengi madawa ya kulevya! Wewe huijui hii serikali dhaifu inayoshirikiana na Wahalifu kuwabambikia kesi hata raia wake!
 
Believe me haiwezi kwenda mahakamani manake yatafumka mengi ya kuwaaibisha!!!! Nijuavyo mimi ni kuwa hadi CHADEMA wanaamua kutoa taarifa kama hizo basi wanakuwa na data kamili!!!!!
 
Wanatapatapa tu, hivi wanadhani usalama wa taifa wote ni mali yao? wako wengine wanamapenzi mema na nchi yetu hivyo hawawezi kuacha mbinu mbaya kama hizo zikapitishwa.

Wale mliotegemea CCM kama Mungu wenu sasa kaeni chonjo maana jahazi la CCM sasa linaelekea kuzama
 
  • Thanks
Reactions: GIB
Niliweka uzi wangu hapa kueleza mpasuko uliopo ndani ya TISS lakini imekuwa ikifutwa na mods kwa sababu wanazodai ni jazba na matusi kutoka kwa wachangiaji. Bado siamini kama hiyo ndio sababu au kuna jingine zito zaidi lililojificha nyuma ya pazia, lakini kwa vile namuheshimu Invisible ngoja niache tu.
 
Waende sasa hivi tena suluhisho la haki yetu watz ni afadhali tupigane maana nadharia inashindikana
 
Nasema mimi najipitia zangu tu,ila hawa jamaa dhaifu wanadhani wa tz wote ndiyo kama wao,sasa tumeamka. Waendelee kutajwa na wengine wengi tupo nao kitaa na majigambo ya ulevi hovyo.si mnajua pombe sio juice,naunga mkono hoja.
 
Niliweka uzi wangu hapa kueleza mpasuko uliopo ndani ya TISS lakini imekuwa ikifutwa na mods kwa sababu wanazodai ni jazba na matusi kutoka kwa wachangiaji. Bado siamini kama hiyo ndio sababu au kuna jingine zito zaidi lililojificha nyuma ya pazia, lakini kwa vile namuheshimu Invisible ngoja niache tu.

basi naomba un pm huo uzi kaka
 
Ile barua ya Mwakyembe kwenda kwa IGP Said Mwema ni Ushahidi wa kwanza maana Viongozi wa CDM walitajwa pia kwenye ile barua. Ushahidi mwingine ni ambao wanao wao wenyewe!
 
Jaffary ni wazi kwamba hili ni tamko lako binafsi yaani umetunga.
Una ubia na serikali weye?

Kichwa cha habari KIKUBWAA habari ndani nyembamba kama ubongo wa nzi. ( Nzi wa MM Mwanakijiji ana akili kwa sababu ni BioNzi)

We hukwenda MabwePande kwenye semina elekevu ya wapiga mizengwe hapa JF??

Au wamekuanzishia na dau dogo?? Tshs150,000 kwa mwezi?

Mvute chemba NAPE uongee naye vizuri.

Wenzio kuleta fujo hapa JF KCC ni Tshs750,00.00 kwa mwezi halafu wapo wanao lipwa $$$

Ukitaka kula PIG ( KITI MOTO) chagua yule alo nona ili hata ukifumaniwa uwe umefaidi vya kutosha.

Baada ya tuhuma nzito ya moja ya chombo cha serikali TISS tunatarajia serikali kuwafungulia mashtaka wakati wowote kutoka sasa. Hii ni defamation kwa serikali na kama serikal haitachukua hatua yoyote itakuwa imetuaminisha sisi wananchi tusioamini juu ya matendo ya kinyama inayotuhumiwa kuyafanya. Kwa hiyo serikal sasa mda umefika kwa nyie kujisafisha mbele ya jamii kwa kuwaburuza hawa cdm mahkman
 
Baada ya tuhuma nzito ya moja ya chombo cha serikali TISS tunatarajia serikali kuwafungulia mashtaka wakati wowote kutoka sasa. Hii ni defamation kwa serikali na kama serikal haitachukua hatua yoyote itakuwa imetuaminisha sisi wananchi tusioamini juu ya matendo ya kinyama inayotuhumiwa kuyafanya. Kwa hiyo serikal sasa mda umefika kwa nyie kujisafisha mbele ya jamii kwa kuwaburuza hawa cdm mahkman
Mahakama ipi hiyo? Ile ambayo jk tayari ameshaitolea hukumu dhidi mgomo wa madaktari na pia hukumu ya kesi ya Lema?
Tanzania kuna mahakama? Tanzania hakuna mihimili mingine kama unavyodanganywa (bunge, mahakama) bali ni serikali tu.
 
Back
Top Bottom