Serikali kutekeleza miradi ya maji kwa Tsh Bilioni 24.4 katika miji ya Tinde na Shelui, yawataka wananchi kutoihujumu

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,204
4,692
Matumizi sahihi ya Rasilimali zetu huleta matokeo chanya siku zote.

Ni fedha zinazotokana na makusanyo ya kodi zetu.

Tshs Bilioni 24.4 zimetolewa na Serikali kupeleka maji kwenye mji wa Tinde Shinyanga na Mji mdogo wa Shelui uliopo Wilaya ya Iramba Mkoani Singida.

Mkataba wa mradi huo umesainiwa na Wizara ya Maji kwa niaba ya Serikali ya awamu ya tano.

=======

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amewaonya wananchi wa Mji wa Tinde wilayani Shinyanga pamoja na Mji wa Shelui wilayani Ilamba mkoani Singida, wasihujumu ujenzi wa mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria ambao utatekelezwa kwenye miji hiyo kwa gharama ya Sh. Bilioni 24.4.

Waziri Aweso ametoa onyo hilo leo katika mji mdogo wa Tinde wilayani Shinyanga wakati wa utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa mradi huo wa maji kutoka Ziwa Victoria utakaopelekwa kwenye miji ya Tinde na Shelui, ambao ulisainiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Athony Sanga na Mkandarasi ambaye ataujenga mradi huo Morali Mohani, kutoka kampuni ya Megha Engeneering Construction ya nchini India.

Amesema fedha ambazo zinatekeleza mradi huo ni nyingi, na kuwaomba ushirikiano wananchi wa maeneo ambao unatekelezwa mradi huo, wasihujumu mradi wala kuiba vifaa vya ujenzi, bali wautunze vizuri ili upate kuwatatulia kero ya ukosefu wa maji safi na salama.

“Mradi huu wa maji safi na salama utawasaidia kuondokana na adha ya kutafuta maji salama umbari mrefu, pamoja na kupoteza muda wa kufanya shughuli za kiuchumi hivyo naomba muutunze,” amesema Aweso na kuongeza.

“Huu ni mradi wangu wa kwanza kusainiwa nikiwa Waziri wa Maji, nawaomba Wakandarasi vipo vya kuchezea lakini siyo mradi huu, umalizeni kwa wakati na hakutakuwa na muda wa nyongeza,”.

Pia amewaagiza wakandarasi wakati wa kuutekeleza mradi huo, vijana ambao ni wakazi wa Tinde na Shelui ndio watakao pewa kazi na siyo kutoka maeneo mengine, ili wapate vipato na kuinuka kiuchumi.

Aidha amezitaka mamlaka za maji ambazo zitakabidhiwa kuendesha mradi huo pale utakapo kamilika na kusambaza huduma ya maji kwa wananchi, wasitoze bili kubwa za maji, bali wafuate viwango vya bili ambazo zinasimamiwa na mamlaka ya udhibiti ubora wa nishati na maji Ewura.

Katika hatua nyingine, Waziri Aweso aliwaonya wahandisi wa maji hapa nchini, kuacha kufanya kazi kizembe, bali wajitume na kufanya kazi kwa weledi, ambapo watendaji wa namna hiyo hatowavumilia, na kubainisha mpaka sasa wamesha fukuzwa Wahandisi 100.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga, amesema fedha za utekelezaji wa mradi huo wa Sh. Bilioni 24.4 ni fedha za mkopo wa mashariti nafuu kutoka nchini India kupitia benk ya Exim, na kuonya kwenye mradi huo hakutakuwa na gharama za nyongeza bali fedha zilizotolewa ndio zitatumika kuukamilisha.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack, ameshukuru Rais Dk. John Magufuli kwa kutekeleza ahadi yake ya kupeleka huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa Tinde, na kuahidi Serikali kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi huyo ili asipate vikwazo vyovyote wakati wa utekelezaji.

Aidha Mbunge wa Jimbo la Solwa Ahmed Salum, amesema kwenye utekelezaji wa mradi huo wa maji vitanufaika vijiji 33, na hivyo kufanya Jimbo hilo hadi kufikia mwaka 2025, asilimia 95 ya wananchi watakuwa wakitumia maji safi na salama jimboni humo.

Nao baadhi ya wananchi ambao walihudhulia kwenye utiaji saini wa mradi huo mkubwa wa maji, akiwamo Happnes Makoye mkazi wa Tinde, amesema mradi huo utawasaidia kuondokana na shida ya kuamka mida ya usiku kufuata maji umbari mrefu, pamoja na kupoteza muda wa kufanyashughuli za kiuchumi.
 
Yafike haraka Dodoma! Haiwezekani Makao Makuu ya Nchi yanatumia maji yenye chumvi aka munyu kwa matumizi yao ya kila siku.
 
Serikali ya hovyo ya wapenda sifa.
Sitaiheshimu serikali hii mpaka nitakapokuwa mzee. Miaka 6 mshahara uleule. Huu ni zaidi ya usheitwani
Punguza hasira kwani msumari badouko kwenye nyama ukigusa mfupa ndio tutakapo ongea lugha moja
 
Matumizi sahihi ya Rasilimali zetu huleta matokeo chanya siku zote.

Ni fedha zinazotokana na makusanyo ya kodi zetu.

Tshs Bilioni 24.4 zimetolewa na Serikali kupeleka maji kwenye mji wa Tinde Shinyanga na Mji mdogo wa Shelui uliopo Wilaya ya Iramba Mkoani Singida.

Mkataba wa mradi huo umesainiwa na Wizara ya Maji kwa niaba ya Serikali ya awamu ya tano.

=======

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amewaonya wananchi wa Mji wa Tinde wilayani Shinyanga pamoja na Mji wa Shelui wilayani Ilamba mkoani Singida, wasihujumu ujenzi wa mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria ambao utatekelezwa kwenye miji hiyo kwa gharama ya Sh. Bilioni 24.4.

Waziri Aweso ametoa onyo hilo leo katika mji mdogo wa Tinde wilayani Shinyanga wakati wa utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa mradi huo wa maji kutoka Ziwa Victoria utakaopelekwa kwenye miji ya Tinde na Shelui, ambao ulisainiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Athony Sanga na Mkandarasi ambaye ataujenga mradi huo Morali Mohani, kutoka kampuni ya Megha Engeneering Construction ya nchini India.

Amesema fedha ambazo zinatekeleza mradi huo ni nyingi, na kuwaomba ushirikiano wananchi wa maeneo ambao unatekelezwa mradi huo, wasihujumu mradi wala kuiba vifaa vya ujenzi, bali wautunze vizuri ili upate kuwatatulia kero ya ukosefu wa maji safi na salama.

“Mradi huu wa maji safi na salama utawasaidia kuondokana na adha ya kutafuta maji salama umbari mrefu, pamoja na kupoteza muda wa kufanya shughuli za kiuchumi hivyo naomba muutunze,” amesema Aweso na kuongeza.

“Huu ni mradi wangu wa kwanza kusainiwa nikiwa Waziri wa Maji, nawaomba Wakandarasi vipo vya kuchezea lakini siyo mradi huu, umalizeni kwa wakati na hakutakuwa na muda wa nyongeza,”.

Pia amewaagiza wakandarasi wakati wa kuutekeleza mradi huo, vijana ambao ni wakazi wa Tinde na Shelui ndio watakao pewa kazi na siyo kutoka maeneo mengine, ili wapate vipato na kuinuka kiuchumi.

Aidha amezitaka mamlaka za maji ambazo zitakabidhiwa kuendesha mradi huo pale utakapo kamilika na kusambaza huduma ya maji kwa wananchi, wasitoze bili kubwa za maji, bali wafuate viwango vya bili ambazo zinasimamiwa na mamlaka ya udhibiti ubora wa nishati na maji Ewura.

Katika hatua nyingine, Waziri Aweso aliwaonya wahandisi wa maji hapa nchini, kuacha kufanya kazi kizembe, bali wajitume na kufanya kazi kwa weledi, ambapo watendaji wa namna hiyo hatowavumilia, na kubainisha mpaka sasa wamesha fukuzwa Wahandisi 100.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga, amesema fedha za utekelezaji wa mradi huo wa Sh. Bilioni 24.4 ni fedha za mkopo wa mashariti nafuu kutoka nchini India kupitia benk ya Exim, na kuonya kwenye mradi huo hakutakuwa na gharama za nyongeza bali fedha zilizotolewa ndio zitatumika kuukamilisha.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack, ameshukuru Rais Dk. John Magufuli kwa kutekeleza ahadi yake ya kupeleka huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa Tinde, na kuahidi Serikali kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi huyo ili asipate vikwazo vyovyote wakati wa utekelezaji.

Aidha Mbunge wa Jimbo la Solwa Ahmed Salum, amesema kwenye utekelezaji wa mradi huo wa maji vitanufaika vijiji 33, na hivyo kufanya Jimbo hilo hadi kufikia mwaka 2025, asilimia 95 ya wananchi watakuwa wakitumia maji safi na salama jimboni humo.

Nao baadhi ya wananchi ambao walihudhulia kwenye utiaji saini wa mradi huo mkubwa wa maji, akiwamo Happnes Makoye mkazi wa Tinde, amesema mradi huo utawasaidia kuondokana na shida ya kuamka mida ya usiku kufuata maji umbari mrefu, pamoja na kupoteza muda wa kufanyashughuli za kiuchumi.
Hata ukijikomba vipi hatuwezi kukupa uteuzi
 
Maji ya ziwa victoria si yameshafika Tabora, acha fix kusema eti wanayatoa tena toka Ziwa victoria.

Waungwana naomba kujua hili bomba linalokwenda ishelui linachukuliwa kuutokea tinde au litaanzia nzega? Ningependa kujua pia kama litapitia vijiji gani vya igunga na iramba
 
Back
Top Bottom