Serikali kuwadhibiti waajiri wanaokiuka haki za wajawazito


kilimasera

kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Messages
3,073
Likes
24
Points
135
Age
42
kilimasera

kilimasera

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2009
3,073 24 135
Wizara ya Kazi, Ajira na Mandeleo imepanga kufuatilia utekelezaji wa sheria ya haki ya mwanamke anapojifungua akiwa kazini.
Kaimu Kamishna wa wizara hiyo, Joseph Lugakingira, amesema kuna taarifa za kuwepo wanawake wanaokosa haki zinazoainishwa katika sheria hiyo, pindi wanapokuwa nje ya maeneo ya kazi kwa ajili ya likizo ya uzazi.
Lugakingira alisema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa kujadili utekelezaji wa sheria hiyo jijini Dar es Salaam.
Alisema baadhi ya waajiri wamekuwa wakiwanyima wanawake hao haki wanazostahili wakati na baada ya kujifungua.
"Mara nyingi wajawazito wanafukuzwa kazi na kutopewa haki zao za msingi, kama wizara tumeliona hili na tumeamua kulifuatilia kwa karibu, tutapitia mahali pa kazi kulifuatilia suala hilo," alisema
Aliongeza, "tunachotaka ni kwamba sheria hii itumiwe na wamiliki wa kampuni na ofisi kama ilivyo na si kuwanyanyasa wanawake pindi wanapokuwa wajawazito," alisema.
Aidha, alisema kama utekelezaji wa sheria hiyo ungefanyika ipasavyo, kungekuwa na mafanikio katika kupunguza vifo vya wajawazito vinavyotokea mara kwa mara.
Alizitaja baadhi ya haki zinazowastahili wajawazito kwa mujibu wa sheria hiyo kuwa ni kutoachishwa kazi, mapumziko yenye malipo kwa siku 84, likizo ya kawaida ya mwaka na kutobaguliwa.
Haki nyingine ni kupewa saa mbili za kunyonyesha ndani ya muda wa kazi kwa kila siku, siku tatu za likizo ya uzazi kwa wafanyakazi wanaume, kurejea kazini kwa maslahi na marupurupu na ulinzi wa afya ya mama na mtoto.
Aidha alisema waajiri wengi wamekuwa hawaifuati sheria hiyo na hatimaye kukwamisha maendeleo kwa wanawake.
 
R

Ruth

Member
Joined
Jul 27, 2009
Messages
27
Likes
2
Points
0
R

Ruth

Member
Joined Jul 27, 2009
27 2 0
Hii itasaidia sana, wanawake wengi wanapokuwa wajawazito mpaka kujifungua wamekuwa wakinyanyaswa hasa kwenye makampuni binafsi.
 

Forum statistics

Threads 1,250,056
Members 481,189
Posts 29,719,425