Serikali kuwarejesha kazini watumishi wote waliondolewa kimakosa nchi nzima

serikali.jpg
 
Hawa watu wa darasa la 7 na form 4 wangewaacha tu wabaki na uzoefu wao kazini na kuweka ceiling ya salary yaani utapanda mshahara mpaka level flani ili uvuke unahitajika uwe na sifa flani au ili uwe promoted kwenda hatua nyingine unatakiwa uwe na sifa flani (automatically wao wenyewe watajiongeza, kwanza wapo wachache na wengi wanaelekea kuwa wahenga hivyo wakija madogo watajishitukia wenyewe)
 
Mbona nafasi zao zimekuwa covered, mfano maafisa watendaji. Sasa wao wataenda kufanya kazi gani na wapi?
 
Mambo mengine yanauudhi,serikali inawayumbisha wafanyakazi sana na hali hii inapunguza molali wa kazi.
 
Mambo mengine yanauudhi,serikali inawayumbisha wafanyakazi sana na hali hii inapunguza molali wa kazi.
Na haya maandamano yanayosemekana, pia yanachochewa na vitu kama hivi.

Mtu unaondolewa kazini ghafla huku una madeni Benki, na sehemu nyingine, nyumba umepanga, watoto wako shule, mgonjwa yuko hospitali ni taabu tupu.

Uwe umeondolewa kwa haki au kuonewa yote ni taabu kwa wahusika na familia zinazowategemea.

Palihitajika Ubinadamu, Uungwana, Hekima na Busara kushughulikia yaha mambo,

Watumishi na wategemezi wao wameathirika sana na hizi harakaharaka za tumbuatumbua kwenye uhakiki wa vyeti na utendaji kazi zinazoendelea.

Watu wengi wameingia kwenye dhiki kubwa ya ghaflaghafla. Wengine wamefariki kwa taharuki na kukosa msaada wa kiuchumi na kijamii kwani hakuna pa kukimbilia.

Hawa ni binadamu na hii ni nchi yao wandugu. Juhudi zote za kuboresha utendaji kazi lazima zizingatie Utu wa Binadamu.

Kuna Leo na Kesho.
 
Yaani kama kuna wakati wananchi wanatakiwa kujionea ufahari ni huu. Kwa khaki ilivyo sasa tunakwenda kwenye wakati ambapo watawala wa kisiasa wanawahitaji wananchi kulikoni wananchi wanavyowahitajo watawalao hao.
Sasa hapa market as the situation means ni inshu ya sell & buy
Over
 
Vyeti feki kurdishwa kazini!
 
View attachment 706317

Video

Katibu Mkuu ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Dr Laurean Ndumbaro amesema watumishi waliondolewa kimakosa katika mfumo wa mishahara na utumishi katika zoezi la uhakiki wa vyeti feki na zoezi la kuondoa darasa la saba warudishwe kazini mara moja, aidha ameziagiza kwa kuziandikia barua mamlaka zote za ajira, mamlaka za mikoa na serikali za mitaa kuharakisha zoezi hilo,

Dr Ndumbaro alikua akiongea na waandishi wa habari nakuwajuza maamuzi hayo ya serikali amesema" Kama mtumishi aliajiriwa kwa sifa ya darasa la saba na faili lake linaonyesha amemaliza kidato cha nne huyo ni feki,

lakini kama mtumishi aliajiriwa kama darasa la saba tarehe 20.5.2004 na ameondolewa kwa kukosa sifa za kidato cha nne hao watarudishwa kazini haraka,

aidha amesema serikali bado inapitia rufaa za vyeti feki na hatima ya waliondolewa na ikimaliza zoezi hilo litatoa hatima ya watumishi hao katika matandao wake wa mawasiliano ya umma kwa kuchapisha majina ya watumishi wanaorejeshwa kazini"

Kama wameamua kuwarudisha basi wawarudishe wote na wawalipe stahiki zao zote. Hakuna sababu ya kuanza kuweka vimasharti vingine.
 
View attachment 706317

Video

Katibu Mkuu ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Dr Laurean Ndumbaro amesema watumishi waliondolewa kimakosa katika mfumo wa mishahara na utumishi katika zoezi la uhakiki wa vyeti feki na zoezi la kuondoa darasa la saba warudishwe kazini mara moja, aidha ameziagiza kwa kuziandikia barua mamlaka zote za ajira, mamlaka za mikoa na serikali za mitaa kuharakisha zoezi hilo,

Dr Ndumbaro alikua akiongea na waandishi wa habari nakuwajuza maamuzi hayo ya serikali amesema" Kama mtumishi aliajiriwa kwa sifa ya darasa la saba na faili lake linaonyesha amemaliza kidato cha nne huyo ni feki,

lakini kama mtumishi aliajiriwa kama darasa la saba tarehe 20.5.2004 na ameondolewa kwa kukosa sifa za kidato cha nne hao watarudishwa kazini haraka,

aidha amesema serikali bado inapitia rufaa za vyeti feki na hatima ya waliondolewa na ikimaliza zoezi hilo litatoa hatima ya watumishi hao katika matandao wake wa mawasiliano ya umma kwa kuchapisha majina ya watumishi wanaorejeshwa kazini"

Swali kwa huyo Waziri kwa akili yake timamua anasema walio ondolewa kimakosa nani alifanya hilo kosa kwann asichukuliwe hatua kwa ksababisha usumbuf mkubwa kwa serikali
 
Back
Top Bottom