Serikali kuwarudisha watumishi 79 wa Balozi mbalimbali Nje ya Nchi

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Watumishi takribani 79 kurudishwa nchini waliomaliza muda wa kazi nje ya nchi.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, wa wizara ya Mambo ya Nje Bi Mindi Kasiga amesema miongoni mwa watumishi watakaorejea nchini wamo mabalozi, maafisa, wahasibu na makatibu muhtasi.

Wizara hiyo imejipanga kuwapeleka kwenye balozi zake nje watumishi wapatao 105 na kuwarejesha nchini wengine 79 ambao miongoni mwao muda wao wa utumishi katika balozi hizo umemalizika na wengine kustaafu kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma.

Wakati huohuo wizara imetolea maelezo ya ziara ya kikazi nchini Tanzania ya waziri wa Viwanda na Biashara wa Oman Mheshimiwa Dkt Ali Bin Masoud Al Sunaidy katika ziara hiyo waziri Al Sunaidy aliongozana na ujumbe wa watu 108 ambapo 12 walikuwa ni maafisa toka taasisi mbalimbali katika serikali ya Oman na wengine waliobakia toka sekta binafsi ndani ya nchi hiyo kwa lengo la kukutana na taasisi kama hizo nchini.
MINDI.jpg

Mkurugenzi wa kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,Wizara ya Mambo ya nje,Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa Bi Mindi Kasiga
 
Serikali ya Magufuli inafanya kazi kama vile ni opposition ndiyo wameingia madarakani ........ Au ni opposition ndani ya CCM!!? Hili zoezi nalo litacost kiasi!!
 
Back
Top Bottom