JERUSALEMU
JF-Expert Member
- Sep 19, 2012
- 3,112
- 3,536
salamu wanajamvi!
kama kuna jambo ambalo binafsi linanikera ni hili la serikali kutunga sheria ambazo haiwezi kuzisimamia.Huwa najiuliza kwanini waliitunga wakati hakuna hata mtu mmoja anaye itekeleza na hakuna mtu anaisimamia kuona watu wanaifuata.Mfano mmoja ni sheria ya kuvuta sigara hadharani na kwenye mikusanyiko ya watu.Ukitembea barabarani unakutana na watu chungu mbovu wanavuta sigara kwa raha zao bila kizuizi chochote!
Mbaya zaidi unakuta miji yote haijajenga vibanda ambavyo mtu akitamani kuvuta sigara basi aende akajifungie na avute.
Ushari wangu serikali iwe inajipanga kuanda mazingira ya namna ya kutekeleza sheria zinazotungwa na bunge ili kulinda hadhi ya serikali na Bunge lenyewe.uholela umekuwa mwingi kiasi kwamba unashindwa kujua nani hasa anahusika kuona sheria zinafuatwa kikamilifu.