Hiyo ni janja ili wasipandishe mishahara. Ni propaganda maana may mosi inakaribia.
 
Waziri Jenister Mhagama akitoa kauli ya Serikali bungeni kuhusu upungufu wa watumishi nchini, amesema Rais ameridhia na kutoa kibali cha kuajiri watumishi 30,000 na wiki ijayo atazitangaza.

Waziri Jenister Muhagama: Nasimama hapa kwa heshima kubwa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninaomba niwaarifu waheshimiwa wabunge, mheshimiwa Rais na Serikali yake wametambua tatizo hili la uhaba wa watumishi na hasa kwenye miradi ya sekta ya afya na sekta ya elimu na hivyo basi, mheshimiwa Rais ametoa kibali, ahadi ya Serikali katika mwaka huu wa fedha ilikuwa tuajiri watumishi elfu 44.

Tayari Serikali ilikwisha kuajiri watumishi wapya na watumishi wa ajira mbadala 12,000. Niwathibitishie wabunge, mheshimiwa Rais ameridhia na wiki ijayo nitatoa tangazo Rasmi la ajira 32,000 na utaratibu wa ajira hizo na mgawanyo wake katika sekta ambazo zinaongoza kwa uhaba wa watumishi, maelezo yote nitayatoa wiki ijayo.

===========================

Serikali imeyangaza kuwa itataoa ajira za watumishi 32,000 ambapo miradi ya afya na sekta ya elimu ndiyo watakaokuwa wanufaika wakubwa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Jenista Mhagama ameyasema hayo Bungeni leo Aprili 6, 2022.

“Kumekuwa na hofu kuhusu sekta ya elimu na afya, naomba niwaarifu kuwa Rais na Serikali yake wametambua tatizo la uhaba wa watumishi hasa kwenye miradi ya afya na sekta elimu, ahadi ya Serikali kwa mwaka huu wa fedha ilikuwa tuajiri watumishi 44,000.

“Tayari Serikali imeshapitisha watumishi wapya 12,000, naomba niwathibitishie kuwa Rais ameridhia na wiki ijayo tutatoa tangazo la ajira 32,000 mpya. Utaratibu na mgawanyo wake, maelezo yote nitayatoa wiki ijayo,” – Jenista Muhagama.
Unamuamini jenester? Genester kweli unamwamini? Huwa simpendi ingawa simchukii
 
Na hao malaki kadhaa walioko kitaa wanawassidiaje kuweza kupata mkate wa kila siku?
 
Back
Top Bottom