KabisaHuyu naye ni waziri mzigo.
😆😃Jiwe alifukuza ndugu zetu akisema vyeti feki huku akijaza wala sato kwenye vitengo
HATARI SANA HAWAYupo pale kwa nguvu za giza, ni kama Mwigulu Nchemba
Waziri MzigoKati ya mawaziri siwapi credit kabisa basi ni huyu, yai wameshindwa kuwa wabunifu kutengeza ajira kweli, mpaka wanatoa ajira kama bonus utafikiri sio haki kuwatengezea ajira Watanzania
Yaani Hizi Siasa Zinawatoa Akili SanaPorojo
Hawawezi ajiri 32k mbwembwe hizoWatu mwaka jana wakajipinda tuma maombi wizara...maombi tamisemi mwisho wa siku wakaajiriwa watu 20 Ajira walizoahidi 2000 sina hamu aisee sema ngoja tuonee
Kwani alisema kuhusu sekta ya afya na elimu?Kwani aliyesema maofisa wanazurula tu makoridoni ni nani?
Hao 12000 waliajiriwa linu?Waziri Jenister Mhagama akitoa kauli ya Serikali bungeni kuhusu upungufu wa watumishi nchini, amesema Rais ameridhia na kutoa kibali cha kuajiri watumishi 30,000 na wiki ijayo atazitangaza.
Waziri Jenister Muhagama: Nasimama hapa kwa heshima kubwa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninaomba niwaarifu waheshimiwa wabunge, mheshimiwa Rais na Serikali yake wametambua tatizo hili la uhaba wa watumishi na hasa kwenye miradi ya sekta ya afya na sekta ya elimu na hivyo basi, mheshimiwa Rais ametoa kibali, ahadi ya Serikali katika mwaka huu wa fedha ilikuwa tuajiri watumishi elfu 44.
Tayari Serikali ilikwisha kuajiri watumishi wapya na watumishi wa ajira mbadala 12,000. Niwathibitishie wabunge, mheshimiwa Rais ameridhia na wiki ijayo nitatoa tangazo Rasmi la ajira 32,000 na utaratibu wa ajira hizo na mgawanyo wake katika sekta ambazo zinaongoza kwa uhaba wa watumishi, maelezo yote nitayatoa wiki ijayo.
===========================
Serikali imeyangaza kuwa itataoa ajira za watumishi 32,000 ambapo miradi ya afya na sekta ya elimu ndiyo watakaokuwa wanufaika wakubwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Jenista Mhagama ameyasema hayo Bungeni leo Aprili 6, 2022.
“Kumekuwa na hofu kuhusu sekta ya elimu na afya, naomba niwaarifu kuwa Rais na Serikali yake wametambua tatizo la uhaba wa watumishi hasa kwenye miradi ya afya na sekta elimu, ahadi ya Serikali kwa mwaka huu wa fedha ilikuwa tuajiri watumishi 44,000.
“Tayari Serikali imeshapitisha watumishi wapya 12,000, naomba niwathibitishie kuwa Rais ameridhia na wiki ijayo tutatoa tangazo la ajira 32,000 mpya. Utaratibu na mgawanyo wake, maelezo yote nitayatoa wiki ijayo,” – Jenista Muhagama.
nami nakaziaWiki ijayo zikitangazwa mje mniambie
Vijana wa siku hizi mna shida, kama ww unazurura Halmashauri ndio unajua kila kitu ?! Kwann usijibu swali nililokuuliza ?!Sisi ambao tunazururazurura Huku Halmashauri nyingi na wakuu wa idara tunaelewa.. wewe hujui lolote, So usinisumbue mkuu kama hutaki pita kushoto na sikulazimishi ukubali nikisemacho