Serikali kusitisha uchinjaji punda imechemka, ingehamasisha watu wafuge punda kwa wingi wapate pesa za kigeni

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,910
51,903
Serikali kusitisha uchinjaji punda imechemka ingehamasisha watu wafuge punda kwa wingi wapate pesa za kigeni

Soko la nyama za punda kubwa mno nchi za Asia

----

Serikali yasitisha uchinjaji punda​

Serikali imesitisha shughuli zote za biashara ya uchinjaji wa punda nchini kutokana na kupungua kwa idadi ya wanyama hao.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amesema hayo leo Jumatano Mei 25, 2022 wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka 2022/2023.

Mashimba amesema kutokana na kupungua kwa idadi ya punda nchini na hatari ya kutoweka kwa kizazi cha punda ambapo katika mwaka wa fedha 2021/2022 idadi ya punda ni takriban 650,000,

“Napenda kutumia fursa hii kuwataarifu wawekezaji waliowekeza katika machinjio za punda nchini watumie miundombinu ya machinjio hizo kwa ajili ya kuchinja na kuchakata aina nyingine za mifugo hususani ng’ombe, mbuzi na kondoo,”amesema.

Aidha, Mashimba amesema matukio ya ukamataji na utaifishaji wa mifugo usiofuata utaratibu hususani kwenye maeneo ya hifadhi yamepungua kutoka mifugo 6,245,356 iliyokamatwa mwaka 2020/2021 hadi mifugo 3,343 iliyokamatwa mwaka 2021/2022.

Amesema hiyo imetokana na wadau mbalimbali kuelewa Sheria ya Ustawi wa na kanuni ya Animal Welfare pamoja na sheria nyingine za nchi.

Punda.jpg
 
Safi sana wachina waache kabisa kumaliza nguvu kazi zetu. Punda wapo wachache halafu unawachinja Kila siku na Wala hufugi au huwazalishi
 
ng'ombe mbuzi kondoo kuku bata etc watanzania wameshindwa kufuga... bado wana taka na punda...

yapo mpaka matangazo ya kuamasishwa kunywa maziwa kwa msaada wa watu wa....

ndio watanzania walivyo, ni watu wakuamasishwa... wenyewe hawa wezi mpaka hamasa
 
Safi sana wachina waache kabisa kumaliza nguvu kazi zetu. Punda wapo wachache halafu unawachinja Kila siku na Wala hufugi au huwazalishi

Wewe akili huna hata kama imesema ulikariri hukuelewa ulichosoma

Serikali inachangia umaskini kwa watanzania

Karne hii kutegemea Punda kama nguvu kazi badala ya kuhamasisha wafugaji wafuge punda wenye soko sana wauza wanunue Toyo au pikipiki za kubeba mizigo au power tiller inaendekeza punda!!

Hivi wizara ya mifugo vichwani kwao kuko sawa au kuna nati zimefyatuka vichwani

Soko la punda kubwa mno lipo tayari .Hivi mtu wa kijijini punda waweza mfanya aondokane na umaskini kwa kutomuuza? Miaka nenda rudi punda wapo mbona umaskini huko kwa wafuge punda mbona haujaondoka ? Tena ndiko kwenye maskini wa kutupwa

Hiyo wizara inahitaji kufumuliwa wawekwe wenye akili na wanaojielewa na watetezi wa kweli wa mtu wa kijijini kuondokana na umaskini aache kutegemea nguvu kazi ya punda

Ni aibu kwa wizara au Waziri kutetea Punda kama nguvu kazi shame to him

Karne hii Waziri mzima unaongelea punda kama nguvu kazi aiseeeeee.Hopeless kabisa
 
Tutaendelea sana kuwategemea wazungu, imagine mpaka leo hatuna uwezo wa kuwazalisha punda wa kisasa (cross breed) ili tuwe nao wengi...
Kifupi wizara ya mifugo hopeless chuo cha kilimo sokoine hopeless na Vyuo vya mifugo hopeless na taasisi za utafiti mambo ya mifugo hopeless
 
Serikali kusitisha uchinjaji punda imechemka ingehamasisha watu wafuge punda kwa wingi wapate pesa za kigeni

Soko la nyama za punda kubwa mno nchi za Asia

----

Serikali yasitisha uchinjaji punda​

Serikali imesitisha shughuli zote za biashara ya uchinjaji wa punda nchini kutokana na kupungua kwa idadi ya wanyama hao.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amesema hayo leo Jumatano Mei 25, 2022 wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka 2022/2023.

Mashimba amesema kutokana na kupungua kwa idadi ya punda nchini na hatari ya kutoweka kwa kizazi cha punda ambapo katika mwaka wa fedha 2021/2022 idadi ya punda ni takriban 650,000,

“Napenda kutumia fursa hii kuwataarifu wawekezaji waliowekeza katika machinjio za punda nchini watumie miundombinu ya machinjio hizo kwa ajili ya kuchinja na kuchakata aina nyingine za mifugo hususani ng’ombe, mbuzi na kondoo,”amesema.

Aidha, Mashimba amesema matukio ya ukamataji na utaifishaji wa mifugo usiofuata utaratibu hususani kwenye maeneo ya hifadhi yamepungua kutoka mifugo 6,245,356 iliyokamatwa mwaka 2020/2021 hadi mifugo 3,343 iliyokamatwa mwaka 2021/2022.

Amesema hiyo imetokana na wadau mbalimbali kuelewa Sheria ya Ustawi wa na kanuni ya Animal Welfare pamoja na sheria nyingine za nchi.

View attachment 2238367
Uko sahihi mkuu,kumejaa wajinga huko Serikalini
 
Back
Top Bottom