Serikali kuwapatia viwanja Polisi ili wasifedheheke wakistaafu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,830
2,000
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. George Simbachawene, amesema kuwa wizara hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi watajadiliana na kuangalia namna nzuri ya kuweza kuwapatia viwanja askari polisi ili kuwaepusha na fedheha wale wanaostaafu na kujikuta hawana kiwanja wala nyumba.

SIMBAAAA.jpg

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. George Simbachawene

Kauli hiyo ameitoa Bungeni Jijini Dodoma hii leo Juni 8, 2021, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Agnesta Lambert, lililohoji umuhimu wa serikali kuweka utaratibu wa askari polisi kusamehewa kodi ya vifaa vya ujenzi na kupewa viwanja kwa bei elekezi ili kuwaepusha na njia za udanganyifu kwa kigezo cha kwamba wanajiandaa na maisha baada ya kustaafu.

"Askari polisi wanafanya kazi nzuri kwa taifa lao na pengine wanafanya hivyo katika mazingira magumu na wengine kulingana na vyeo vyao ni ngumu kujikomboa na kupata hata maisha mazuri baada ya kumaliza utumishi wao, nataka niseme tutajadiliana na wenzetu wa Wizara ya Ardhi tuone uwezekano wa kuwapatia viwanja, wengine wanastaafu na umri mdogo halafu hana hata nyumba wala kiwanja, tutaangalia namna ya kuwapatia viwanja angalau wale wa vyeo fulani fulani," amejibu Mh. Simbachawene.
 
Bambushka

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
2,739
2,000
Polisi pekee ndiyo watumishi nchi hii?

Walimu na mishahara yao duni hawahitaji viwanja? Hawahitaji unafuu wa bei?

Kupanga ni kuchagua hao wanaoadhirika wakistaafu, hawakujipanga.

Tuache upendeleo kwenye kada fulani.

Everyday is Saturday :cool:
 
Detective J

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
13,961
2,000
Raia ndiyo tunatakiwa kuishi maisha magumu?
maisha magumu ni concept pana.
Uchumi wa nchi,mzinguko wa pesa , ajira.
hayo mambo yana determine maisha yawe magumu au ya nafuu kwa watu wake.

Kama uchumi wa nchi wenyewe haujafika level za juu..kiasi kwamba hata budget tu ya ku run operation za serikal ni ya shida..
ww huku chini watakuona muda gani?

pambana upate chako. ikisubiria serikal ikuletee kiwanja na umekaa hapo.butangoja hadi unazeeka. hakuna serikal inatoa cha bure
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
49,061

Sisubiri isipokuwa nataka niwekewe mazingira mazuri
 
Janja weed

JF-Expert Member
Nov 20, 2020
1,097
2,000
Hii nchi inashangaza sana yani limtu kama Muroto na majigambo yote yale linakua hata halina kibanda baada ya kustaafu loh, na kwa jinsi yalivyo na roho mbaya yanatakiwa yakistaafu yasipate hata wa kuyatembelea wale jeuri yao ,wanapokua kazini wanasahau kama na wao ni binadamu na watafika kipindi watarudi kwenye jamii
 
Agresive

JF-Expert Member
Feb 18, 2018
589
1,000
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. George Simbachawene, amesema kuwa wizara hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi watajadiliana na kuangalia namna nzuri ya kuweza kuwapatia viwanja askari polisi ili kuwaepusha na fedheha wale wanaostaafu na kujikuta hawana kiwanja wala nyumba.

SIMBAAAA.jpg

Kauli hiyo ameitoa Bungeni Jijini Dodoma hii leo Juni 8, 2021, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Agnesta Lambert, lililohoji umuhimu wa serikali kuweka utaratibu wa askari polisi kusamehewa kodi ya vifaa vya ujenzi na kupewa viwanja kwa bei elekezi ili kuwaepusha na njia za udanganyifu kwa kigezo cha kwamba wanajiandaa na maisha baada ya kustaafu.

"Askari polisi wanafanya kazi nzuri kwa taifa lao na pengine wanafanya hivyo katika mazingira magumu na wengine kulingana na vyeo vyao ni ngumu kujikomboa na kupata hata maisha mazuri baada ya kumaliza utumishi wao, nataka niseme tutajadiliana na wenzetu wa Wizara ya Ardhi tuone uwezekano wa kuwapatia viwanja, wengine wanastaafu na umri mdogo halafu hana hata nyumba wala kiwanja, tutaangalia namna ya kuwapatia viwanja angalau wale wa vyeo fulani fulani," amejibu Mh. Simbachawene.
Usenge kabisa,,polisi,gani wanafanya kazi nzuri na kazi gani,,taasisi,imejaa rushwa tu .

Watu na pesa ya posho, wana mshahara leo tena wanawazia viwanja, kwa hiyo hii nchi polisi tu ndiyo wanashida.

Usenge kabis HUU
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom