Serikali kutumia milioni 740 kutengeneza mashine za X-ray za Ocean Road

Display Name

JF-Expert Member
Feb 11, 2014
410
500
Serikali kutumia milioni 740 kutengeneza mashine za X-ray za Ocean Road

SERIKALI imesema imeagiza mafundi na vifaa kutoka nchini Canada kwa ajili ya kutengeneza ya mashine mbili za mionzi zilizoharibika katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road ya jijini Dar es Salaam, ambao watawasili nchini wakati wowote kufanya kazi hiyo, matengenezo yanayotarajiwa kugharimu shilingi milioni 740.


Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Stephen Kebwe, ametoa kauli ya serikali leo Jumanne Mei 27, 2014 wakati akiwa katika mahojiano na FikraPevu na kusema kuwa serikali imefikia katika hatua hiyo baada ya kukosekana kwa huduma hiyo kwa muda.


Aidha, amesema kuwa matengenezo hayo yanategemewa kuchukua siku nne hadi kukamilika na tayari serikali imelipa kiasi cha shilingi 365,046,000 ikiwa ni nusu ya gharama zinazotakiwa.


Hata hivyo, amesema mashine zinazotoa tiba ya mionzi katika taasisi hiyo ni mbili na hutibu asilimia 95 ya wagonjwa wa saratani na wanaohitaji mionzi na pamoja na nyingine ndogo inayotumika kwa wagonjwa wachache hususani wenye saratani ya ngozi.


"Kwa kawaida mashine hizi zinatakiwa kufanyiwa matengenezo kila baada ya miezi mitatu, aidha mafundi wa kutengeneza mashine hizo wanatoka nje ya nchi hivyo kuharibika kwa mashine hizo kunasababisha wagonjwa kukosa huduma kwa muda" alisema Kebwe.

Amebainisha kuwa mashine zinazohitaji matengenezo ni Equinox no 2002, ambayo chanzo chake cha mionzi bado ni kizima, lakini kimeharibika na Equinox no 2004 inayohitaji chanzo kipya cha mionzi zitakazotengenezwa na kampuni ya Theratronics kutoka Canada ambayo ilipewa zabuni ya kutengeneza mashine hizo.


Alisema mwaka 2013/2014 Taasisi hiyo ilihudumia wagonjwa wapatao 4,712 wa Saratani, ikiwa ni ongezeko la wagonjwa 976, ikilinganishwa na kipindi cha mwezi Julai hadi Machi mwaka 2012/2013 waliofika katika taasisi hiyo.

Kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopo zinaonyesha kuwa takribani wagonjwa 3,295 walitibiwa kama wagonjwa wa nje na 1,417 walilazwa huku wanawake 4,985 walifanyiwa uchunguzi wa Saratani ya shingo na matiti ambapo kati ya hao wanawake 197 waligundulika kuwa na dalili za awali za Saratani ya kizazi na 61 walikuwa na dalili za kuwa na saratani ya matiti katika kipindi cha mwaka 2012/2013.

Chanzo:

[h=2]Serikali kutumia milioni 740 kutengeneza mashine za X-ray za Ocean Road[/h]
 

Bucktooth Maftaha

JF-Expert Member
Jun 27, 2012
379
225
Hizi hela mbona nyingi sana? Dola 470,000 kwa ukarabati wa mashine mbili tu? Hizi mashine mpya kwani zina bei gani? Wameshindwa kupata hata za Kichina?
 

pleo

JF-Expert Member
Jun 20, 2013
2,833
2,000
China unapata 4 mpya na moja ya nyongeza. Wasawasi ni usalama wa afya kwa wagonjwa watakazozitumia.

Hizi hela mbona nyingi sana? Dola 470,000 kwa ukarabati wa mashine mbili tu? Hizi mashine mpya kwani zina bei gani? Wameshindwa kupata hata za Kichina?
 

Nyalotsi

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
6,433
2,000
China unapata 4 mpya na moja ya nyongeza. Wasawasi ni usalama wa afya kwa wagonjwa watakazozitumia.

Mkuu utatokea ubishani mkali hapa. Weka source ya hii taarifa yako ili kuweka mambo sawa kama ilivyokuwa kwa ct scan.! Ie weka aina ya mashine na bei ya sokoni ili wote tukubaliane na wewe!
 

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
5,930
2,000
kwa uelewa wangu mashine nyingi za X RAY nchini ni za muda mrefu,na zinahitaji matengenezo makubwa au hata kubadilishwa.
Iko haja ya setikali kujipanga na kununua mashine hizi kwa wingi zaidi.
Kuhusu bei za matengenezo sitii neno
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom