Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,188
Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani, inatarajia kutoa magari 700 ambayo yanatarajiwa kusambazwa katika wilaya na mikoa yote nchini kwa ajili ya kusaidia kukabiliana na vitendo vya uhalifu nchini.
Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Hamad Masauni, alisema hayo wakati akizindua kituo cha askari polisi wa majini na kukabidhi boti wilayani Chato mkoani Geita, itakayotumika kusaidia shughuli za ulinzi katika Ukanda wa Ziwa Victoria.
Masauni alieleza kuwa, Serikali imejipanga kupunguza tatizo la uhaba wa vitendea Kati na uchakavu wa vifaa vya Jeshi la Polisi kwa kununua magari ya kutosha.
Ni vyema katika kipindi hiki ambacho Serikali ya Awamu ya Tano inaboresha utendaji kazi wa Jeshi la Polisi kwa kulipatia vitendea kazi, tukumbuke kuwa, katika kipindi kilichopita, Jeshi hilo lilijikuta linategemea waliokuwa wakiitwa wadau kwa kuomba mafuta ya magari ama kupeleka kwenye matengenezo. Hili suala lilikuwa la aibu na ndilo lililosababisha kuwepo kwa kundi la watu wasioshikwa na Polisi, licha ya wengi wao kuwa wahalifu wakubwa.
Uamuzi huu wa Serikali ni wa kupongeza, ila Serikali ijitahidi kuongeza kasma ya Ofisi za Ma-OCDs kwani bado ni ndogo mno, in fact ni kama nil hasa kwa Wilaya za pembezoni.