mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,219
- 6,650
Nimeisikia muda huu kupitia channel Ten Waziri mhusika akilisema hilo. Faida alizozitaja (pato kwa Serikali na Ajira) hazihakisi thamani ya madini ambayo ni "non-renewable natural resource). Watachimba na kuacha mashimo (uchumi usio endelevu)
Kama Serikali ina nia ya dhati ya nchi kuwa na uchumi endelevu iweke mazingira rafiki ya uwekezaji kwenye kilimo na uchumi wa bluu. Nchi ina ardhi ya kutosha yenye rutuba pia ina mito, maziwa kwa ajili ya uvuvi na umwagiliaji.
Vilevile ina ukanda wa bahari wa kuwezesha uvuvi. Sekta ya kilimo na uvuvi siyo tu zitaongeza nafasi za ajira bali zitatoa nafasi kwa ujenzi wa viwanda vya kuongeza thamani ya mazao yake.