Serikali kupitia Wizara ya Elimu itupie macho vyuo vyenye vyenye kashfa nchini! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali kupitia Wizara ya Elimu itupie macho vyuo vyenye vyenye kashfa nchini!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by mmaroroi, Oct 30, 2011.

 1. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2011
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kuna vyuo mbalimbali vilivyokumbwa na kashfa mbalimbali nchini, suala hili lisipochuliwa hatua litaidhalilisha elimu ya Tanzania. Mfano Chuo cha Ustawi wa Jamii Kijitonyama ilishakubwa na kashfa na Serikali ikachukua hatua na inaendelea kuchukua hatua. Hivyo ni vema ikachukuliwa hatua pia kwa vyuo vingine ili kulinda heshima ya elimu yetu kwa manufaa ya Taifa letu. WanaJF tusaidiane kutaja vyuo vyote vyenye kashfa mbalimbali katika elimu. Mojawapo ya Vyuo hivyo ni CBE ilishawahi kukumbwa na kashfa ya kuhonga Fedha ili mwanafunzi afaulu. Chuo Kingine ni UDOM kukumbwa na Kashfa ya kutoa maksi kwa masomo yasiyofundishwa kwa kutokuwepo wahadhiri. Chuo kingine ni MNMA kimetolewa na Gzeti la DIRA kukumbwa na kashfa ya ngono (aibu tupu) na mambo mengi kadhaa utadhani haina uongozi. Serikali ichukue hatua haraka kwani kuyalea haya ni hatari sana kwa mustakabali wa taifa letu. Wanajamvi toeni maoni yenu na mtaje vyuo vingine.
   
 2. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Serikali iko likizo kwa sasa.
   
 3. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2011
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sasa tufanye nini maana kama kuna Mafisadi wa Elimu na Vyuo hali ndio hiyo hali ni tete mbele ya safari.
   
 4. Pdraze

  Pdraze JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2011
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 611
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Kashfa nyingine umebuni wewe mbona hujatoa source ulipozipata!!
   
 5. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2011
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Source Gazeti la Dira ya Mtanzania Tolea la 126, Alhamisi Oktoba 27-30, 2011. Huna utafiti huna haki ya kuongea, niombe radhi.
   
 6. Pdraze

  Pdraze JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2011
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 611
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Siwezi kukuomba radhi we hadi leo unayatumia magazeti ya bongo kudhibitisha ukweli wa kitu?
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,337
  Likes Received: 19,509
  Trophy Points: 280
  kama/?
   
 8. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #8
  Oct 31, 2011
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sikubaliani wewe kwani ufisadi uliotokea hapa nchini ni magazeti ya hapa ndio yalianza kufichua yakabishwa hatimaye ikawa kweli hapo unasemaje.Au kwani nini basi usichunguze kabla ya kurukia kubisha bila utafiti.Tanzania inabaki nyuma kwasababu ya watu kama wewe.Kwa hiyo wewe huamini yanayoandikwa na magazeti hapa nchini?WanaJF tumsaidie ndugu huyu maana anawakilisha Watanzania wengi wasioamini yanayoandikwa na magazeti makini.Naliomba gazeti la DIRA liendelee kufichua maovu katika Vyuo vyetu na nchi yetu kwa ujumla.
   
 9. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #9
  Nov 3, 2011
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  WanaJF ili kuondoa ufisadi katika elimu ni muhimu kutoa maoni kwa serikali yetu namna ya kushughulikia tatizo hili.
   
 10. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #10
  Nov 3, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Katika utafiti wangu japo sijamalizia analysis,lakini nimegundua mawaziri wengi kama sio wote wanateuliwa SI kwa mujibu wa uwezo wao...., bali kulingana na mahusiano,interests binafsi za mtawala,ama kama jamii au kikundi fulani cha watu kimetokea kuupenda ushupavu wa mbunge fulani,mtawala anaona airidhishe jamii ile kwa kumteua huyo. Matokeo yake ni kushindwa kuwajibika ipasavyo,na panapo kuwajibika utata na mtawala unaonekana. Rejea,mbunge wa Chato na JMK na mama Tiba,au mambo ya kina IMMA Advocates,na uwaziri na ujaji n.k. unganisha S. Kawambwa mara mawasiliano mara elimu sasa.Ongezea JKM na Pinda,mambo ya Jairo,na Katibu Kiongozi.Na kuachwa kichwa adimu cha Gharib Bilal kiwe kama mapambo.Mambo kama hayo. Pia ni udhaifu tu wa kawaida ambao Katiba mpya haina budi kuyaondoa.Yaani mbunge anapoteuliwa kuwa waziri,anawajibika zaidi kwa serikali kuliko wananchi waliompeleka huko bungeni. Lakini watu haohao waambie nyie ni TUME ya jambo mfano Elimu,utaona matokeo yake.Utafahamu ndani mpaka nje matatizo katika elimu yanasababishwa na nini, na njia za kujikwamua kuboresha elimu yetu. Mimi pia napenda zaidi tume...kwani zinafanya kazi kwa UHURU. Nafikiri hata MICHEZO ili kujikwamua tuunde tume tuipe hadidu za rejea,kama tatizo ni kocha wa kigeni itajulikana,kama sio itajulikana..na namna ya kufanya ili kujikwamua.
   
 11. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #11
  Nov 3, 2011
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Nakubaliana na wewe kuwa haya ndiyo yanayochangia kushusha hadhi ya elimu yetu. Sasa nashauri tufichue Vyuo vyote vyenye kashfa kama ya ngono, vyeti bandia na usanii kwa ujumla katika elimu. Vyuo vyenye matatizo haya viongozi wa taasisi hizo wawajibishwe.
   
 12. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #12
  Nov 4, 2011
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Toa mchango wako turekebishe vyuo vyetu na elimu inayotolewa.
   
 13. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #13
  Nov 6, 2011
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kwanini serikali yetu inayafumbia macho kashfa za ngono katika vyuo vya elimu ya juu?Kweli tunakubaliana na digrii za chupi?Waziri wa elimu tafakari na uchukue hatua.
   
 14. l

  lowamond Member

  #14
  Nov 8, 2011
  Joined: Nov 2, 2011
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kaka hiyo ya UDOM ndo nasikia toka kwako,.UDOM Haijawahi kukutwa na kashfa ya kugawa marks kwa masomo ambayo hayana walimu.Ikitokea somo halina Walimu Huwa wanachukua wa part time na wakikosekana somo hl hufutwa kwa semista hy..Mi nimema graduate hp UDOM.
   
Loading...