Serikali kuvifunga vituo vya watoto visivyo na kibali

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275

Amiri kilagalilia na Biligither nyoni-Njombe

Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo (daycare) wilayani wanging`ombe mkoani Njombe wametakiwa kufuata utaratibu wa usajili na kuonywa kuwa vituo vyote visivyofuata utaratibu vitafungiwa kuendesha shughuli zake.

Hayo yamesemwa na afisa ustawi wa jamii wa halmashauri ya wilaya ya Wanging’ombe Barnabas sichone,wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo amesema wamiliki wasiofuta utaratibu serikali haitawafumbia macho hivyo wanatakiwa kufuata sheria zilizopo ikiwa ni pamoja na kupata usajili ili kuweza kutoa malezi bora kwa watoto wanaowalea.

‘Nitoe onyo kwa wale wote ambao wanaanzisha daycares ambazo hazifati utaratibu,hakuna daycares yoyote ambayo inaruhusiwa kufunguliwa bila kupata kibali kutoka idara ya ustawi wa jamii na kwamba vile vituo vyote visivyofuta utaratibu vitafungiwa’ alisema Sichone

Akizungumzia umuhimu wa watoto kupata malezi kwenye vituo hivyo Sichone amesema kuna umuhimu mkubwa wa watoto kuwepo kwenye vituo kwa kuwa vinawajengea uwezo wa kujiamini,kushirikiana na wenzao pamoja na kujieleza.

‘katika malezi ya watoto kuna kitu tunaita malezi changamshi,na malezi changamshi yanaanzia kwenye ngazi ya familia na ngazi ya taasisi,kwenye ngazi ya familia wazazi wanakuwa ndo msaada mkubwa lakini kwenye taasisi kuna

walezi maalumu ambao wamepata mafunzo kwa ajili ya kulea watoto hivyo watoto wanalelewa kwa kupata malezi changamshi watoto inakuwa rahisi kungundulika mapungufu waliyonayo labda mtoto hajiamiamini,kuongea pamoja na kushrikiana na wenzake'alisema

Hata hivyo amesema mpango ya serikali katika kuvisimamia vituo hivyo ni kufanya usimamizi elekezi kwa kuvitembelea vituo hivyo mara kwa mara ili kuhakikisha watoto wanapata malezi yanayostahili.

‘mipango ya halmauri katika kuvisimamia hivi vituo ni kutoa usimamizi elekezi kwa kuvitembelea mara kwa mara ingawa tunauhaba wa maafisa katika kata lakini wanashirikiana na kamati za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto kuweza kuvitembelea'alisema Sichone

Nao baadhi ya wamiliki akiwemo Bahati Kiwambe,Aron Kabuka Pamoja na Jitunze Tweve, Licha ya kukiri kutokamilika kwa mahitaji yote katika vituo vyao lakini wameahidi kuboresha miundombinu ya vituo pamoja na kuviendesha kwa kufuata taratibu zilizo.

'sisi kama mmiliki wa vituo naona kuna umuhimu wa kuwa na vifaa changamshi kwa ajili ya watoto kwa kuwa vinachochea ukuaji pamoja na ubunifu lakini tunatakiwa kuviendesha kwa kufuata utaratibu'wamesema

Hata hivyo baadhi ya wazazi wamesema kuwepo kwa vituo hivyo kunawasaidia katika kuwalea watoto wao kutokana na wazazi wengi kujikita na shughuli za uzalishaji huku baadhi yao wakidai gharama kubwa zinasababisha kushindwa kuwapeleka kwenye vituo hivyo.
 
Back
Top Bottom