OSOKONI
JF-Expert Member
- Oct 20, 2011
- 10,965
- 5,336
Wapendwa wana JF nianze kwa kuwatakia heri ya mwaka mpya 2012, pokeeni baraka za mungu kwenye mwaka huu.
Ninachotaka tujadili ni hiki hapa:
Bunge kwa maana yake ndicho chombo cha juu kabisa cha kuwakilisha wananchi, bunge linatunga sheria, linaisimamia serikali nakutenda yote kwa niaba ya wananchi, Kwa nyakati tofauti bunge limekuwa likitoa maazimio mbalimbali kwa serikali mfano kamati ya Dr. Mwakyembe ilitoa mapendekezo 23 kwa serikali kwa ajili ya utekelezaji mfano bunge liliagiza serikali kuwachukulia hatua za kisheria wote waliohusika na kashfa ile wakiwepo mawaziri waliojiuzulu, mwanasheria mkuu na Dr. Hosea na wengine wengi lakini serikali haikufanya hivo.
Hivi karibuni kwenye kashfa ya Jairo na wenzie Bunge limetoa maazimio kadhaa kwa serikali kwa utekelezaji ikiwepo kuwachukulia hatua za kisheria Jiaro, Luhanjo, Ngeleja. CAG na wengine wote waliohusika serikali haijachukua wala haionyeshi dalili za kutekeleza, sasa pointi yangu ya mjadala ni hii utekelezaji wa maazimio ya bunge na serikali huwa ni lazima au serikali ina uhuru wa kutekeleza au kutokutekeleza??
Na je pale serikali kwa kiburi chake inapokataa kutekeleza maazimio ya bunge ambalo ndio sauti ya wananchi walioiweka madrakani serikali ni nini kinachotakiwa kufanywa na bunge??
Nawasilisha