Honorable GPA
Senior Member
- Mar 31, 2019
- 149
- 223
Jamani! Suala la wakuu wa shule kutuma majina ya walimu wanaojitolea ofisi ya Rais-tamisemi kwa lengo la kupatiwa ajira ni ubaguzi na siyo haki kabisa.
Kama mtakumbuka baada ya ajira kuwa ngumu! Serikali ilitoa tamko vijana kutafuta fursa kwenye mashirika na shule binafsi pia serikali ilisisitiza vijana kujiajiri kwa lengo la kujikwamua kimaisha kwa kipindi chote wakisubiria fursa za ajira zitakapotangazwa.
Kweli! Baada ya matamko hayo vijana wengi walianza kutafuta fursa kila mahali! Kwenye mashirika, shule binafsi, kufungua mabanda ya chips, kulima bustani etc.
Lakini! Leo katika hali ya kushangaza serikali inapita kuchukua majina ya walimu wanaojitolea shule za serikali ili wapatiwe ajira za moja kwa moja!
Kinacho nisikitisha ni namna zoezi hili lilivyofanywa! Mfano mimi nilipomaliza chuo 2017 nilienda kujitolea sekondari fulani hapa jijini Dar! Lakini mazingira niliyokutana nayo ikiwemo kunyanyaswa kingono na walimu waajiriwa na gharama za nauli 800 kwa siku! kusema kweli ilifikia hatua nikashindwa kuendelea!
Mwaka huu mwezi wa pili! Wilaya ya temeke ilipotanga uhitaji wa walimu wa kujitolea nilienda kwa bahati mbaya huko nako nilipofika nikaambiwa wameshajaa hawahitaji tena!
Kwahiyo! Serikali inapotaka walimu waliojitolea ndio waajiriwe tu naona kabisa haitutendei haki ni bora ajira ziwe kwa wote ila wakujitolea wapewe kipaumbele kwanza!
Kitu kingine! Kwenye utumaji majina si kweli majina yote yaliyotumwa walikuwa wakijitolea! Wengine wameandikwa baada ya kusikia ofisi ya Rais- tamisemi inayahitaji. Yaani mkuu wa shule anamwandika ndugu yake kisha anamwambia awe anajisogeza sogeza hapo shuleni ili siku team ya tamisemi ikipita kufanya ukaguzi imkute!
Sisi ambao hatujuani na hatukuwa na hela za kuwaonga wakuu wa shule watume majina yetu naona giza tuturu kwa upande wetu! naomba serikali ilitazame upya suala la kujitolea kwa mapana zaidi ili na sisi wanyonge tupate fursa ya ajira!