BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,116
Serikali kuwashirikisha Watanzania wa ughaibuni kujenga uchumi
2008-04-20 11:44:29
Na Mwandishi Maalum, London
Rais Jakaya Kikwete amesema serikali inatambua hazina kubwa ya uwezo wa kitaalam, nguvu kazi na hata uwezo wa kuwekeza walionao Watanzania wanaoishi ughaibuni.
Kwa kutambua hazina hiyo, alisema serikali imeunda kamati maalum ya kuangalia namna ya kuwashirikisha Watanzania hao katika kujenga na kuendeleza uchumi wa nchi katika mfumo rasmi pamoja na masuala mengine yanayohusu ustawi wa Watanzania hao hapa nchini.
Rais alisema hayo katika hotua yake iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Rais Dk. Ali Mohammed Shein, katika ufunguzi wa kongamano la kwanza la Watanzania wanaoishi Uingereza, lililofanyika Ijumaa mjini London, Uingereza.
Rais Kikwete aliwaeleza Watanzania hao kuwa idadi ya Watanzania wanaohamia nje kutafuta maslahi bora na kwa sababu nyingine, inazidi kuongezeka jambo ambalo linatoa changamoto kwa serikali kufikiria na kupanga namna ya kuwashirikisha watu hao katika maendeleo ya taifa.
``Hali hii inatoa changamoto kubwa kwetu sisi tulioko serikalini katika kubuni na kuandaa mikakati na sera za kuwatambua Watanzania hao na hatimae kuweka utaratibu wa kuwahamasisha ili waweze kuchangia kwa ukamilifu katika maendeleo ya taifa.
``Umoja wa Afrika ambao mimi ni Mwenyekiti wake, ulitangaza tangu mwaka 2003 kutambua Waafrika waishio nje ya bara letu kuwa jimbo rasmi.
Uamuzi huo ulitokana na mchango mkubwa wa Waafrika waishio ughaibuni katika uchumi wa nchi zao,`` alisema.
Kutokana na umuhimu huo, Rais Kikwete alisema kuanzia sasa serikali imeamua kuwahesabu Watanzania hao kama mkoa rasmi wa nchi na mipango ya maendeleo inapoandaliwa, itazingatia hilo pia.
Rais Kikwete alifafanua kuwa, Kamati Maalum iliyoundwa na serikali kwa sasa inaangalia masuala matatu ambayo kwanza ni kuwashirikisha Watanzania hao katika kujenga na kuendeleza uchumi wa nchi katika mfumo rasmi.
Alisema suala la pili ni la kufanya mchakato wa marekebisho ya sheria zinazohusiana na marejesho ya fedha na mikopo kwa watu waishio nje ili utaratibu wa Watanzania hao kufungua akaunti maalum zitakazorahisisha utumaji wa fedha nyumbani kwa kutumia mfumo rasmi.
Kwa mujibu wa Rais, jambo la tatu ni kupitia upya sheria ya uraia ili kuona uwezekano wa kuruhusu uraia wa nchi mbili na pia aliahidi kamati hiyo itapitia pia mapendekezo yatakayotolewa na mkutano huo.
Akitumia takwimu za Benki ya Dunia kuhusu mchango wa watu wanaoishi nje kwa nchi zao Rais Kikwete alisema watanzania wako nyuma wakilinganishwa na majirani zao wa Kenya.
``Hata majirani zetu wa Kenya, hupata mapato ya kutosha yatokanayo na raia wao waishio nje.
Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, Kenya mwaka 2006 iliingiza dola za Kimarekani bilioni moja, ikilinganishwa na dola milioni moja tu zilizorejeshwa Tanzania na Watanzania waishio ughaibuni,`` alisema.
Kuhusu kilio cha Watanzania hao cha kukosekana vivutio vya kuwahamasisha kuwekeza nyumbani, Rais aliwapa changamoto ya kuorodhesha mapendekezo ya vivutio ambavyo wao wanadhani vinafaa, na kuahidi serikali kuyafanyia kazi.
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Bi. Mwanaidi Sinare Maajar, akizungumza katika kongamano hilo, alisema miongoni mwa madhumuni ya Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Uingereza ni pamoja na kupata takwimu sahihi za Watanzania hao wa Uingereza na kufahamu shughuli wanazozifanya.
Kusudio jingine ni kuwahamasisha kurejesha fedha nchini Tanzania, kuhamasisha kampuni za nje zinazofanya shughuli zao Tanzania, kuajiri Watanzania walio nje wenye sifa zinazotakiwa na kuwaweka Watanzania walio nje karibu na serikali yao.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio Uingereza, Bw. Abubakar Faraji, alisema mkutano huo ni wa aina yake na kwamba umefungua njia katika kuiunga mkono kauli ya Rais Kikwete ya kuwataka Watanzania kuwekeza nyumbani.
Bw. Faraji alizishukuru kampuni zilizochangia kufanikisha mkutano huo za ZANTEL, TIGO, VODACOM, Benki za Posta, CRDB, Commercial Bank of Afrika, Western Union, Kampuni ya KPMG, Cargo Stars na Shirika la ndege Kenya Airways.
SOURCE: Nipashe