Serikali kupeleka Sh. 18.77 bilioni kila mwezi shule za sekondari na msingi, kugharamia elimu

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
SERIKALI imepanga kupeleka Sh. 18.77 bilioni kila mwezi katika shule za sekondari na msingi kwa ajili ya kugharamia elimu ili kutekeleza dhana ya elimu bure kuanzia Januari, 2016.

Taarifa hiyo ilitolewa Mjini Dodoma jana na Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa elimu bure.

Alianisha fedha zitakazotolewa na Serikali kwa ajili ya kugharamia elimu ni pamoja na gharama za mitihani ya kidato cha nne ambazo zitatolewa moja kwa moja na Serikali katika Baraza la Mitihani (Necta).

“Serikali itatoa pia ruzuku ya uendeshaji wa shule Sh. 10,000 kwa shule za msingi na Sh. 25,000 kwa shule za sekondari kwa kila mwanafunzi kwa mwaka.

“Vilevile itatoa Sh. 1,500 kwa siku kwa mwanafunzi kwa shule za msingi na sekondari kwa ajili ya chakula kwa wanafunzi wanaokaa bweni,” amesema.
Simbachawene amesema pia Serikali itatoa fedha kwa ajili ya fidia ya ada Sh. 20,000 kwa kila mwanafunzi wa shule ya kutwa na Sh. 70,000 kwa mwanafunzi wa sekondari kwa mwaka.

Amesema fedha za ruzuku ya uendeshaji wa shule zitasaidia pia uendeshaji wa shule za hosteli ikiwemo gharama za chakula, mlinzi, mpishi, umeme na maji.

Aliwaagiza wakurugenzi wa halmashauri husika kuhakikisha fedha hizo zinafika kwa wakati na zinatumika kwa kazi iliyokusudiwa.

Simbachawene amesema majukumu ya wazazi pamoja na mambo mengine yatakuwa ni kununua sare za shule, vifaa vya kujifunzia, gharama za matibabu, nauli, gharama za chakula kwa wanafunzi wa shule za kutwana kununua magodoro, shuka, vifaa vya usafi binafsi kwa wanafunzi wa bweni.

“Natoa wito kwa viongozi wote wakiwemo wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa kusimamia utekelezaji wa elimu bila malipo,” amesema.

Aidha, Simbachawene aliziagiza halmashauri na mikoa ambayo haikufanya vizuri katika mitihani ya darasa la saba kujieleza sababu za kutofanya vizuri.

“Iwapo itathibitika kwamba kuna wahusika walizembea kutimiza majukumu yao wachukuliwe hatua zinazostahili.

“Nawaagiza pia wakurugezi mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma kwamba ifikapo Februari 15 mwakani wawe wamekamilisha miundombinu ya shule ili wawewezeshe wanafunzi 12,647 waliosalia kujiunga na elimu ya sekondari wanaenda shule,” amesema.
Simbachawene pia alizitaka kamati za ulinzi na usalama za mikoa na wilaya kuwachukulia hatua za kisheria watu watakaosababisha wanafunzi kukatisha masomo kwa utoro na mimba pamoja na wale waliooa watoto wa kike.

‘’Tusifanye kazi kwa mazoea, tunatakiwa tuendane na kasi ya Rais John Magufuli ya kufanya kazi kuwasaidia wananchi hasa katika sekta ya elimu,’’ amesema.

Chanzo: Mitandaoni
 
waangalie kwa umakini utaratibu wa kutoa na ku evaluate usefulness ya hizo pesa
kwani kisije kuwa ni kichaka kipya cha watu kuponda raha .
 
Ni fedha kidogo mno. Hazifiki hata dola milioni 10 kwa mwezi. Ruzuku ya shilingi 10,000 kwa mwanafunzi kwa mwaka itatosha kuchimba vyoo vinavyohitajika? Huko kwenye shule za msingi wanatumia choo kimoja wanafunzi wengi sana pamoja na waalimu wao. Na kuna kipindupindu. Lazima sasa tuwe na vyoo na maji safi ya kunawa mikono na kunywa kwenye kila shule ya msingi. Bla bla ziachwe.

Inatakiwa 20 - 25% ya bajeti yote itumike kwenye elimu.
 
Sijaona ya madawati, na madawati yetu haya ni disposable mwaka mmoja kwisha habari yake. Mi naona serikali ingechonga madawati ya vyuma na meza kama za sekondari zile za zamani hapo unakuwa mkataba.

Yale hata miaka kumi yana survive lkn hizi za mbao za mnazi. TUSUBIRI
 
Hapa tunasubiri utekelezaji tuu, kazi ipo mwaka huu. Wapigaji wote naona wanakuna vitambi na Mabwana jela wanaongeza majengo ya jela.

Ila 1500 ajili ya chakula kwa wanafunzi wa Bweni sijaelewa vizuri. Ni hatua nzuri ngoja tusubiri utekelezaji.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Utaelewa tu Kaka yangu Mkubwa..ni kama hivi..kama unaye mwananfunzi anayesoma msingi au sekondari. Kumbuka ruzuku kwa mwananfunzi kwa mwaka ni elefu 10 tu. Hiyo ndio capitation yenyewe. Sasa endelea kujiuliza kuhusu vifaa vya kufundishia kama chaki vile, maandalio ya somo, makaratsi kwa ajili ya mitihani ya majaribio, kuchapisha mitihani pia..few to mention. Kuhusu vyakula vya mchana kwa wanafunzi wa kutwa na wale wa shule za msingi fedha za ulinzi, maji "mzazi atachangia" i.e mzazi ampe hela ya mwanaye akale shuleni..with assumption that kila mzazi anao uwezo wa kufanya hilo..though serikali haiwezi kugharamikia kila kitu..ila ELIMU NI BUREE...tafakari
 
Hivi vifaa vya kujifunzia si ndo matatizo kwa wazazi hii? Hapo ndo watoto watatumwa ream za A4 kumi kila muhula! Hivi Magufuli aliposema "nataka iwe bure na iwe bure kweli kweli" alimaanisha nini?
 
Ni fedha kidogo mno. Hazifiki hata dola milioni 10 kwa mwezi. Ruzuku ya shilingi 10,000 kwa mwanafunzi kwa mwaka itatosha kuchimba vyoo vinavyohitajika? Huko kwenye shule za msingi wanatumia choo kimoja wanafunzi wengi sana pamoja na waalimu wao. Na kuna kipindupindu. Lazima sasa tuwe na vyoo na maji safi ya kunawa mikono na kunywa kwenye kila shule ya msingi. Bla bla ziachwe.

Inatakiwa 20 - 25% ya bajeti yote itumike kwenye elimu.
Choo ni sehemu ya jengo na kinatakiwa kuwepo, haiwezi ikawekea bajeti kila mwezi.
Shule kutokuwa na choo ni tatizo jingine na halihusiani na hiyo 10,000
 
Namshukuru JPM kwa kuandaa majipu mengine mengi mno! Huu mchakato wa elimu bure, sion wapi elimu imekuwa bure kama wanavyojidai bana!

Kwanza hii dhana ya elimu bure nini maana yake?! Ni ili kuongeza idadi ya wanafunzi au kuongeza ufaulu au ni kuwapunguzia wazazi mzigo wa kulipa ada?! Napata wakati mgumu sana jinsi ambavyo scientific issues zinatatuliwa politically! Nachelea kusema kwamba huu mpango wao ni siasa tu na hakuna ukombozi wowote kwenye elimu yetu ambayo ipo ICU!

Ni mtazamo tu!!

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Dah kichefuchefu! Mimi nilisoma sekondari ya serikali bweni nililipa tshs 70000 kwa mwaka! Na hiyo nilianza mwaka 2002! Leo wanapeleka 10000 kwa mwaka na gharama zote zilivyopanda?

Nasubiri matokeo ya vidato mwakani anyway!!
 
Namshukuru JPM kwa kuandaa majipu mengine mengi mno! Huu mchakato wa elimu bure, sion wapi elimu imekuwa bure kama wanavyojidai bana!

Kwanza hii dhana ya elimu bure nini maana yake?! Ni ili kuongeza idadi ya wanafunzi au kuongeza ufaulu au ni kuwapunguzia wazazi mzigo wa kulipa ada?! Napata wakati mgumu sana jinsi ambavyo scientific issues zinatatuliwa politically! Nachelea kusema kwamba huu mpango wao ni siasa tu na hakuna ukombozi wowote kwenye elimu yetu ambayo ipo ICU!

Ni mtazamo tu!!

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
Mkuu ultaka na uniform za mwanao ziwe buree anunuliwe na serikali.?kutoa pesa za ada na examination fees mbna,hulipii chalk wala dawati,hvi ultaka nn kikubwa ili ujue ni buree..
 
Ni fedha kidogo mno. Hazifiki hata dola milioni 10 kwa mwezi. Ruzuku ya shilingi 10,000 kwa mwanafunzi kwa mwaka itatosha kuchimba vyoo vinavyohitajika? Huko kwenye shule za msingi wanatumia choo kimoja wanafunzi wengi sana pamoja na waalimu wao. Na kuna kipindupindu. Lazima sasa tuwe na vyoo na maji safi ya kunawa mikono na kunywa kwenye kila shule ya msingi. Bla bla ziachwe.

Inatakiwa 20 - 25% ya bajeti yote itumike kwenye elimu.
10millions USD
 
Sijaona ya madawati, na madawati yetu haya ni disposable mwaka mmoja kwisha habari yake. Mi naona serikali ingechonga madawati ya vyuma na meza kama za sekondari zile za zamani hapo unakuwa mkataba.

Yale hata miaka kumi yana survive lkn hizi za mbao za mnazi. TUSUBIRI
Mazuri ni ya plastic kutoka china bei chee kabisa
 
Utaelewa tu Kaka yangu Mkubwa..ni kama hivi..kama unaye mwananfunzi anayesoma msingi au sekondari. Kumbuka ruzuku kwa mwananfunzi kwa mwaka ni elefu 10 tu. Hiyo ndio capitation yenyewe. Sasa endelea kujiuliza kuhusu vifaa vya kufundishia kama chaki vile, maandalio ya somo, makaratsi kwa ajili ya mitihani ya majaribio, kuchapisha mitihani pia..few to mention. Kuhusu vyakula vya mchana kwa wanafunzi wa kutwa na wale wa shule za msingi fedha za ulinzi, maji "mzazi atachangia" i.e mzazi ampe hela ya mwanaye akale shuleni..with assumption that kila mzazi anao uwezo wa kufanya hilo..though serikali haiwezi kugharamikia kila kitu..ila ELIMU NI BUREE...tafakari
Sijaona mahali hiyo kitu. Vifaa vya kujifunzia sio vya kufundishiwa (mwanafunzia anhitaji madaftari, kalamu, penseli, vifutio etc). Hizo chaki na mengineyo hivyo ni vya kufundishia sio gharama ya mzazi!Chakula kwa wanafunzi wa kutwa wataenda kukikuta nyumbani kwao, mzazi amuandalie mwanae chakula
 
Namshukuru JPM kwa kuandaa majipu mengine mengi mno! Huu mchakato wa elimu bure, sion wapi elimu imekuwa bure kama wanavyojidai bana!

Kwanza hii dhana ya elimu bure nini maana yake?! Ni ili kuongeza idadi ya wanafunzi au kuongeza ufaulu au ni kuwapunguzia wazazi mzigo wa kulipa ada?! Napata wakati mgumu sana jinsi ambavyo scientific issues zinatatuliwa politically! Nachelea kusema kwamba huu mpango wao ni siasa tu na hakuna ukombozi wowote kwenye elimu yetu ambayo ipo ICU!

Ni mtazamo tu!!

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
Huu uliandaliwa kisiasa kwa ajili ya kampeni.nakumbuka james mbatia alisema kuwa ukawa ingetenga trillion 4 kwa ajili ya elimu bure.
 
Back
Top Bottom