kupelwa
JF-Expert Member
- Aug 24, 2011
- 1,087
- 450
Mnyika kaomba kwanini tunasikiliza upande mmoja tu wa serikali mbona kamati ya bunge na madaktari hawasikilizwi?
Siku ya leo kwenye kiti yupo naibu spika bwana job ndugai mhavizina wa serikali ya magamba, bila kujali masilahi ya umma.Bwana job ndugai , ameshakuwa na kinyongo na mhe.mnyikaHoja ya mnyika ni msingi mno.Ni muda sasa sula la madaktar lemkuwa na upotoshwaji wa wa serikali bila kubalance upande wa madaktari.
Pinda si mtoto wa mkulima , ni mpotoshaji , mara nyingi amekuwa hoja zake dhaifu kwa serikali yake.Hili swala serikali nawahakikishia wadau , taarifa ya kesho ni jazba, ubabe, upotoshaji , sababu, wao serikali wamefikisha tatizo hili hatua hiina hasa pinda mwenyewe.
Hivyo kujitetea ni kupotosha umma kwa kutumia askofu mokiwa, mashekhe; wao ndo wanaona ni jambo la msingi. Ni kweli serikali ni dhaifu, kukimbilia mahakamani ni kupoteza muda na si suluhisho. Serikali inafanya hivyo, kwa kuwa mahakama tanzania ni chombo cha serikali.
Nakumbuka miaka ya nyuma, mkuu wa wilaya na mkurungezi wa halmashauri ya kilosa, waliamua kukamata mifugo kama njia na kumaliza tatizo la migogoro ya wakulima na wafugaji. Utaratibu huo ulikuwa unakiuka haki za mifungo, haki za wafungaji, haki za binadamu.Baada ya hapo wadau wa mifugo wa wakalalamikia utekelezaji wake, na kuomba tamko la serikali.Aliibuka mtoto wa mkulima, akaropoka kama leo, akisema upuuzi wa kukimbilia mahakamani.
Mwisho wa siku alirudi kimya kimya kuwaomba waondoe dhamira yao ya kwenda mahakamani kwa sababu angeshughulikia tatizo lao.Hivyo siku zote pinda amekuwa hana jipya ni mpotoshaji ila anakingiwa kifua na bwana ndugai.
kimsingi hoja ya mnyika ni ya msingi tusikie na upande wa kamati ya bunge kunalipi kuliko kusikia matamko ya upotoshwaji huku serikali inakwepa kutatua matatizo ya kisekta.Kwenda makamani ni hatua dhaifu, kuliko hoja ya kutatua tatizo.
Hapa tayari serikali ina kesi hewa kuwa madaktari wana taasisi ya MART bali wana jumuiya ya madaktari, sijui watafungua kesi nyingine.