SERIKALI KUTUMIA Tzs. 100,000 KWA MAENDELEO NCHINI KWA MWAKA 2012/2013 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SERIKALI KUTUMIA Tzs. 100,000 KWA MAENDELEO NCHINI KWA MWAKA 2012/2013

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kwaroz, Jun 18, 2012.

 1. Kwaroz

  Kwaroz Member

  #1
  Jun 18, 2012
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Baada ya kusomwa kwa bajeti imenifanya nitafakari sana mambo kwa kina, wiki iliyopita Zitto Kabwe alisema kwamba kwa sasa kila Mtanzania aliye hai anadaiwa jumla ya kiasi Tzs. 488,888 ilinifanya niende mbali zaidi ya maneno hayo. Kwa kuangalia bajeti ya 2012/2013 nimeamua kuifafanua kwa urahisi ili hata yule mtu wa Gezaulole mwenye elimu na asiye na elimu haielewe. Mambo ya kuzingatia ni kama yafuatayo:

  1. Deni la Taifa kwa sasa ni Tzs. 22,000,000,000,000
  2. Jumla ya Watanzania woti ni 45,000,000
  3. Bajeti mpya ya Tanzania kwa mwaka 2012/2013 Tzs. 15,000,000,000,000

  Mahesabu ni kama ifuatavyo;

  A. Deni la kila Mtanzania = Deni la Tanzania/Idadi ya Watanzania
  = 22,000,000,000,000/45,000,000
  = 488,888.89

  Deni la kila Mtanzania aliye hai kama lingegawanywa kwa kila mmoja ni Tzs. 488,888.89

  B.
  Bajeti ya mwaka 2012/2013 kwa kila mtanzania mmoja = Bajeti ya 2012/2013/Idadi ya Watanzania
  =15,000,000,000,000/45,000,000
  = 333,333.33
  Bajeti ya kila Mtanzania kama ingegawanywa kwa kila moja kwa mwaka mzima ni Tzs. 333,333.33

  C. B
  ajeti ya mtanzania kwa siku moja = Bajeti kwa kila mtanzania/siku katika mwaka
  = 333,333.33/365
  = 913.24
  kwa siku moja bajeti ya kila mtanzania kama ingegawanya kwa kila mtu ni Tzs. 913.24

  D. Bajeti ya maendeleo kwa kila mtanzania kwa siku ni 30% ni 913.24*30% = 273.97

  E. Bajeti ya shuguli za utawala kwa kila mtanzania kwa siku ni 70% ambayo ni 913.24*70% = 639.27

  kwa mahesabu ya haraka hapo juu ni kwamba bajeti ya kila mtanzani kwa ajili ya maendeleo kwa mwaka ni Tzs. 100,000 na kwa ajili ya utawala (administration expenses) ni Tzs. 233.333.33.

  Note: Kwa mtazamo wa haraka bajeti ya mwaka 2012/2013 haitarajiwi na haitoweza kukidhi ndoto na matarajio ya watanzania kwa kuwa kiasi kilichotengwa ni kiasi kidogo sana cha pesa. pia kwa bajeti ya mwaka jana imethibitika kwama fedha iliyotengwa kwa maendeleo haikutumika yote isipokuwa ni 22% ndiyo ilitumika kuleta maendeleo lakini kwa upande wa expenses najua ni asilimia zote zilizotengwa zimetumika mpaka kumega bajeti ya maendeleo.

  USHAURI WANGU KWA SERIKALI
  Nikiwa kama mwananchi wa kawaida ningependa niungane mkono na wadau wengine ambao wamependekeza kwamba pesa zote za wafadhili zitumike katika kufanya miradi ya maendeleo na kuleta maendeleo tarajiwa kwa wananchi ili kuharakisha maendeleo kwa wananchi maana inaonyesha serikali imekuwa kama NGO kwa kufanya matumizi yasiyozingatia kipato cha Nchi na kuongeza uwanja wa kukusanya kodi na si kutegemea wafadhili.

  ANGALIZO: SIKU WAVUTA SIGARA NA WANYWAJI WATAKAPOGOMA KUTUMIA HUDUMA HUSIKA SIJUI ITAKUWAJE KWA NCHI HII.


  NI MTAZAMO WANGU
   
 2. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,628
  Likes Received: 2,047
  Trophy Points: 280
  Sina uhakika na takwimu zako lakini kiukweli nimependa jinsi ulivyoainisha hata kama wanasiasa wangekuwa wanaitafsiri budget kwa mtindo wananchi wangeelewa na kuchukua hatua maana mara nyingi wanasiasa wetu huwa wanataja vitu kwa ujumla mara utasikia serikali imetengenga milion 100 kwa ajili ya kulipa malimbikizo ya wafanyakazi ukija kwenye utekelezaji unakuta kuna wafanyakazi wamepewa mpaka alfu ishiriki. Good analysis
   
Loading...