Serikali Kushindana na JF?

M

MegaPyne

Guest
WanaJF.

Kwa kile ambacho naona kimetokea ni kwamba. Serikali kupitia DailyNews TSN wameanzisha forum yao.
 
WanaJF.

Kwa kile ambacho naona kimetokea ni kwamba. Serikali kupitia DailyNews TSN wameanzisha forum yao.

Link hii hapa:

http://forum.dailynews.habarileo.co.tz

anybody has a news on why it has started JUST NOW?

Wewe una mawazo kama mimi!...:) Baada ya kuyaona mabadiliko yaliyofanywa katika page ya Daily News Online na kuiona forum hiyo, nikasema wanajaribu kuiga umaarufu wa JF lakini sijui kama watakuwa na mafanikio makubwa kama ya JF ambayo sasa hivi ina traffic kubwa kuliko website yoyote ile Tanzania. Let's wait and see.
 
Nani mjinga atakaekwenda kupost kwenye site ya serikali issue serious?

Kuna jamaa mikocheni wapo kama nane hivi kazi yao ni kuingia JF na kuangalia nani anafanya/post nini, na sometimes nao wanajibu hoja humu. Mnajijua sina haja ya kuwataja.

Ila kama mnafanya kwa wema KAZI NZURI. Tunahitaji maendeleo ya wananchi walala hoi wa hii Danganyika country!
 
Tunawakaribisha kwenye "Dunia ya Hoja yenye Msingi na Ukweli siku zote hujitenga na Propaganda" Kwanza wangejiuliza kabla ya kuianzisha hiyo forums, kwanini Magazeti ya Habari Leo na Daily News hayana mvuto machoni pa Watanzania wengi. Dhiki na Matatizo yamezidi Tz huku Watawala wanaishi kama vile wako peponi.
 
Na hakika hiyo forum yao haitafika mahala popote kwa kuwa wengine hatuna hata chembe ya nia ya kutembelea hiyo link. Nafikiri wengi watakuwa na mtazamo kama wangu!! Nikatafute nini huku?? ??http://forum.dailynews.habarileo.co.tz, propaganda na ahadi zisizotekelezeka.
 
labda JF ikiwa na ushindani itazidi kujionesha kuwa ni ya pekee; kudos to them, watafute wanachotaka kusimamia. Miye naenda kujiunga nao nione how much button I can push.. ..
 
halafu nimecheki member list yao, nimeona jina Kikwete, sijui huyo ni Kikwete Mdogo au Kikwete mkubwa, au Kikwete mjomba,
 
niliwaambia kada si mwenzetu halafu ana asili ya kiasia mkakataa angalieni lugha in his/her typings
 
nadhani pia muwe waangalifu ambao mnajiunga kule kwani ni rahisi kuwa tracked and hakuna privacy kama JF kwani sijaona desclaimer ya administrators wao hawana statement ya kulinda ip za watu. Mnaokwenda kule sio mbaya mkajua hilo.

tangu nijiunge JF nimekua kiakili na sasa nategemea kuoa karibuni ingawa mnanibania michango yenu
 
Natumaini watakuwa wanaweka nyeti za jikoni kabla hazijapakuliwa bila kinyongo au kuwekana roho juu
 
......sidhani kama wamefanya kosa kuanzisha hiyo forum,
......nadhani kuwa mwanachama ni mapenzi ya mtu kwani nacho ni kijiwe kama vijiwe vingine ambavyo watu tunapenda kuchangia mawazo ya kujenga au ya kupoteza muda,
......sidhani kama mtu ukiwa mwanachama JF unakatazwa kuwa member wa forums nyingine,
......sidhani kama JF ipo against Daily news forum,
......nadhani kuwa forums zote zinalengo la kutoa habari na kupata habari na kuwawezesha watu kuchangia n.k na pia kusocialize,
......Sidhani kama mtu akichangia Daily news 'forum' tumeshampajezi ya kijani.

nawapa hongera daily news!!!!
tuendelee kukata issue.
 
Watavumilia madongo against serikali? Naona Mwanakijiji keshaanza kuwachokoza kuhusu Kiwira/Mkapa.
 
hata mie nimeitembelea na kusajili huko na imekuwa verry personal hamtanijua. ingawa moderator mmoja namfahamu personal kule.
nimeiona post ya Mzee Mwanakijiji
popote walipo tupo nao, tutalia na kucheka nao kwani hii ni nchi ya watanzania na sio wateule wachache
 
Mie nimemwona huko Willo,

Hili jina limenikumbusha wakatainshu wa BCStimes, narudia tena ES, Willo, Sam, Mkandara, Ogah, Kadogoo, Nyani Ngabu, Njabu Ngabu,.. nk...

Yaonesha kama DailyNews watasimamia kujirejista kwa majina likuki kwa mtu mmoja, wataweta kutaka issue kuipiku JF ya sasa!

Kitendo cha juzi Mbalamwezi aka Code Zero kujibu hoja(akashikwa pabaya na Ogah) kutuma message mbili kanakwamba ni watu tofauti kimeitia simamzi JF, kwani ni UTOTO!

NAJUA MLIOJIBALIDI MAJINA MNAYO ZAIDI YA TANO HUKU, MTAKUJA NA VIJIMAMBO NA VIJINENO KULIZUMGUMZIA HILI! Kwani ni fani yenu!
 
Mie nimemwona huko Willo,

Hili jina limenikumbusha wakatainshu wa BCStimes, narudia tena ES, Willo, Sam, Mkandara, Ogah, Kadogoo, Nyani Ngabu, Njabu Ngabu,.. nk...

Yaonesha kama DailyNews watasimamia kujirejista kwa majina lukuki kwa mtu mmoja, wataweta kutaka issue kuipiku JF ya sasa!

Kitendo cha juzi "Mbalamwezi" aka "Code Zero" kujijibu hoja(akashikwa pabaya na Ogah) kutuma message mbili kanakwamba ni watu tofauti kimeitia simamzi JF, kwani ni UTOTO!

NAJUA MLIOJIBALIDI MAJINA MNAYO ZAIDI YA TANO HUKU, MTAKUJA NA VIJIMAMBO NA VIJINENO KULIZUMGUMZIA HILI!
Kwani ni fani yenu!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom