Serikali kupitia Wizara na Waziri husika Mwakyembe ' chonde chonde ' msiruhusu hili kwani tutapata Msiba mwingine tena!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
38,686
2,000
Jana wakati nikiwa nasikilizika Redio One hasa Kipindi chao cha Michezo nilipatwa na ' Mshtuko ' kidogo pale niliposikia ya kwamba kuna Bondia mmoja nchini Tanzania ( bahati mbaya nimemsahau Jina ila kama kuna anayemkumbuka anisaidie Kumtaja hapa ) tena kwa ' Kujigamba ' kama siyo ' Kujishebua ' kabisa kuwa anataka apambanishwe na Bondia Bingwa duniani Flyod Myweither na ana uhakika kuwa atampiga asubuhi ( mapema ) tu.

Serikali na Waziri Mwakyembe nadhani Tanzania kwa sasa bado tupo katika ' Majonzi ' makubwa sana ya Kumpoteza Jasiri Muongoza Njia Ruge Mutahaba hivyo sidhani kama tunataka tena Kupatwa na Msiba mwingine wa Kujitakia kama siyo wa Kujilazimisha wa Bondia kutoka nchini Tanzania.

Hivi kweli Bondia ambaye Bajeti yake nzima ya Chakula cha Siku haizidi hata Tsh 7,500/= anaweza kweli Kupambana / Kupigana na Bondia ambaye ' Breakfast ' yake tu ni Mishahara ya Mwezi kwa Wafanyakazi wa Wizara moja nzima nchini Tanzania?

Pia nitoe RAI Kubwa kwa Serikali kuwa najua fika kwamba Bangi / Bange hairuhusiwi nchini Tanzania ila kama itawezekana naomba huyu Bondia ' Mtafuta Kifo cha lazima ' kutoka nchini Tanzania aitwe na apimwe ' Akili ' na kama kuna Bange / Bangi anayovuta basi ifanyiwe ' Utafiti ' kwani kuna uwezekano hiyo ni aina mpya ya Bange / Bangi ambayo ' Waasisi ' wake akina Hayati Bob Marley na Peter Tosh hawakuicha katika ' mzunguko ' wake hapa duniani.

Hata hivyo simzuii huyu Bondia ' Mtafuta Kifo cha lazima ' kutoka Tanzania kwa kutaka ' Kuzichapa ' na Bondia Bingwa Flyod Myweither wa Marekani kwani hatuwezi jua anajiamini na nini au anapata Kiburi hiki chote wapi ila Mimi GENTAMYCINE namuomba tu kwamba kabla hajapanda Ulingoni hiyo Siku basi awe tayari ameshatuambia ni wapi angependa Tukamzike pale Akifa kama siyo Kufariki kati ya hapa Kinondoni Makaburini au na Yeye tukamlaze Kijijini Kwao. Pia atuambie angependa Mrithi wa Mali zake awe nani na angapenda pia ' akishakufa ' Jeneza lake tulipitishe katika barabara gani za Jiji la Dar es Salaam ili tumkumbuke na Yeye pia.

Nawasilisha.
 
GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
38,686
2,000
Ha ha ha ha ha my weather ndio anasubiriwa eeee haya tusubiri mtanange
Mpaka sasa hivi najaribu kuwaza tu kwamba huyu Bondia ' Mtafuta Kifo cha lazima ' kutoka nchini Tanzania alikuwa anatania au alimaanisha kweli? Kuna Watu kweli ' wameyachoka ' Maisha yao hapa duniani.
 
Miss Madeko

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
3,901
2,000
Mpaka sasa hivi najaribu kuwaza tu kwamba huyu Bondia ' Mtafuta Kifo cha lazima ' kutoka nchini Tanzania alikuwa anatania au alimaanisha kweli? Kuna Watu kweli ' wameyachoka ' Maisha yao hapa duniani.

Ha ha ha ha hajachoka maisha ya duniani kayachoka ya Tanzania anatafuta yajayo
 
GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
38,686
2,000
Ha ha ha ha hajachoka maisha ya duniani kayachoka ya Tanzania anatafuta yajayo
Najua ' Mtani ' wangu wa Kihaya na ' Boss ' Deogratius Rweyunga wa Radio One yupo sana hapa JamiiForums na ni mmoja wa ' Followers ' wangu wakubwa sana hebu nisaidie ' Mtani ' wako kwa Kuniombe kwa Watangazaji wako wa Michezo Jina la huyo Bondia au waulize pia na wale wa Kipindi cha Michezo cha Capital FM akina Ndokeji wakupe Jina lake huyo Bondia ' Mtafuta Kifo cha lazima ' nchini Tanzania kwani Mimi simkumbuki vizuri. au kama kuna mwana JamiiForums ambaye alikisikiliza Kipindi kile jana na analikumbuka hili Jina la huyu Bondia aliweke hapa tafadhali. Nitashukuru.
 
Mzingo

JF-Expert Member
Nov 2, 2014
1,510
2,000
Mywether hapigi kuua,hupiga ashinde tu. Tofauti na Mfilipino.

Ila Yule bondia Mkurya wa Rorya ndio alikuwa anasema ataua.
 
Baba jay'rose

JF-Expert Member
Jun 29, 2015
1,129
2,000
Jana wakati nikiwa nasikilizika Redio One hasa Kipindi chao cha Michezo nilipatwa na ' Mshtuko ' kidogo pale niliposikia ya kwamba kuna Bondia mmoja nchini Tanzania ( bahati mbaya nimemsahau Jina ila kama kuna anayemkumbuka anisaidie Kumtaja hapa ) tena kwa ' Kujigamba ' kama siyo ' Kujishebua ' kabisa kuwa anataka apambanishwe na Bondia Bingwa duniani Flyod Myweither na ana uhakika kuwa atampiga asubuhi ( mapema ) tu.

Serikali na Waziri Mwakyembe nadhani Tanzania kwa sasa bado tupo katika ' Majonzi ' makubwa sana ya Kumpoteza Jasiri Muongoza Njia Ruge Mutahaba hivyo sidhani kama tunataka tena Kupatwa na Msiba mwingine wa Kujitakia kama siyo wa Kujilazimisha wa Bondia kutoka nchini Tanzania.

Hivi kweli Bondia ambaye Bajeti yake nzima ya Chakula cha Siku haizidi hata Tsh 7,500/= anaweza kweli Kupambana / Kupigana na Bondia ambaye ' Breakfast ' yake tu ni Mishahara ya Mwezi kwa Wafanyakazi wa Wizara moja nzima nchini Tanzania?

Pia nitoe RAI Kubwa kwa Serikali kuwa najua fika kwamba Bangi / Bange hairuhusiwi nchini Tanzania ila kama itawezekana naomba huyu Bondia ' Mtafuta Kifo cha lazima ' kutoka nchini Tanzania aitwe na apimwe ' Akili ' na kama kuna Bange / Bangi anayovuta basi ifanyiwe ' Utafiti ' kwani kuna uwezekano hiyo ni aina mpya ya Bange / Bangi ambayo ' Waasisi ' wake akina Hayati Bob Marley na Peter Tosh hawakuicha katika ' mzunguko ' wake hapa duniani.

Hata hivyo simzuii huyu Bondia ' Mtafuta Kifo cha lazima ' kutoka Tanzania kwa kutaka ' Kuzichapa ' na Bondia Bingwa Flyod Myweither wa Marekani kwani hatuwezi jua anajiamini na nini au anapata Kiburi hiki chote wapi ila Mimi GENTAMYCINE namuomba tu kwamba kabla hajapanda Ulingoni hiyo Siku basi awe tayari ameshatuambia ni wapi angependa Tukamzike pale Akifa kama siyo Kufariki kati ya hapa Kinondoni Makaburini au na Yeye tukamlaze Kijijini Kwao. Pia atuambie angependa Mrithi wa Mali zake awe nani na angapenda pia ' akishakufa ' Jeneza lake tulipitishe katika barabara gani za Jiji la Dar es Salaam ili tumkumbuke na Yeye pia.

Nawasilisha.
Hivi bondia huyo ndio yule aliyekua anatoa mimacho jana???? Maana nimecheka saana baada ya kusoma hii post..salute mzee!!
 
Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
1,800
2,000
Kuna bondia wa Tanzania anaitwa Rogers Mtagwa alipigana New York miaka kadhaa nyuma. Alikuwa anatandikwa ngumi hatari kila round ila jamaa alikomaa tu alikataa kwenda chini. Ukumbi mzima ulikuwa unamshangilia. Alikuja kushindwa kwa points.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom