Magazetini

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
588
1,698
Waziri Jenister Mhagama akitoa kauli ya Serikali bungeni kuhusu upungufu wa watumishi nchini, amesema Rais ameridhia na kutoa kibali cha kuajiri watumishi 30,000 na wiki ijayo atazitangaza.

Waziri Jenister Muhagama: Nasimama hapa kwa heshima kubwa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninaomba niwaarifu waheshimiwa wabunge, mheshimiwa Rais na Serikali yake wametambua tatizo hili la uhaba wa watumishi na hasa kwenye miradi ya sekta ya afya na sekta ya elimu na hivyo basi, mheshimiwa Rais ametoa kibali, ahadi ya Serikali katika mwaka huu wa fedha ilikuwa tuajiri watumishi elfu 44.

Tayari Serikali ilikwisha kuajiri watumishi wapya na watumishi wa ajira mbadala 12,000. Niwathibitishie wabunge, mheshimiwa Rais ameridhia na wiki ijayo nitatoa tangazo Rasmi la ajira 32,000 na utaratibu wa ajira hizo na mgawanyo wake katika sekta ambazo zinaongoza kwa uhaba wa watumishi, maelezo yote nitayatoa wiki ijayo.

===========================

Serikali imeyangaza kuwa itataoa ajira za watumishi 32,000 ambapo miradi ya afya na sekta ya elimu ndiyo watakaokuwa wanufaika wakubwa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Jenista Mhagama ameyasema hayo Bungeni leo Aprili 6, 2022.

“Kumekuwa na hofu kuhusu sekta ya elimu na afya, naomba niwaarifu kuwa Rais na Serikali yake wametambua tatizo la uhaba wa watumishi hasa kwenye miradi ya afya na sekta elimu, ahadi ya Serikali kwa mwaka huu wa fedha ilikuwa tuajiri watumishi 44,000.

“Tayari Serikali imeshapitisha watumishi wapya 12,000, naomba niwathibitishie kuwa Rais ameridhia na wiki ijayo tutatoa tangazo la ajira 32,000 mpya. Utaratibu na mgawanyo wake, maelezo yote nitayatoa wiki ijayo,” – Jenista Muhagama.
 
Hayo yamesemwa na Jenifer Mhagama wakati akijibu swali bungeni.
Ameongeza kuwa serikali ilikusudia kuajiri watumishi 44000 ambapo tayari 12000 walishaajiriwa na tayari serikali imetoa kibali Cha ajira zingine 32000.

Source:Mwananchi

Nani Kama Samia
Namshukuru Samia kwa kupata bando la kupost humu JF
 
Waziri Jenister Mhagama akitoa kauli ya Serikali bungeni kuhusu upungufu wa watumishi nchini, amesema Rais ameridhia na kutoa kibali cha kuajiri watumishi 30,000 na wiki ijayo atazitangaza.

Waziri Jenister Muhagama: Nasimama hapa kwa heshima kubwa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninaomba niwaarifu waheshimiwa wabunge, mheshimiwa Rais na Serikali yake wametambua tatizo hili la uhaba wa watumishi na hasa kwenye miradi ya sekta ya afya na sekta ya elimu na hivyo basi, mheshimiwa Rais ametoa kibali, ahadi ya Serikali katika mwaka huu wa fedha ilikuwa tuajiri watumishi elfu 44.

Tayari Serikali ilikwisha kuajiri watumishi wapya na watumishi wa ajira mbadala 12,000. Niwathibitishie wabunge, mheshimiwa Rais ameridhia na wiki ijayo nitatoa tangazo Rasmi la ajira 32,000 na utaratibu wa ajira hizo na mgawanyo wake katika sekta ambazo zinaongoza kwa uhaba wa watumishi, maelezo yote nitayatoa wiki ijayo.

===========================

Serikali imeyangaza kuwa itataoa ajira za watumishi 32,000 ambapo miradi ya afya na sekta ya elimu ndiyo watakaokuwa wanufaika wakubwa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Jenista Mhagama ameyasema hayo Bungeni leo Aprili 6, 2022.

“Kumekuwa na hofu kuhusu sekta ya elimu na afya, naomba niwaarifu kuwa Rais na Serikali yake wametambua tatizo la uhaba wa watumishi hasa kwenye miradi ya afya na sekta elimu, ahadi ya Serikali kwa mwaka huu wa fedha ilikuwa tuajiri watumishi 44,000.

“Tayari Serikali imeshapitisha watumishi wapya 12,000, naomba niwathibitishie kuwa Rais ameridhia na wiki ijayo tutatoa tangazo la ajira 32,000 mpya. Utaratibu na mgawanyo wake, maelezo yote nitayatoa wiki ijayo,” – Jenista Muhagama.
Hawa watu wana ona sekta 2 pekee?
 
Kati ya mawaziri siwapi credit kabisa basi ni huyu, yai wameshindwa kuwa wabunifu kutengeza ajira kweli, mpaka wanatoa ajira kama bonus utafikiri sio haki kuwatengezea ajira Watanzania
Huyu mama atakuwa mshirikina sn, haiwezekani kila Rais akija ana mrudisha pale pale na wakati hakuna kitu anafanya zaidi ya usanii sanii
 
Yeye sioni kama anafanya mambo kwa maslahi ya wengi anglia mifuko sasa mfano wa NSSF hii mifuko ya jamii imekua ni tabu watu kuchukua chao kisa visheria alivyovipendekeza na vimekua mwiba kwa wajiriwa, mtu kapigika lakini mafao yake kuyapata ni shuhuli, hako kafao ka kujitoa imekua ni kero hata watumishi wanashindwa kuwajibu waajiriwa na waajiri kwa upupu uliowekwa
 
Yupo pale kwa nguvu za giza, ni kama Mwigulu Nchemba
 
Back
Top Bottom