Serikali kutoza kodi viwanja vilivyo na title/offer/kimila

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
23,814
27,700
February 27, 2017
Dar-es-Salaam, Tanzania

Kuanzia Julai mwaka huu 2017 serikali kutoza kodi viwanja vyote mijini vilivyo na hati za kisheria yaani title/ offer na pia viwanja vya kimila au mauziano baina ya watu visivyo na hati.

Hii inatokana na serikali kubaini kuwa ilikuwa inatoza kodi kwa wale tu wenye title deed (hati miliki) wakati wamiliki waliokuwa hawana title/ offer au walikuwa wanamiliki kimila walikuwa hawatozwi kodi. Zoezi hili pia linasisitiza kuwa hata wale wanaomiliki viwanja ambavyo havijapimwa rasmi yaani squatters mijini pia wanatakiwa kulipa kodi.

Source: MCL Digital
 
Aisee, ila naunga mkono...serikali imechelewa hata hivyo. Lakini kwanini mtu akajisalimishe mwenyewe wakati kuna viongozi wa mitaa/ vijiji na mabalozi?
 
Unalipa kodi ya ardhi ambayo haijapimwa, kwanini?
Kama wanataka hiyo kodi kwanini wasipime hivyo viwanja?

Mtu analipa kodi ya ardhi na jengo kwakuwa assets hizo zinatambulika kisheria na anaweza kuzitumia katika kuboresha maisha yake. Sasa kama hakujapimwa kwanini watoto kodi? Kodi wanataka lakini huduma wanayopaswa kutoa kwanza hawaitaki. Huu ni muendelezo wa yale yale ya kutokujali wanyonge
 
Back
Top Bottom