Serikali kuunganisha wilaya kwa barabara za changarawe:Samia

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,107
18,322
Mh Samia akiwa arusha amewaeleza wananchi kuwa serikali iraunganisha wilaya zote kwa kuondoa barabara za vumbi na kuweka barabara za changarawe..ili wananchi waweze kupita kwa urahisi.


Hadi 2025 tutafika tumechoka
 
hukuelewa? kiswahili cha mzanzibar kitakupa taabu sana

alipofika kenya aliwaambia ametia dole kenyata alicheka sana
 
Kwani sasa hivi zina nini? Kuna barabara moja huku, kila mwaka msimu wa mvua ukiisha(sababu inakuwa imeharibika) wanaikarabati kwa kumwaga kifusi na mawe.
 
Unataka kusema Samia hajui neno lami, au kwa kipemba lami ni changarawe
hukuelewa? kiswahili cha mzanzibar kitakupa taabu sana

alipofika kenya aliwaambia ametia dole kenyata alicheka sana
 
Wakati wa JK walisema barabara zinazounganisha mikoa zote ziwekwe lami lakini mpaka leo bado.

Matharani barabara inayounganisha mkoa wa Morogoro na Tanga kupitia Tuliani-Mziha Handeni hadi leo ni bado ni kusadikika.

Barabara inayounganisha mkoa wa Tanga zidi ya Mkoa wa Manyara kupitia Wilaya ya Kilindi - Handeni bado ni kusadikika.

Inashangaza na kusikitisha sana.
 
Back
Top Bottom