Serikali kuuza nyumba za wananchi wake kwa kukosa kulipa kodi ya malimbikizo ya kodi,inafikia shilingi 100000,ni sahihi?

kambale mnene

JF-Expert Member
Mar 15, 2022
271
197
Hodi wakuu!
Nimeingia na swali,serikali imeweka sheria za ukusanyaji kodi mbalimbali,ikiwemo ya majengo.
Sasa hivi kuna zoezi la ukusanyaji kodi kupitia mahakama za ardhi nchi nzima.

Kinachoendelea hapo mahakamani ni hukumu za kuuza nyumba za mtu ambae hajalipa hata kama anadaiwa laki tano.

Ndipo nauli hii ni sahihi?
Maana maisha kwa sasa ni magumu kuliko wakati wowote uliopita.
Mpaka chumvi imepanda bei.

Pamoja na hali ya maisha kupanda,tozo zote zipo palepale,leo wanataka kuuza nyumba za hao wanaowakamua mpaka damu inatoka baada ya maziwa kuisha.
 
Mkuu chanzo cha taarifa hii ni nini? Tujuze kwanza kabla kuumiza akili za kujadili
 
Hodi wakuu!
Nimeingia na swali,serikali imeweka sheria za ukusanyaji kodi mbalimbali,ikiwemo ya majengo.
Sasa hivi kuna zoezi la ukusanyaji kodi kupitia mahakama za ardhi nchi nzima.

Kinachoendelea hapo mahakamani ni hukumu za kuuza nyumba za mtu ambae hajalipa hata kama anadaiwa laki tano.

Ndipo nauli hii ni sahihi?
Maana maisha kwa sasa ni magumu kuliko wakati wowote uliopita.
Mpaka chumvi imepanda bei.

Pamoja na hali ya maisha kupanda,tozo zote zipo palepale,leo wanataka kuuza nyumba za hao wanaowakamua mpaka damu inatoka baada ya maziwa kuisha.
Kwani sasa kodi si wanakata kwenye luku? Hata isingekuwa hivi si sahihi kwani huo ni sawa na unyang'anyi mtu akumbushwe mbele ya mahakama kulipa ndani ya muda flan tofauti na hapo zifuate hatua nyingine.
 
Serikali haijatengeneza ardhi,haikumsaidia mtu kujenga,kajenga kwa nguvu zake na Kodi za vifaa vya ujenzi alilipa...Leo wanataka alipie jengo lake na ardhi,alishindwa wauze nyumba ili awe fukara hohehahe...ukoloni,unyama mtupu
 
Ni sawa hata huko mbeleni mtaachia viwanja maana kodi itathaminisha kutokana na ubora wa nyumba
 
Umeambiwa na nani? Utakamatwa kwa kuleta taharuki.
Mkuu kama hufahamu uliza,sheria mpya ya ardhi inaruhusu kuuzwa kwa eneo kufidia kodi!!

Sheria hii kandamizi ilipitishwa mwaka jana,ni sheria ambayo italeta tafaruku sana!!
 
Mkuu, kwanza hakuna sheria mpya ya ardhi. Upande wa ardhi sheria mpya ni ya mwaka 1999 iliyoanza kutumika 2001 kama si 2002.

Mbili hakuna mahakama ya ardhi inayokusanya kodi, si ya pango wala kodi ya ardhi. Nchi yetu inakusanya kodi ya aina mbili kwenye upande wa ardhi. Kodi ya jengo(pango) hii mwanzo ilikuwa ikilipwa kwa mamlaka ya serikali za mtaa(halmashauri), kisha ikahamishiwa TRA na baadae ikahamishiwa TANESCO(nimeandika hili kimuktadha).

Aina nyingine ya kodi ni kodi ya ardhi hii inalipwa kwa mamlaka ya serikali za mtaa kupitia mamlaka ya ardhi ya eneo husika.

Kodi ya ardhi Inapaswa ilipwe kwa maana ardhi ni mali ya watanzania na anayekabidhiwa umiliki hufanyiwa hivyo kwa masharti na mojawapo ni kukubali kulipa kodi ya ardhi elekezi. Kukosa kulipa kodi kunaondoa sifa ya umiliki. Ukiwa na malimbikizi mamlaka husika huandika notisi ya kudai kodi. Hii huja na tishio kuwa utapelekwa mahakamani na pengine mwenye ardhi ataiuza ardhi yako ili apate kodi yake.

Kuhusu swala la hukumu ya kuuza nyumba sijui ukweli wake ikiwa ni hivyo ushahidi wa ruling utasaidia sana. Jukwaa hili ni huru na mtu anaweza kuuleta.
 
Hata sijaelewa lolote!, Kodi ya nyumba inapelekea kuuzwa nyumba yako kivipi wakati kuna 1000 kila mwezi unakatwa?.
 
Nimeshuhudia Nyumba ikipigwa mnada.
Ikipigwa mnada kwa kushindwa kulipa kodi ya ardhi?

Mwenye uhalali wa kuidhinisha mnada huo ni raisi...madaraka aliyoyakasimisha kwa waziri husika. Kubatilisha umiliki wa mtu ni jambo gumu Kuliko unavyofikiri. Mchakato wa kupiga mnada nyumba kwa deni la kodi ni mrefu.
 
Tena ilikuwa imeandikwa kwa maandishi makubwa ya tarehe ya mnada.
 
Serikali haijatengeneza ardhi,haikumsaidia mtu kujenga,kajenga kwa nguvu zake na Kodi za vifaa vya ujenzi alilipa...Leo wanataka alipie jengo lake na ardhi,alishindwa wauze nyumba ili awe fukara hohehahe...ukoloni,unyama mtupu
Mkuu....
serikali haianzishi biashara na wanatoza kodi na wafanyabiashara wasipotoa kodi tunawaita wakwepa kodi.

kulipa Kodi kunaletaje umaskini? Nafikiri with proper systems kutolipa kodi ndio kunaleta umaskini.

Wananchi wanapaswa kuhoji juu ya kodi ya majengo kulipwa serikali kuu. Kodi ya pango inapaswa kuwa contributed Kulingana na huduma zinazowafikia wananchi. Ndio maana ratings zilikuwa zikifanywa kujua what has to be paid.

Ni halali kulipa kodi na ni wajibu sadly hata watoa elimu hawawezi kutoa maana kodi Inayotolewa haitendi kazi stahiki.
 
Tena ilikuwa imeandikwa kwa maandishi makubwa ya tarehe ya mnada.
Minada ya nyumba kwa agizo la mahakama au mabaraza ya ardhi ni jambo La kawaida, sijakutana na kesi ya kodi though. Kama yupo aliyetendewa hivyo basi atakuwa ni mwenye bahati mbaya zaidi.
 
Imeandikwa inapigwa mnada kwa kushindwa kulipa kodi ya Ardhi.
 
Mkuu....
serikali haianzishi biashara na wanatoza kodi na wafanyabiashara wasipotoa kodi tunawaita wakwepa kodi.

kulipa Kodi kunaletaje umaskini? Nafikiri with proper systems kutolipa kodi ndio kunaleta umaskini.

Wananchi wanapaswa kuhoji juu ya kodi ya majengo kulipwa serikali kuu. Kodi ya pango inapaswa kuwa contributed Kulingana na huduma zinazowafikia wananchi. Ndio maana ratings zilikuwa zikifanywa kujua what has to be paid.

Ni halali kulipa kodi na ni wajibu sadly hata watoa elimu hawawezi kutoa maana kodi Inayotolewa haitendi kazi stahiki.
Kodi ya jengo ni ulafi uso mantiki
 
Back
Top Bottom