Serikali kupuuzia maadhimisho ya sherehe za Muungano, Watanzania sio wajinga tena...

kasenene

JF-Expert Member
Jun 6, 2008
1,632
2,413
Kwa namna yoyote ile hakuna muumini wa kweli wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar atakwa ameipokea vyema kauli ya serikali ya kuamua kuzima na kuyafutilia mbali maadhimisho ya sherehe za muungano mwaka huu tena bila ya sababu angalau za "kudaganyia" kama tulivyozoea.

Na pengine hii imezidi kuifunulia dunia na kuweza kutambua kuwa viongozi wa sasa wa nchi yetu hawakuwahi kumuelewa Marehemu Mwalimu juu ya nia yake kuuenzi Muungano au hawaoni umuhimu wa kuwepo kwa muungano wa hizi nchi mbili zaidi ya kuona aibu ya kwamba wasijeonekana kuwa wao ndiyo walikuwa chanzo cha kuumalzia muungano. Watani zangu wahaya wanao msemo usemao "kitandugao".
 
Kwa namna yoyote ile hakuna muumini wa kweli wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar atakwa ameipokea vyema kauli ya serikali ya kuamua kuzima na kuyafutilia mbali maadhimisho ya sherehe za muungano mwaka huu tena bila ya sababu angalau za "kudaganyia" kama tulivyozoea...Na pengine hii imezidi kuifunulia dunia na kuweza kutambua kuwa viongozi wa sasa wa nchi yetu hawakuwahi kumuelewa Marehemu Mwalimu juu ya nia yake kuuenzi Muungano au hawaoni umuhimu wa kuwepo kwa muungano wa hizi nchi mbili zaidi ya kuona aibu ya kwamba wasijeonekana kuwa wao ndiyo walikuwa chanzo cha kuumalzia muungano. Watani zangu wahaya wanao msemo usemao "kitandugao".
Hawana hela nakuambia hawana hela hakuna kifung cha bajeti kina hela hiyo mishahara ni kubahatisha
 
Mkuu, mie nipo tofauti kidogo nawe. Nadhani serikali inachukua maamuzi sahihi kutokuwa na misherehe lukuki kwa maadhimisho kama vile ndo tukio linatokea. Tujenge nchi na hizi ziwe kumbukumbu tu kama siku ya kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi.
Hapana aisee. Sherehe muhimu kwa nchi yetu ni siku ya Uhuru na Muungano. Watoto wetu watajifunza nini baadae halafu mnataka watu wawe wazalendo wakati siku hizo muhimu zimekua zinachukuliwa kama sherehe za ccm hauko serious
 
Tangu magu kaingia madaraka sikumbuki kama Tanzania imesheherekea siku ya uhuru. Kila mwaka hela inaenda kufanya jambo lingine. Leo tena siku ya muungano inapigwa danadana
Hii ni muungano...sio uhuru
 
Unawezaje kuahirisha jambo kubwa kama hilo bila kuwashirikisha watanzania?...juzi tu wao wamekasirika kisa hawakushirikishwa kwenye ripoti ya IMF
 
Naunga mkono serikali kwa kutopoteza pesa kwenye sherehe nyingi zinazolibebesha mzigo taifa
 
Hapana aisee. Sherehe muhimu kwa nchi yetu ni siku ya Uhuru na Muungano. Watoto wetu watajifunza nini baadae halafu mnataka watu wawe wazalendo wakati siku hizo muhimu zimekua zinachukuliwa kama sherehe za ccm hauko serious
Zina umuhimu, lakini kiuhalisia hatuwezi ku afford sherehe kama hizo kila mwaka

Matatizo ya watanzania ni mengi mno, huduma za msingi kama zahanati, maji safi tu ni mtihani

Halafu tufanye sherehe za uhuru, muungano zinazogharimu mabilioni na bado watu hawaendi kazini
 
Siku hizi wanakata wapinzani wooote kisha wa CCM anapita bila kupingwa...Wame save gharama, hahaaa
Bado utaambiwa kuna kama m200 zimetumika hapo so far.. Wanajifanya wanachukia ubadhirifu kumbe wenyewe ndo wanaoongoza kwa ubadhirifu..
 
Zina umuhimu, lakini kiuhalisia hatuwezi ku afford sherehe kama hizo kila mwaka

Matatizo ya watanzania ni mengi mno, huduma za msingi kama zahanati, maji safi tu ni mtihani

Halafu tufanye sherehe za uhuru, muungano zinazogharimu mabilioni na bado watu hawaendi kazini
Mandege na billions of money zinazopotea unnecessarily kwanini zisinge enda kwenye hizo huduma muhimu. Kwan marais wengine waliwezaje kubalance??
 
Gharama za kukumbuka Muungano na kuzidi kuuenzi /kuuhamasisha, zinatokana na nini?
 
Kuna umuhimu wa kuwepo sherehe hizo lakini la msingi ni kuwa nini kifanyike siku ya sikukuu hiyo. Tubadilike sio lazima tufanye gwaride na mambo ambayo nadhani yataingizia nchi gharama kubwa sana lakini tuwe na sherehe itakyo onyesha tunaenzi muungano huo kwani kutofanya chochote na kuita sikukuu haitakuwa na maana. Watoto wetu wanatakiwa waone tunavyoezi sikukuu hiyo. Ubunifu unatakiwa kuhakikisha tunaendelea kusherekea sherehe zote za kitaifa kwa gharama ndogo.
 
Mkuu, mie nipo tofauti kidogo nawe. Nadhani serikali inachukua maamuzi sahihi kutokuwa na misherehe lukuki kwa maadhimisho kama vile ndo tukio linatokea. Tujenge nchi na hizi ziwe kumbukumbu tu kama siku ya kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi.
Wewe sema unavyosema sababu una huo uhuru lakini kwa Mwendo huu tutaendelea kupunguza kiwango cha uimarishaji wa uzalendo.

Sikukuu za uhuru wa Tanganyika (December 9, 1961) mapunduzi ya Zanzibar (January 12, 1964) na siku ya Muumgano (April 26, 1964) ni siku za muhimu sana kwa taifa letu na sikukuu haziwezi kuwa lukuki.
 
Back
Top Bottom