Serikali kuwanyang'anya ardhi watu wenye Uraia wa Nchi mbili

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
SERIKALI imetangaza kuwanyang’anya umiliki wa ardhi watu wenye uraia wa nchi mbili na imeondoa tozo kubwa ya asilimia 67 iliyokuwa ikiwakwaza Watanzania na wawekezaji katika umiliki wa ardhi.

Hayo yalibainishwa jana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, alipokuwa akichangia na kujibu hoja mbalimbali zilizowasilishwa na wabunge,

Lukuvi alisema baada ya kuondoa tozo hiyo, kodi mpya itaanza kutumika Julai mwaka huu. Kwamba kama kuna mtu alikuwa anatakiwa kulipa Sh milioni 100 sasa atalipa Sh milioni 33, lengo likiwa ni kuwapa nafuu Watanzania wote waweze kumiliki ardhi na Serikali kupata mapato.

Alisema wawekezaji walikuwa hawawezi kufika Dodoma kwa sababu ya mkanganyiko wa umilikaji wa ardhi.

“Sasa hivi wenye hati za kumilii ardhi kwa miaka 33 wataendelea kupata hati za miaka 99 kama ilivyo kwa watu wengine nchini,” alisema.

Credit: Kulwa Mzee
 
Figa bado sijakuelewa. penye red, kama nalipa elfu 20 kwa sasa say, hapo pakoje?
 
Hadi leo hii sijajua Serikali inachohitaji kutoka kwa raia ni kitu gani haswa...
 
Back
Top Bottom