Serikali kupitia upya sera ya kilimo iliyopo sasa kwani ndio chanzo cha wakulima kuwa maskini

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,402
Serikali imesema sera iliyopo ya sekta ya kilimo inayotumika sasa, ndiyo cha chanzo cha wakulima kuwa masikini kutokana na kuwatumikisha wananchi kuilisha nchi na matajiri, huku wakiwa wanakabiliwa na changamoto kubwa.

Kutokana na hali hiyo, imesema sera imepitwa na wakati ambapo wizara imelazimika kuanza kuipitia upya na kuondoa changamoto na vikwazo kwa wakulima.

Bashe ametoa kauli hiyo Jumamosi Agosti 3, 2019 wakati akifungua maonesho ya Nanenane Mikoa ya Kagera, Geita na Mwanza yaliyofanyika viwanja vya Nyamhongoro jijini Mwanza ambapo aliwapiga marufuku wakuu wa wilaya na mikoa kuwazuia wakulima kuuza chakula chao kwa kuhofia uwepo wa njaa.

Alisema kila mkulima, anajua namna anavyotunza na kuilisha familia yake hivyo kama kuna kiongozi anahofia uwepo wa njaa ni vema akanunua mazao hayo kwa bei anayotaka mkulima na kuyatunza ili yaweze kusubiria dhana aliyoiweka kichwani kwake, kwamba kutakuwapo na uhaba wa chakula.

"Nataka niwaulize hata kama tumejaza mahindi hiki kiwanja chote kama hamna hela ya kuyanunua hayo mahindi yatawasaidia? Wakulima wanalima mazao ya kilimo, ya chakula na ya biashara ili kupata uwezo wa mifuko yao.”

"Hatuwezi kujenga viwanda wakati wakulima ni masikini, haiwezekani na ili wakulima waweze kupata fedha ni lazima tuwaruhusu kufanya biashara za mazao yao pale ambapo wanaweza kuuza mazao yao,” alisema Bashe

“Sera iliyopo imepitwa na wakati kabisa, inawaumiza wakulima na kuwafanya kubaki kila mwaka kuilisha nchi na matajiri huku wao wakibaki na umasikini wao huku kukiwapo na utitiri wa taasisi nyingi ambazo ukichunguza zimeanzishwa kwa lengo la kuwakandamiza, hii haiwezekani kama wizara tumeanza kuangalia ni taasisi gani zinatakiwa kufutwa na kubaki chache.

“Fedha ambazo zilikuwa zikielekezwa kwenye utitiri wa taasisi hizo, zitaelekezwa katika mfuko maalum ambo wizara tunatarajia kuanzisha na kazi ya mfuko huo ni kufidia mkulima pale inapotokea mtikisiko wa bei katika soko la dunia, kama serikali hatuna uwezo wa kuthibiti bei ya soko la dunia, mfuko huo ndio utakaokuwa na kazi ya kutafuta fedha kwa ajili ya kuwafikia wakulima,”alisema.

Alisema Serikali ilikuwa ikipokea fedha nyingi kutoka mataifa ya nje ili kuendeleza kilimo, lakini zilikuwa zikishia katika semina mafunzo kwa watendaji, huku asilimia 50 ya fedha zilizokuwa zikipokelewa ndizo zinafika kwa wakulima.
 
Niliwahi kusema Wakulima nchini hawataweza kufanikiwa pasipo kwanza kupiga marufuku
Kangomba!
 
Kwa speed 360 alioanza nayo Mh Hussein Mohamed Bashe ya kutetea wananchi wa hali ya chini, hasa wakulima, ataishia kupigwa vita mubashara badala ya kuungwa mkono. Tulishuhudia wabunge wa CCM waliotetea wakulima wa Korosho waliionja sekeseke.

Na watakaompiga vita Mh Bashe ni CCM wenyewe, maana hawaeleweki, kuna mwenzao aliwatetea waandishi wa habari (Ishu ya Clouds) alionja sekeseke sambamba na kunyooshewa bastola mchana kweupe, wana lumumba wenye njaa na madaraka watasimamia SHOW ili atumbuliwe mtu mwingine achukue kigoda chake.
 
Big up Bashe mwanzo nzuri sana. Wakulima wa nchi hii unaanza kuwapa matumaini. Very good
 
Wakulima hawawezi Shiba matumaini.Policy Sio Sheria.Kama policy bovu tupa jalalani toa tu maelekezo Nini kifanyike wakulima watoke hapo walipo halafu uendelee na kulitengeneza Hilo policy lako huko kwenye ofisi.
 
Kwa taarifa yako policies zote zimetungwa na wasomi wabobezi na hazikutungwa kwa bahati mbaya!
 
Unajua hii nchi ina sera za hovyo sana kwa wakulima. Hili suala lilikuwa linawafanya wakulima wanyonge kwamba kazi yao ni kuzalisha chakula halafu kukiweka kwa jili ya kutatua shida ya njaa. Yaani mkulima unalima kibiashara lakini unazuiwa kuuza eti kuna njaa, sasa hiyo njaa mimi inanihusu nini na mazao yangu? Kama una njaa njoo ununue au kama umehisi kaya fulani itakuwa na njaa waambie wanunue au walime na sio kuja kumuonea mwingine kwa hoja za kijinga.
Sera za nchi zinachekesha sana halafu tunatarajia wawekezaji waje. Hahahahaha....Yaani mtu analima ekari 2000 za mahindi halafu kesho mnamwambia hauruhusiwi kuuza nje ya nchi kwa sababu hali ya hewa wanasema kutakuwa na njaa. Kama kutakuwa na njaa basi nyie mnunue kwa bei ya soko napo mnapanga bei zenu na mahesabu yenu ya uzalishaji mnajipigia. Unakuta mtu kalima kisasa kabisa na kila kilo moja inagharimu Tsh. 600 halafu nyie mnataka kununua kwaTsh. 550, huu ni upunguani na hatuwezi kuendelea mbele kwa sera hizi na akili hizi. Tunahitaji wawekezaji wakubwa wenye nguvu kwenye kilimo ila kwa sera zetu kwamba mkulima ndio amlishe tajiri wakati wa njaa ni uonevu mkubwa.
Mwaka fulani wakati wa kikwete nilishuhudia mama fulani mfanyabiashara Iringa akilia kilio kikubwa kabisa akimbembeleza mkuu wa Mkoa aruhusu asafirishe mahindi yake ambayo yalikuwa ni tani nyingi sana tena akimwambia benki watauza nyumba yangu nimechukua mkopo lakini wao wakwambia kwamba kuna suala la njaa hautaruhusiwa kuuza huko nje ya nchi. Wakati huyu ananyanyaswa kwenye biashara yake kwa kuwatetea hao wanaosemekana watakufa njaa, wanaotetewa wanaendelea na biashara zao kama kawaida ila mkulima ananyanyaswa.
Iko hivi, bila kuwa na sera za kuwavutia wakulima wakubwa wakubwa kuja kuwekeza Tanzania suala la njaa litaendelea kuwepo kwa sababu watu wengi wamekata tamaa ya kulima TZ.

Ila Bashe jiandae kwa sababu watakupiga vita na utaondolewa hapo. Hili kundi la wapigaji hawapendi watu wakweli wenye malengo ya kuwasaidia watanzania. Wamekaa kwa upigaji tu.
Nilipenda kauli ya Magufuli kwamba mwenye njaa akalime na sio kuwaonea wakulima na kwamba wakulima wauze biashara zao kokote
 
Kama "Wakulima wanatumikishwa kwa ajiri ya Chakula cha Nchi na Matajiri " so kwanini Serikali isiwape wakulima wake hasa wanaozalisha kwa tija incentives, hapo maana yake serikali na wakulima watakua wanalima, sio sasa analima mkulima peke yake alafu mazao ni ya Serikali.
 
Kwa speed 360 alioanza nayo Mh Hussein Mohamed Bashe ya kutetea wananchi wa hali ya chini, hasa wakulima, ataishia kupigwa vita mubashara badala ya kuungwa mkono. Tulishuhudia wabunge wa CCM waliotetea wakulima wa Korosho waliionja sekeseke.

Na watakaompiga vita Mh Bashe ni CCM wenyewe, maana hawaeleweki, kuna mwenzao aliwatetea waandishi wa habari (Ishu ya Clouds) alionja sekeseke sambamba na kunyooshewa bastola mchana kweupe, wana lumumba wenye njaa na madaraka watasimamia SHOW ili atumbuliwe mtu mwingine achukue kigoda chake.
ANATAKA KUWALAZA NJAA MABOSI WAKE WALIOMPA CHEO 😂😂😂😂 MABOSI KATIKA MWAKA MZIMA WENYE MIEZI 12 WAO MWEZI 1 TU UNAWALIPA NA KUSTAREHE MENGINE YOTE 11 WAKISUBIRIA MSIMU WA MAVUNO WAKANYONYE....
 
Wakulima hawawezi Shiba matumaini.Policy Sio Sheria.Kama policy bovu tupa jalalani toa tu maelekezo Nini kifanyike wakulima watoke hapo walipo halafu uendelee na kulitengeneza Hilo policy lako huko kwenye ofisi.
lakini bashe ameeleza mambo ambayo hayafai. Hiyo ni ishara nzuri kwamba kinachochangia kuwakwamisha wakulima sasa policy na decision makers wanakijua na kuna hatua wanachukua. Labda ndio utaratibu wa serikali kuanza kwanza na Sera!!
 
Mambo ya tuko mbioni kufanya hili na hili.Hizo mbio dead line lini nobody knows.Lakin wananchi eleweni tu tuko mbioni kutunga policy mpya!!!!! Huku wakulima wanaendelea kuumia
 
Kula tano mkuu... Umemaliza kila kitu hii nchi ina mambo ya ajabu sanaa..
Unajua hii nchi ina sera za hovyo sana kwa wakulima. Hili suala lilikuwa linawafanya wakulima wanyonge kwamba kazi yao ni kuzalisha chakula halafu kukiweka kwa jili ya kutatua shida ya njaa. Yaani mkulima unalima kibiashara lakini unazuiwa kuuza eti kuna njaa, sasa hiyo njaa mimi inanihusu nini na mazao yangu? Kama una njaa njoo ununue au kama umehisi kaya fulani itakuwa na njaa waambie wanunue au walime na sio kuja kumuonea mwingine kwa hoja za kijinga.
Sera za nchi zinachekesha sana halafu tunatarajia wawekezaji waje. Hahahahaha....Yaani mtu analima ekari 2000 za mahindi halafu kesho mnamwambia hauruhusiwi kuuza nje ya nchi kwa sababu hali ya hewa wanasema kutakuwa na njaa. Kama kutakuwa na njaa basi nyie mnunue kwa bei ya soko napo mnapanga bei zenu na mahesabu yenu ya uzalishaji mnajipigia. Unakuta mtu kalima kisasa kabisa na kila kilo moja inagharimu Tsh. 600 halafu nyie mnataka kununua kwaTsh. 550, huu ni upunguani na hatuwezi kuendelea mbele kwa sera hizi na akili hizi. Tunahitaji wawekezaji wakubwa wenye nguvu kwenye kilimo ila kwa sera zetu kwamba mkulima ndio amlishe tajiri wakati wa njaa ni uonevu mkubwa.
Mwaka fulani wakati wa kikwete nilishuhudia mama fulani mfanyabiashara Iringa akilia kilio kikubwa kabisa akimbembeleza mkuu wa Mkoa aruhusu asafirishe mahindi yake ambayo yalikuwa ni tani nyingi sana tena akimwambia benki watauza nyumba yangu nimechukua mkopo lakini wao wakwambia kwamba kuna suala la njaa hautaruhusiwa kuuza huko nje ya nchi. Wakati huyu ananyanyaswa kwenye biashara yake kwa kuwatetea hao wanaosemekana watakufa njaa, wanaotetewa wanaendelea na biashara zao kama kawaida ila mkulima ananyanyaswa.
Iko hivi, bila kuwa na sera za kuwavutia wakulima wakubwa wakubwa kuja kuwekeza Tanzania suala la njaa litaendelea kuwepo kwa sababu watu wengi wamekata tamaa ya kulima TZ.

Ila Bashe jiandae kwa sababu watakupiga vita na utaondolewa hapo. Hili kundi la wapigaji hawapendi watu wakweli wenye malengo ya kuwasaidia watanzania. Wamekaa kwa upigaji tu.
Nilipenda kauli ya Magufuli kwamba mwenye njaa akalime na sio kuwaonea wakulima na kwamba wakulima wauze biashara zao kokote
 
Mambo ya tuko mbioni kufanya hili na hili.Hizo mbio dead line lini nobody knows.Lakin wananchi eleweni tu tuko mbioni kutunga policy mpya!!!!! Huku wakulima wanaendelea kuumia
Policy nzuri ndiyo dira, ndiyo muelekeo... Lakini kwa kuwa ninyi sasa mnaendesha nchi kwa matamko ya majukwaani ya mtu kamwe hamuwezi kuona umuhimu wa kuwa na sera nzuri...
 
Kilimo Kwanza iliishia wapi?
Tutakuwa watu wa kuja na policies mpya day in day out.
Au ndio tuseme kila awamu itaingia na kuondoka na policy zake?
Ni wapi tunakosea kwenye implementation ya hizi policies tunazozindua kila Mara?
 
Mambo ya tuko mbioni kufanya hili na hili.Hizo mbio dead line lini nobody knows.Lakin wananchi eleweni tu tuko mbioni kutunga policy mpya!!!!! Huku wakulima wanaendelea kuumia
ndugu yangu sasa unafikiri wataanzaje kurekebisha mapungufu haya?!?!
 
Back
Top Bottom