Serikali kupitia TCRA yavifungia Vituo vya Redio na TV vikiwemo Star TV, Uhuru FM, RFA...

Mtini

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
1,491
2,355
Mamlaka ya mawasiliano nchini Tanzania, TCRA leo imevifungia vituo 21 vya Radio na 6 vya Television kwa muda wa miezi 3 kikiwemo kituo cha Star TV, Radio free Afrika, Kiss Fm na Uhuru FM.

=======
UFAFANUZI
=======
Wamefungiwa kutoa huduma kwa miezi 3 kutolipa ada/kodi

Mwezi July 2015 ilitolewa taarifa kwa umma na TCRA kwamba baadhi ya radio na Televisheni zipatazo 40 zinadaiwa ada na tozo mbalimbali.

Septemba 28 wakapewa onyo la mwisho kwamba hadi Tar 31 dec wawe wamelipa ada zao. Wengine wakalipa Jan 4. Wengine wakakausha.

Kwa mujibu wa sheria unapokua hujalipa kodi TCRA wanakuchukulia kuwa wewe haupo.

TCRA wanasema hata miezi 3 ya adhabu ikiisha na bado hamjalipa, further actions kama kunyang'anywa leseni kunaweza kutokea.

Ni vituo 11 tu kati ya vituo vilivyokuwa vinadawa na mamlaka vilitii.

Sasa basi TCRA wanasema kuanzia Jumatatu tar 18, Radio 21 na TV 6, vituo hivi havitatakiwa kuwa hewani kufanya kazi kutokana na tamko la Mkurugenzi wa TCRA

1. Sibuka FM
2. Breez FM
3. Country FM
4. Ebony FM
5. Hot FM
6. Impact FM
7. Iringa Municipal TV
8. Kiss FM
9. Kitulo FM
10. Kifimbo FM
11. Mbeya City Municipal TV
12. Radio 5
13. Radio Free Afrika (RFA)
14. Musa Television Network
15. Pride FM radio
16. Radio Huruma
17. Radio Uhuru
18. Star TV
19. Rock FM Radio
20. Standard FM radio
21. Sumbawanga Municipal TV
22. Tanga City TV
23. Top Radio FM limited
24. Ulanga FM
 
# Habari Mamlaka ya mawasiliano nchini Tanzania TCRA leo imevifungia vituo 21 vya Radio na 6 vya Television kwa muda wa miezi 3 kikiwemo kituo cha Star TV,Radio free Afrika,Kiss Fm na Uhuru FM,Zaidi utafahamu kupitia Taarifa yetu ya habari Sambili usiku.

Chanzo: ITV
Kuanzia lini mkuu? Niandikavyo nasikiliza RFA
 
Back
Top Bottom