GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,073
- 107,563
Jana wakati nikiwa nasikilizika Redio One hasa Kipindi chao cha Michezo nilipatwa na ' Mshtuko ' kidogo pale niliposikia ya kwamba kuna Bondia mmoja nchini Tanzania ( bahati mbaya nimemsahau Jina ila kama kuna anayemkumbuka anisaidie Kumtaja hapa ) tena kwa ' Kujigamba ' kama siyo ' Kujishebua ' kabisa kuwa anataka apambanishwe na Bondia Bingwa duniani Flyod Myweither na ana uhakika kuwa atampiga asubuhi ( mapema ) tu.
Serikali na Waziri Mwakyembe nadhani Tanzania kwa sasa bado tupo katika ' Majonzi ' makubwa sana ya Kumpoteza Jasiri Muongoza Njia Ruge Mutahaba hivyo sidhani kama tunataka tena Kupatwa na Msiba mwingine wa Kujitakia kama siyo wa Kujilazimisha wa Bondia kutoka nchini Tanzania.
Hivi kweli Bondia ambaye Bajeti yake nzima ya Chakula cha Siku haizidi hata Tsh 7,500/= anaweza kweli Kupambana / Kupigana na Bondia ambaye ' Breakfast ' yake tu ni Mishahara ya Mwezi kwa Wafanyakazi wa Wizara moja nzima nchini Tanzania?
Pia nitoe RAI Kubwa kwa Serikali kuwa najua fika kwamba Bangi / Bange hairuhusiwi nchini Tanzania ila kama itawezekana naomba huyu Bondia ' Mtafuta Kifo cha lazima ' kutoka nchini Tanzania aitwe na apimwe ' Akili ' na kama kuna Bange / Bangi anayovuta basi ifanyiwe ' Utafiti ' kwani kuna uwezekano hiyo ni aina mpya ya Bange / Bangi ambayo ' Waasisi ' wake akina Hayati Bob Marley na Peter Tosh hawakuicha katika ' mzunguko ' wake hapa duniani.
Hata hivyo simzuii huyu Bondia ' Mtafuta Kifo cha lazima ' kutoka Tanzania kwa kutaka ' Kuzichapa ' na Bondia Bingwa Flyod Myweither wa Marekani kwani hatuwezi jua anajiamini na nini au anapata Kiburi hiki chote wapi ila Mimi GENTAMYCINE namuomba tu kwamba kabla hajapanda Ulingoni hiyo Siku basi awe tayari ameshatuambia ni wapi angependa Tukamzike pale Akifa kama siyo Kufariki kati ya hapa Kinondoni Makaburini au na Yeye tukamlaze Kijijini Kwao. Pia atuambie angependa Mrithi wa Mali zake awe nani na angapenda pia ' akishakufa ' Jeneza lake tulipitishe katika barabara gani za Jiji la Dar es Salaam ili tumkumbuke na Yeye pia.
Nawasilisha.