Serikali kutochapisha takwimu za kiuchumi: Ifahamu IMF

Ukipingana na WB na IMF jiandae kula nyasi ,mwalimu Nyerere yalimkuta haya, maisha hayakuwa rahisi,kupata vitu kwa foreni mpaka aliposalimu amri,haya mabeberu sio ya mchezomchezo
Pia ukijifanya mjanja wanakufanya kama Libya, Syria, Iraq, Sudan na Venezuela.
 
Naona mnaanza kutafuta maoni ya watu kutoka jf kijanja baada ya kuona kuwa mmelibananga! Hamlikwepi hili linyweni hadi liishe!
Kwani mlisahau kuwa mna mkataba wa kikazi nao wa kuchapisha taarifa za kifedha kila baada ya miezi mitatu?
Mbona mnauvunja mkataba nao kibabe?
Mnasahau kuwa imf ni macho ya wawekezaji duniani kote? Mmewakimbiza wawekezaji wote na hata china itakimbia kwani inajua madhara ya kwenda kinyume na imf!
Bado mna muda wa kuomba poh na mkishupaza shingo zitakatikia bulawayo!
 
thetallest ,

..TZ ni wanachama wa WB na IMF tangu kipindi cha MWALIMU NYERERE.

..kwa hiyo tupime faida na hasara za kuwa wanachama wa taasisi hizo.

..na kama taasisi hizo zinatuzingua basi tunapaswa kujitoa.

..kuna nchi kama North Korea, na Cuba, siyo wanachama wa taasisi hizo kwa hiyo Tz tunao uwezo wa kujitoa pia.

Cc chige, Kobello
 
Hichi kipengere ndicho wanachotumia kutumaliza,kitaonyesha positive ikiwa umekubali kupelekeshwa,na ukigangamala lazima taarifa iwe negative,lengo ni makampuni makubwa ku-exploit,na yanatumia hii taasisi kama instrument kufanikisha malengo yao
Endelea kujitekenya huku ukicheke mwenyewe
 
Naona mnaanza kutafuta maoni ya watu kutoka jf kijanja baada ya kuona kuwa mmelibananga! Hamlikwepi hili linyweni hadi liishe!
Kwani mlisahau kuwa mna mkataba wa kikazi nao wa kuchapisha taarifa za kifedha kila baada ya miezi mitatu?
Mbona mnauvunja mkataba nao kibabe?
Mnasahau kuwa imf ni macho ya wawekezaji duniani kote? Mmewakimbiza wawekezaji wote na hata china itakimbia kwani inajua madhara ya kwenda kinyume na imf!
Bado mna muda wa kuomba poh na mkishupaza shingo zitakatikia bulawayo!
Pessimism
 
Ungeanza na sababu zinazofanya serikali kuficha takwimu zake, hadi kutunga sheria ni zipi ingekusaidia kabla ya kuomba msaada.
Kwa nini serikali inapenda kufanya mambo yote gizani, hata wananchi wake nao ni maadui wa kufichwa mafanikio ya kazi zao?
Nimeuliza pros na cons ya serikali kufanya hivyo,badala ya kunijuza wewe unahamisha goli
 
Ukipingana na WB na IMF jiandae kula nyasi ,mwalimu Nyerere yalimkuta haya, maisha hayakuwa rahisi,kupata vitu kwa foreni mpaka aliposalimu amri,haya mabeberu sio ya mchezomchezo
Bora useme mkuu. Ni aibu nchi kuongozwa na vilaza wasiotaka ushauri.
 
Hiyo namba 7 Leo ndo unauliza swali la mtindo huo?si huwa mnaambiwa humu nyie mnajifanya kuweka akili zenu makalioni?
Tatizo uzi unawazidi kimo,maelezo ya mtu mjinga sana ,hapa tunataka hoja zwnye mantiki watu wajifunze wewe unaleta funza,
 
Uchumi unapimwa kwa kutumia Circular flow theory ya Maynard Keynes or simply put as 'Keynesian Model'.

Hiyo picha ndio ina sum up kila kitu

View attachment 1076509

Kuna flows tofauti hapo kwenye picha and each has its own explanations, because this is not an economics class there is no point going into details.

For the purpose of economic growth kuna vitu viwili vinaangaliwa kutoka kwenye hiyo flow

Injections (vilivyochorwa na mstari wa kijani).
  • Government expenditure (G) mara nyingi ni miradi (japo nchi nyingine zinaweza weka na recurrent expenditure, hili alikubaliki; its a long debate to why so)
  • Exports (E)
  • Investment (I)zilizotumika kwenye maswala ya uwekezaji (kwa ivyo ukisikia tu bank imepunguza mikopo ya kibiashara ujue itaathiri ukuaji wa uchumi)
Mwisho wa siku sums of (G+E+I) ndio source ya ukuaji wa uchumi au vinavyoongeza mzunguko wa pesa

Withdrawals or leakage (Vilivyochorwa mstari mwekundu)
  • Imports (M)
  • Taxes (T)
  • Savings (S)
Na zenyewe zinajumlishwa (M+T+S) unapata picha ya kiasi gani uchumi umepoteza kwenye mzunguko

Kipimo rahisi ni kupitia; Injection - Withdrawals = positive answer implies growth whereas negative is vice-versa

Kupiga hesabu za GDP kinacho ongezwa ni Consumption/Expenditure (mstari wa blue) kwa kujumlisha all the amount ambazo watu wametumia roughly (its common to leave mircro businesses the sort of people Magu anaotaka wapewe vitambulisho badala ya kulipa kodi).

Kwa hiyo AD (GDP)= G + C + I + (X - M)

Kwa kuangalia hali ya Tanzania sasa

Government Expenditure (zimeongezeka)
Consumption (imeshuka)
Investment (zimeshuka)
Tuna deficit ya export and import

Clearly lazima uchumi ilikuwa ushuke tu maana factors zote zimepungua sana labda kilichoongezeka ni government investments.

Swala la IMF linaingia vipi na kwanini they matter that is another long story inabidi kwanza ufahamu historia ya kukopana, athari zilizotokea baada ya nchi kushindwa kulipa, sababu za kufanya risks assessment, sababu za kuendelea kusaidia nchi maskini and historical evolution ya policies za sasa and the reasons behind.

Sio kila kitu tunaonewa kama wanasiasa wanavyowaaminisha matatizo mengine tunajitengenezea wenyewe waafrika halafu tunataka kulaumu mzungu kwa kila kitu.
Angalau niseme katika wote waliochangia umejaribu kuelezea kwa ustadi,na kuna la kujifunza,asante,na ndio nilichotegemea kutoka kwa wachangiaji
 
Kama wewe sio mchumi usindandie uzi na mistari miwili

Google na usome Bretton Woods Institutions. Lakini in summary soma hapo chini. Kwa kifupi; ukigombana na mmoja wao usitarajie kupata mkopo nafuu mahali popote duniani.

The Bretton Woods Institutions are theWorld Bank, and the International Monetary Fund ( IMF ). They were set up at a meeting of 43 countries in Bretton Woods, New Hampshire, USA in July 1944. Their aims were to help rebuild the shattered postwar economy and to promote international economic cooperation.
 
Yaani leo CCM inawaona IMF ni wabaya. Narubiri siku mtakapowapiga pin na World Bank ndiyo utakuwa wanzo wa safari ya Zimbabwe.
Inabidi tukiwa kama Zimbabwe.tunaanza nao waliovaa kijani.na tikiwakuta wameweka bendera ya ccm ndio watakuwa wameshiba tunachukua chao
 
Summary ya kazi za IMF inachokifanya https://www.imf.org/en/About/Factsheets/Financial-System-Soundness

How they go about doing that businesses kuelewa au kuwa na interest zaidi in my opinion you need to be working in the DMO office wizara ya fedha maana huko it is to do with accepted accounting regulations and accepted use of formulas to assess the stability of various economic variable and applications of appropriate debt sustainability formulas, tofauti ya mikopo ya serikari na mashirika yake (ambayo inalipwa na mashirika yenyewe kama TANESCO et al), na mambo mengine luluki ambayo uoni faida yake to a layman kueelewa.

Beside ataukiweka mambo ya DeMPA, Brady Bonds, Policy zilizokuja kutokana na irresponsibility za watu kutoa mikopo ovyo na kuatharisha ulipaji wa madeni, etc etc etc ni vitu ambavyo pia mtu inabidi ajifunze zaidi mwenyewe.

Kitu cha kuelewa kuna mabenki au mataifa nyuma ya hizi hela tunazokopa wengi uwapa IMF ndio watukopeshe kwa niaba yao kwa maana hiyo kuna aspect of global finance uki default, someone somewhere in the world registers loss in his income statement.

Kwa historia ya karibu miaka ya 70-80 waarabu baada ya kujikuta wanahela za kuchezea za mafuta wakaanza kuwapa mabenki wakopeshe mataifa bila kupitia IMF. Matokeo nchi zikawa zinamadeni makubwa ya waarabu kupitia bank walizokopa jumlisha na madeni yao ya awali ya IMF nchi maskini nyingi sana zili default na kuwapelekea watu hasara (case studies ni nyingi)

Kutatua maswala kama hayo IMF huja na frameworks za kutaka kujua madeni ya nchi ya ndani, ilipokopa kwengine, its current liabilities, long term liabilities, etc, etc,etc Ripoti zao zina assess mambo yote hayo kusaidia watu wanaofikiria kuikopesha nchi kupata picha if the nation is credit worthy.

Haya mambo ya IMF if you're not into finance, public accounts or other specialized professions za public finance its complicated and long story na hakuna mtu yeyote anaeonewa basi tu waafrika ni watu wakulalamika.
 
Kuna mjadala kwa sasa unaendelea kuhusu serikali kugoma kuruhusu kuchapisha taarifa za majadiliano ya kiuchumi yaliofanyika, baina ya serikali na wadau wa IMF takwimu zinaozoonyesha uchumi wa Tanzania kukua kwa 4% badala ya 7% ilotarajiwa.
sababu zimeelezwa katika tafiti

Mjadala huu ningependa uwe wenye tija ,kwa maana ya kulisaidia taifa,dhidi ya kitu kinachoitwa vita vya kiuchumi,

Sina uzoefu sana na masuala ya kiuchumi,ila naamini wachumi wabobezi wazalendo wa kitanzania kwani nia ya dhati kabisa watatueleza kama ni kweli,
kwa nini serikali imegoma kuruhusu kutolewa tafiti hizo,kuna faida zipi na hasara ipi kwa kuzitoa au kutozitoa.

Pia ningependa kufahamu historia ya IMF ,

1,kuanzishwa kwake

2,kusudio la kuanzishwa kwake

3,Malengo ya kuanzishwa kwake

4,uaminifu wa taarifa zake kwa wanachama,especially nchi zinazoinukia kiuchumi

5,kilicho nyuma ya pazia kuhusu shirika hili ambacho hatukielewi,ispokua wachumi wabobezi mnakielewa.

6,chombo hiki cha kimataifa hakiwezi tumika kama siraha kwa baadhi ya mataifa yasiokubaliana na baadhi ya sera?

7,kama nchi, inajinasuaje na hali hii?.maswali ni mengi lakini naamini wachumi wabobezi wazalendo wasio na mlengo wowote wanaweza kutusaidia kujifunza kupitia uzi huu.
Heko kwa uzi huu maana michadema humu kushabikia chochote mradi kupinga. Hawajui asili ya imf na wb ni nini.
 
Back
Top Bottom